Lowasa kusomewa mashtaka mapya Zanzibar

Lowasa kusomewa mashtaka mapya Zanzibar

b2015

Member
Joined
Nov 14, 2013
Posts
42
Reaction score
22
Nimeshindwa kuweka link mwenye kuweza aende kwenye Twitter ya absolam kibanda kuna hii habari,vilevile kubenea kafichua njama za kumfukuza uanachana Lowasa.
 
mashtaka gani ?? lini alisomewa mashtaka ya zamani zanzibar na hayo mapya ni ya lini tena?
 
Hayo ya zamani ni yapi? Hakuna awezaye kumgusa Edo Lowasa pale Lumumba. Yule ni samaki mkavu banaa huwezi kumtafuna mzima mzima upone. Atakaye peleka kihere here chake kule aende na kadi yake ya chama kwani itachanwa na atatupwa nje.
Mwaiona CCM kuwa ni mbumbumbu sana? Wamtimue yeye ambaye ushindi wake ni lazima? Well wish to yu EDOOOO my next president.
Tungojee tuone CCM ikimtupa. Ni sawa na kuchezea shilingi yako chooni tena cha shimo
 
Kwa mujibu wa Kibanda Kesho ndo mashtaka mapya atasomewa
 
Afukuzwe tu kwani ana faida gani? Cha kushangaza wanaokuwa na hofu ni Kibanda na Kubenea ambao walikuwa wanufaika wa fedha za Fisadi Lowasa

Wewe unanufaika na za wa-commoro ndo maana unam-diss. Na huyu Mende wako hapati kitu nyambafu.
 
Mkakati wa kumfukuza Lowassa CCM waiva

Posted by:-Saed Kubenea-57 mins ago0 Comments-57 Views

MBUNGE wa Monduli, Edward Ngoyai Lowassa, aweza kuvuliwa uwanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), muda wowote kutoka sasa.-Saed Kubenea, anaripoti.

Hoja ya kumvua uwanachama Lowassa imepangwa kuwasilishwa katika kikao cha Kamati Kuu (CC), kinachotarajiwa kufanyika Jumanne wiki hii, mjini Zanzibar.

Taarifa kutoka ndani ya chama hicho zinasema, mkakati wa kumvua uwanachama Lowassa, unasukwa kwa ustadi mkubwa na baadhi ya viongozi wandamizi ndani ya CCM ili kumzua kutimiza ndoto yake ya kuwa rais.

“Ni lazima tumfukuze uwanachama katika chama chetu. Hakuna namna nyingine ya kukinusuru chama hiki,” ameeleza kiongozi mmoja mwandamizi ndani ya chama hicho.

Amesema, “Bwana huyu (Lowassa), amekuwa akikivuruga chama chetu kwa muda mrefu. Tumemvulia, lakini sasa tumechoka. Nilazima tumuondoe ili kukinusuru chama chetu.”

Ajenda ya kumfukuza Lowassa kutoka ndani ya chama hicho, imejificha katika kinachoitwa, “Tathmini hali ya kisasa kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka huu.”

Lowassa alikuwa waziri mkuu wa kwanza katika serikali ya Jakaya Kikwete. Anatajwa kuwa miongoni mwa makumi ya wanachama wa CCM waliotangaza au kutajwa, kusaka urais kwa udi na uvumba katika uchaguzi mkuu ujao.

Januari mwaka jana, Lowassa na makada wenzake kadhaa walipewa “onyo” kwa kile kilichoitwa, “kuanza kampeni kabla ya muda kufika.”

Mtoa taarifa wa gazeti hili anasema, kabla ya kikao cha CC, kutafanyika kikao cha Kamati Ndogo ya Maadili na Nidhamu, ambacho kitafanya tathmini ya adhabu zilitolewa kwa Lowassa na wenzake.

Lowassa anatuhumiwa kuendelea na mkakati wake wa kampeni kwa kukusanya watu na kujipanga kwa ajili ya uchaguzi mkuu ujao, jambo ambalo viongozi wake wakuu wanamtuhumu kukipasua chama chao.

Anasema, kikao cha CC kitatekeleza mradi huo kwa kutumia ripoti zilizotengenezwa na timu za maofisa usalama wa chama hicho, zilizotumwa mikoa yote ili kukusanya kile kilichoitwa, “mkakati wa Lowassa wa kusaka urais.”

Kutokana na hali hiyo, Kamati Kuu iliitaka Kamati ya Maadili kufanya marejeo na kuangalia utekelezaji wa adhabu kwa makada
 
hizi issue za lowassa zinaboa sasa, si msubiri wamalize tuone matokeo?
 
Afukuzwe tu kwani ana faida gani? Cha kushangaza wanaokuwa na hofu ni Kibanda na Kubenea ambao walikuwa wanufaika wa fedha za Fisadi Lowasa

Mbona ukisikia jina la EL unaweweseka sana? We si ndie uliyesema akifukuzwa atapata umaarufu? Mbona umebadili tena msimamo wako?
 
Afukuzwe tu kwani ana faida gani? Cha kushangaza wanaokuwa na hofu ni Kibanda na Kubenea ambao walikuwa wanufaika wa fedha za Fisadi Lowasa

Damu ya mzee warioba inaanza kukutafuna.


swissme
 
Afukuzwe tu kwani ana faida gani? Cha kushangaza wanaokuwa na hofu ni Kibanda na Kubenea ambao walikuwa wanufaika wa fedha za Fisadi Lowasa
Shortsighted politician kama wewe ndo utatoa kauli kama hiyo coz uwezo wako nikuangalia maslahi ya tumbo lako na mabwana zako..kwa maslahi ya chama unamfukuza lowassa kwa kosa gani wakati wewe na kutengeneza fitina kama hakubaliki shindaneno nae kwenye kura kama fisadi mlishaimba sana hatachaguliwa.vinginevyo njama zote za kumshinikiza kikwete amfukuze Lowasa hamtafanikiwa na nawaambia hapa msijifanye watakatifu ikiwa Mungu an memchagua Edward Lowassa hats mfute na uraia wake wa nchi kwa Miujiza ya Mungu aliyefanya njia katika shamu ya farao Israel wakavuka Lowasa atainuka na timu yako kutwa vikao vya majungu
 
Kama ccm i-mfukoni mwake watamfukuzaje? Ila itashangaza ulimwengu kama akiteuliwa mpeperusha bendera ya mafisadi wenzie.....ninachokiona hata akipewa nafasi hiyo kwa uroho wa madaraka aliyonayo hatatofautiana na Mwai Kibaki...kukubali kushindwa kwake itakuwa vigumu!
 
Wote mafisadi na wezi hakuna mwenye haki ya kumnyooshea mwenzake kidole.
 
Back
Top Bottom