Lowasa anautaka u Rais kwa nguvu zote

Lowasa anautaka u Rais kwa nguvu zote

Nimeipenda hiyo watanzania ni kumuogopa kama ukoma mtu anayetaka kuingia Ikulu kwa nguvu ambaye yuko tayari kununua cheo kwa gharama yoyote ile , tafsiri yake ni kwamba apewi kwa watu kupenda bali kwa sababu ana nguvu ya kununua !

Hii nimeipenda, ni kweli, sijui kama watu wa makanisani na misikitini wanamuuzia Uraisi au wanachukua pesa zake then waendelee na shughuli zao, au anarejesha fungu la kumi? sijui kama TRA wanachukua kodi kwa pesa hizo zinazomwagwa kama njugu?
 
Hivi kwa akili yako unafikiri LOWASA ndiyo CCM?

Kuna kila dalili kuwa kwa sasa Lowassa atawanyamazisha wote CCM, hivi kweli inaingia akilini waziri aliyejiudhuru kwa kukosa uadilifu akiwa madarakani juzi tunamuona eti naye ni miongoni mwa mawaziri wastaafu CCM tabu tupu
 
Yaani hilo jamaa likigombea urais, tutahamasisha maandamano nchi nzima, limefisad mali ya umma likiwa liwaziri leo ligombee urais tulipe, imekula kwake.
 
Nchi hii ikitokea kama muujiza aichukue Lowasa na mafisadi wenzake cjui itakuwaje kwanza itabaki kuwa kapi, hivi Rostam na Chenge ni wa kuchekea? Yatupasa tukasirike hili Taifa niletu sote hakuna atakayekuja kututetea watanzanzania ktk rasilimali zetu isipokuwa sisi wenyewe, Lowasa shame on you kwann ucihurtmie Tanzania na vizazi vyake kwann ujitazame mwenyewe 2, hizo kodi za watanzania unazorudisha indirect kupitia harambee na mambo mengine kama hayo si kununua cheo
 
Kila kukicha ni makanisani,misikitini,kwa wamachinga,saccos nk..huku akitoa mabilion ya pesa.Najiuliza swali hizi pesa anazitoa wapi? Na kama anavyosema kuwa anatoa kwa marafiki zake ,rafiki zake hao ni akina nani?
Lowasa atakuja kuigawa nchi na atakuwa rais mbovu zaidi ya Jk.Pia hao marafiki zake atakuja kuwalipa nini akipata urais? Hizi ndizo seriali za makundi ya kirafiki na udini,kitu ambacho ni nyayo zile zile za akina Jk.
Lowasa ili tumwamini aweka hadharani kampuni anazomiliki,biashara zake,vinginevyo pesa za EPA NA RICHMOND ZINARUDI KUPITIA MLANGO WA NYUMA.
Lowasa akiwa rais ataligawa taifa hili kwa misingi ya fulani,uthibitisho upo. Jiulize kwanza maswali haya.
1.Kwa nini Monduli ina maendeleo kuliko baadhi ya majimbo mkoani Arusha mfano Arusha? Hapa tutaona economic imbalance between one region and another..kama Jk kuanzia kila kitu Bagamoyo.
2.kwa nn anatumia muda mwingi sana kutoa michango? Alikuwa wapi zamani? Huyu jamaa ni hatari sana
3.Je,pengine kuna ahadi ambazo anazitoa kwa wahusika anaowapa michango,akishindwa kuwatekelezea taifa hili litakuwa wapi? Nyayo zile zile za ahadi za kikwete juu ya mahakama ya kadhi,nitakupa uwaziri mkuu,ooh utakuwa waziri wa fedha n.k yamemshinda anaanza kulalamika.Na EL ndio wale wale,huyu jamaa hawezi kuepuka serikali ya makundi siku akiwa rais kwanza ataanza na marafiki zake wanaompa michango ya harambee,kutimiza ahadi za viongoz wa dini..yakimushinda kitu kile kile kwa Jk.
EL hana uzalendo na taifa hili,si mwadilifu anafuta urais kwa nguvu zote.
Mosi,inawezekana EL akawa ni mtu wa visasi baada ya yeye kujiuzulu kwa shinikizo la Tume iliyoongozwa na Mwakyembe.Hawa waliomfanya ajiuzulu Uwaziri mkuu unafikiri akiwa rais atawafanya nini,na EL ni mtu wa maamuzi magumu.
Pili,inawezekana kafanya mambo mabaya kuliko kawaida hivyo akiwa rais itakuwa ni sehemu ya kujilindia na kuwa na uwezo wa kutunga sheria ya kumkinga hata akiondoka madarakani.Mambo mabaya ambayo pengine alikuwa anafanya alikuwa anakingwa na kulindwa na serikali ya ccm,hivyo basi kwa kuwa walijijengea mtandao wa kushika madaraka na inaonekana mtandao huo unagonga mwamba hana budi kuutaka urais kwa nguvu zote ili iwe kinga kwake.
EL hana nia ya dhati kwa taifa hili,ana uchu wa madaraka,mtuhumiwa wa kampuni hewa(Richmond) iliyokuwa inalipiwa billions of money per day.
 
Mwalimu alishatuonya, kua mtu anayewahi Ikulu inabidi tumuogope kama ukoma. Up to now Magufuli na huyu Bwana "milioni 10' wameshafeli litmus test ya Mwalimu/
 
Mwalimu alishatuonya, kua mtu anayewahi Ikulu inabidi tumuogope kama ukoma. Up to now Magufuli na huyu Bwana "milioni 10' wameshafeli litmus test ya Mwalimu/

mkuu,awataje kwanza marafiki zake ili tujue ni akina nani,sitta alithubutu walianza kumkana hadharani....sasa amebaki yeye
 
mkuu,awataje kwanza marafiki zake ili tujue ni akina nani,sitta alithubutu walianza kumkana hadharani....sasa amebaki yeye
Marafiki zake ni 'wafanyabiashara' wengi wakiwa wahindi na wamangakoko. Hawa nadhani kila mtz mwene akili timamu anajua kua wameshiriki kwa namna moja au nyingine ktk kila grand-corruption in our beloved but crazy bongoland.

Mtu mwengine ambaye anajifanya very vocal na anadhani kua tunahitaji kusikia his 2 cents in every matter in the country ni Sumaye. Huyu ndie aliesema kua "Ukitaka mambo yako (ya uzi) yaende swafi njoo CCM", sasa anataka kutuaminisha kua naye ni masiya wa kututoa utumwani. Huyu bwana hata wenzake wanashindwa kumwambia ukweli kua hana mvuto. lol
 
sisi vijana watanzania tunadhambi kubwa sana ya utumwa, tumekuwa watumwa wa fikra,watumwa wa utu,watumwa wa fedha ndio maana hata akitokea mpuuzi tu akatununulia pombe zile za kienyeji lita moja tu, au bia moja basi tutamshukuru huyo mtu kuwa ni mzuri,anauwezo na anafaa kukabidhiwa madaraka. Ndugu zanguni hususani vijana tubadilike,leo tunaimba wimbo wa kumtukuza Lowasa kutokana na sisi kuijikubali kuwa watumwa, Tufanye kazi kwa bidii, waliopo serikalini vijana wenzetu mbadilike toene huduma kwa jamii na kuweni tufauti na wao na fanya kazi kwa bidii. Tatizo sio umaskini na kama sisi vijana tukaamini ni maskini na ukaamini kuwa EL ndio mkombozi basi utaendelea kubaki maskini hivyo hivyo.wewe ukifuatilia kipindi JK anaingia madarakani vijana walinunuliwa mhindi wa kuchoma tu, basi vijana waligeuka hayawani na kuona kama JK ndio mkombozi.Jamani watanzania Kuna watu wachapakazi wengi sana hapa nchini, tutulie na tutafakari kwa kina sana.
 
Mwalimu alishatuonya, kua mtu anayewahi Ikulu inabidi tumuogope kama ukoma. Up to now Magufuli na huyu Bwana "milioni 10' wameshafeli litmus test ya Mwalimu/

magufuli kafanya nini mbona slaa ametangaza na ametangazwa siku nyingi lakini hujamsema au ndiyo iliko lalia?
 
Marafiki zake ni 'wafanyabiashara' wengi wakiwa wahindi na wamangakoko. Hawa nadhani kila mtz mwene akili timamu anajua kua wameshiriki kwa namna moja au nyingine ktk kila grand-corruption in our beloved but crazy bongoland.

Mtu mwengine ambaye anajifanya very vocal na anadhani kua tunahitaji kusikia his 2 cents in every matter in the country ni Sumaye. Huyu ndie aliesema kua "Ukitaka mambo yako (ya uzi) yaende swafi njoo CCM", sasa anataka kutuaminisha kua naye ni masiya wa kututoa utumwani. Huyu bwana hata wenzake wanashindwa kumwambia ukweli kua hana mvuto. lol

MIMI NAOGOPA KWANI ANYTHING CAN HAPPEN AS LONG AS TUTAENDELEA KUWA KATIBA HII MBOVU PIA KUPUUZWA KWa RASIMU HII ILOJAA MAONI YA WATANZANIA WALIO WENGI AMBAYO CCM WASHAJIPANGA KUYACHAKACHUA NA KUJAZA INTEREST ZAO.
PIA ENDAPO TUME YA UCHAGUZI ITABAKI KUWA HII AMBAYO PASI NA SHAKA IMEOZA.
NA ENDAPO MFUMO HUU MBOVU UNAOTAWALA TAASISI IZI IKIWAMO USALAMA WA TAIFA UTAENDELEA KUWA KAMA ULIVYO.
VINGINEVYO HAKUNA AJA YA KUWAHOFIA AWA MAFISAD TOKA CCM ASA KAMA AYO APO JUU YATAFANYWA KAMA MAONI YA WATANZANIA WANAVOTAKA. TENA LOWASA NDO MWEPESI SANA KWANI UMAHARUFU WAKE UKO CCM CHAMA AMBACHO KIMEKUWA KIKIPOTEZA MVUTA KILA KUKICHA
 
Zamani serikali iliheshimika kutokana na ukweli kwamba haikuvumilia hata chembe ya ubadhilifu.Nakumbuka Bibi yangu alinikataza katika masomo yangu nisisomee Uhasibu kisa tu kwamba alikuwa na Ndugu yake karani wa Gulio la pamba akapoteza hela na baadaye kufungwa.Leo hii inashangaza watu kama akina Lowasa ndiyo kielelezo cha Jamii pamoja na tuhuma nzito za ukwapuaji kwa njia za kifisadi kodiza Watu maskini wa Taifa hili.
 
magufuli kafanya nini mbona slaa ametangaza na ametangazwa siku nyingi lakini hujamsema au ndiyo iliko lalia?
Labda nimeandika kwa haraka na kutoelezea concept ya Mwalimu. Mwalimu alimaanisha kua mtu anayetaka kuwa rais awe na nia na sababu za kizalendo kwa maana ya kuomba ridhaa ya wananchi baada ya kujua changamoto za hiyo nafasi na kua radhi kujitoa muhanga.
 
Nakumbuka nasaha ya baba wa Taifa mwl. Nyerere kuwa mtu aliyefirisika kisiasa uhuburi udini na ukabila, Edward Lowasa alianza na kampeni makanisani na kutoa fedha nyingi ili kujijenga kisiasa katika harakati zake za kuingia ikulu 2015. baada ya kuona mambo hayaendi sasa ameanza siasa za kikabila kwa kuwakusanya wazee wakimasai ili waandamane kuichafua chadema, na baada ya kushindikana maandamano hayo sasa amewapangia wazee hao wafanye mkutano wa hadhara, huyu ni mtu hatari sana kupewa urais
 
Acha uongo wewe wazee wa kimasai waandamane sababu ya Chadema? Maandamano yanaanzia wapi na kuishia wapi?
 
mleta maada umekuruuka,nenda kanawe tongotongo,lowasa nyota yake yazidi kungara kila kukicha,,lowasa rais 2015
 
Kama lowasa ndo atawakilisha magamba 2015 basi chama cha mapinduzi kimeoza tena kinatoa harufu kali kwa kujifanya kufumba macho na kusahau misingi aliyoiacha mwl nyerere (unafadhiliwa kwa fedha ili uingie ikulu kuna biashara gani ikulu?Ikulu ni mzigo) na kwa sababu hiyo basi malipo yake ni cdm kusimama madarakani tena kwa staili ya kumwangusha mlevi dhidi ya fisadi huyo ambaye ni tapeli wa kutupwa

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom