Ng'wanangwa
JF-Expert Member
- Aug 28, 2010
- 10,827
- 4,172
Nilimskiza vizuri huyu mtu hatari anayeitwa waziri mkuu mstaafu (na TBC) wakati akizungumzia masuala aliyoyaita uzushi wa Dr. Slaa.
Alisema "Dr. Slaa hazijui siasa za nchi hii". Wingi wa watu kwenye mikutano "si kwamba watakupigia kura".
Akaendelea kujifanya anaienzi amani ya Tanzania kama ilivyobuniwa na Julius Kambarage.
My Take:
Lowasa ni fisadi. Na fisadi ni fisadi tu hata akijikosha vipi.
Pili, suala la kutokuzijua siasa za Tanzania hata yeye ni muathirika.
Kambarage alishamchulia(si kwa ubaya) kwamba: Lowasa HAFAI kuwa Rais wa JMT. Kwa watu wanaomuenzi Nyerere bila unafiki, wanaelewa maana ya kauli hiyo ya 'Mchongameno'.
Ili kumuondoa kwenye reli, Lowasa alikikwaa kisiki. Mkwere akampoza (Mkwere kwa kung'ata na kupuliza ninamuamini). Why? Kambarage alimuambia Mkwere, SUBIRI (hakumuambia 'hufai'). Akasubiri. Akaukwaa Urais. Japo naye Mkwere anacheza sana viduku, lakini alikuwa na barka za Kambarage.
Bwana Mvi yeye aliambiwa hufai. Lakini nadhani Mkwere alielewa zaidi kauli hiyo kuliko Bwana Mvi. Na Mkwere naye kapita shule. Anajua kusoma baadhi ya mambo. Anaogopa mzimu wa Nyerere usimfuate pindi atakapokosea kukabidhi kijiti kwa mtu aliyeambiwa 'hafai kuwa Rais' wetu. Ndiyo kisa cha Richmonduli. Watu wamempa rungu Mmasai. Mmasai alishazoea ng'ombe kaanza kushika noti za Dola. Akaona Ameula. Anaweza kununua kila kitu. Hata Urais. Wapi?
Umeshindwa kununua ubunge wa Batilda Buriani, utaweza kununua Uspika wa Bunge la JMT? Unaweza kununua Urais? Aaah Wapi? Subutu!!!
Watu walishamuingiza mkennge kwenye dili ya Richmonduli. Watu wanaozijua Siasa za Tanzania. Ili aliyosema Nyerere yatimie. Na yatatimia kweli. Lazima yatimie.
Na kumtukana Dr. Slaa ni kumdharau Kambarage. Alisema upinzani wa kweli utatoka CCM. Leo kuna watu kibao waliopinga baadhi ya mambo yaliyoko CCM, wakaenda upinzani na wamefanikiwa.
Mwisho:
JK (Mkwere) ni mjanja. Mtu wa Pwani. Msanii. Anayejua kuchakachua hata kura akaingia Ikulu 'akikuna kichwa'.
Lakini Mkwere huyu huyu ninayemjua mimi. Piga ua.
HAWEZI KUCHAKACHUA MAONO YA KAMBARAGE.
Rais yeyote makini hatakubali kumuachia Lowasa kuwa Rais wa nchi.
Nawasilisha.