Lowasa Anasema Dr. Slaa Hazijui Siasa Za Tanzania, Yeye Anazijua?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lowasa Anasema Dr. Slaa Hazijui Siasa Za Tanzania, Yeye Anazijua??

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Ng'wanangwa, Nov 8, 2010.

 1. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #1
  Nov 8, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 897
  Trophy Points: 280
  Nilimskiza vizuri huyu mtu hatari anayeitwa waziri mkuu mstaafu (na TBC) wakati akizungumzia masuala aliyoyaita uzushi wa Dr. Slaa.

  Alisema "Dr. Slaa hazijui siasa za nchi hii". Wingi wa watu kwenye mikutano "si kwamba watakupigia kura".

  Akaendelea kujifanya anaienzi amani ya Tanzania kama ilivyobuniwa na Julius Kambarage.

  My Take:

  Lowasa ni fisadi. Na fisadi ni fisadi tu hata akijikosha vipi.

  Pili, suala la kutokuzijua siasa za Tanzania hata yeye ni muathirika.

  Kambarage alishamchulia(si kwa ubaya) kwamba: Lowasa HAFAI kuwa Rais wa JMT. Kwa watu wanaomuenzi Nyerere bila unafiki, wanaelewa maana ya kauli hiyo ya 'Mchongameno'.

  Ili kumuondoa kwenye reli, Lowasa alikikwaa kisiki. Mkwere akampoza (Mkwere kwa kung'ata na kupuliza ninamuamini). Why? Kambarage alimuambia Mkwere, SUBIRI (hakumuambia 'hufai'). Akasubiri. Akaukwaa Urais. Japo naye Mkwere anacheza sana viduku, lakini alikuwa na barka za Kambarage.

  Bwana Mvi yeye aliambiwa hufai. Lakini nadhani Mkwere alielewa zaidi kauli hiyo kuliko Bwana Mvi. Na Mkwere naye kapita shule. Anajua kusoma baadhi ya mambo. Anaogopa mzimu wa Nyerere usimfuate pindi atakapokosea kukabidhi kijiti kwa mtu aliyeambiwa 'hafai kuwa Rais' wetu. Ndiyo kisa cha Richmonduli. Watu wamempa rungu Mmasai. Mmasai alishazoea ng'ombe kaanza kushika noti za Dola. Akaona Ameula. Anaweza kununua kila kitu. Hata Urais. Wapi?

  Umeshindwa kununua ubunge wa Batilda Buriani, utaweza kununua Uspika wa Bunge la JMT? Unaweza kununua Urais? Aaah Wapi? Subutu!!!

  Watu walishamuingiza mkennge kwenye dili ya Richmonduli. Watu wanaozijua Siasa za Tanzania. Ili aliyosema Nyerere yatimie. Na yatatimia kweli. Lazima yatimie.

  Na kumtukana Dr. Slaa ni kumdharau Kambarage. Alisema upinzani wa kweli utatoka CCM. Leo kuna watu kibao waliopinga baadhi ya mambo yaliyoko CCM, wakaenda upinzani na wamefanikiwa.

  Mwisho:
  JK (Mkwere) ni mjanja. Mtu wa Pwani. Msanii. Anayejua kuchakachua hata kura akaingia Ikulu 'akikuna kichwa'.

  Lakini Mkwere huyu huyu ninayemjua mimi. Piga ua.

  HAWEZI KUCHAKACHUA MAONO YA KAMBARAGE.

  Rais yeyote makini hatakubali kumuachia Lowasa kuwa Rais wa nchi.

  Nawasilisha.
   
 2. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #2
  Nov 8, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,950
  Likes Received: 2,093
  Trophy Points: 280
  Kwenye red: yeye amejuaje kama si wote wanaofika kwenye mikutano ya kampeni hawapigi kura? Yeye anaangalia umati wa mikutano ya kampeni ya CCM ya kubeba watu na malori na kukusanya wanafunzi kama kule Iringa na kuchakachua picha. Pia Dr. Slaa hajatoa kigezo cha umati kwenye mikutano yake ya kampeni katika kuibiwa kura, sasa huyu Lowassa kayatoa wapi haya - I doubt his thinking capacity.
   
 3. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #3
  Nov 8, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  toka lini Lowassa anawaza mambo ya maana..siku zote anawaza kuiba tu ni JIZI hili zee
   
 4. w

  walonge Member

  #4
  Nov 8, 2010
  Joined: Aug 1, 2010
  Messages: 25
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  HApo alomaanisha siasa za wizi ambazo dokta hana muda nazo....
   
 5. K

  Kifimbocheza JF-Expert Member

  #5
  Nov 8, 2010
  Joined: Aug 7, 2008
  Messages: 496
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  Jamani

  huyu Lowasa mi nasali naye Kanisani Azania.........mbona mnamsingizia kuwa ni Mwizi

  Ni muumini mzuri 2 Kanisani LAKINI Roho yake kwa ndani SIIJUI
   
 6. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #6
  Nov 8, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Kweli Tanzania tumefulia, hadi Lowassa leo anapata confidence ya kujadili siasa wakati ana tuhuma alfu leal u lela?
   
 7. D

  DENYO JF-Expert Member

  #7
  Nov 8, 2010
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 699
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Wezi wote hao mkwere, lowasa, vijisent, sita, wote wote wote wezi ndio maana wakaunguna kumchakachua dokta slaa, nguvu ya umma inawangalia tu lazima iwalipukie hatuangalii pesa sasa hizi tunaangalia utendaji, lengo letu kwa sasa tume -nec ipigwe chini staki kupoteza welekeo nina machungu nao tume sijui nitafanya nini wezi wakubwa.
   
 8. makoye2009

  makoye2009 JF-Expert Member

  #8
  Nov 8, 2010
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,646
  Likes Received: 500
  Trophy Points: 280
  Labda kama Lowassa anazungumzia siasa za KIFISADI na WIZI WA MALI YA UMMA ndizo siasa ambazo Dr.Slaa hazijui.
  Vinginevyo anaoongea pumba tu. Hana jipya huyu,mwambieni akachunge ngombe huko masaini. Pambaf.
   
 9. sensa

  sensa JF-Expert Member

  #9
  Nov 8, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 398
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Tanzania tumemezwa na mafisadi.Ndio wameshika nchi,wameifanya yao.Zinatakiwa harakati za kuikomboa nchi kutoka mikononi mwa mafisadi,harakati kama zile za kumng'oa kaburu south africa.
   
 10. F

  Fishyfish JF-Expert Member

  #10
  Nov 8, 2010
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 231
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  CCM is full of hypocrites, not surprised.
   
 11. Pakawa

  Pakawa JF-Expert Member

  #11
  Nov 8, 2010
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,744
  Likes Received: 3,182
  Trophy Points: 280
  Huyu mtu mimi huwa ananinyima raha sana halafu akitoa kauli zake hizi uchwara ndio kabisaaaaaaaa..Dr. Slaa hajui siasa za maji taka anajua siasa ya ukweli na wewe lowassa unajua siasa za maji taka na kuiba tuuuuuuuuu huna lingine. YES I SAID,' WEWE NI MWIZI KUPINDUKIA'
   
 12. B

  Babasean Member

  #12
  Nov 8, 2010
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 35
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Niwalukumbushe kidogo viwanda vinavyohusishwa na huyu mzee wa nvi!
  Mbolea Tanga ilibidi kife ili Mbolea Minjingu kinyanyuke
  General tyre Arusha ilibidi kife ili vile vinu vya kuzalishia matariri vipelekwe nairobi (vilikuwa vinatolewa usiku pale Njiro) kuanzisha kiwanda cha Yana tyres
  Chupuchupu Tanga cement ife ili materials nyawe yanaletwa ktk kiwanda cha ARUSHA CEMENT (hakijaanza uzalishaji).
  maeneo ya kota za serikali pale maeneo ya kaloleni Arusha yaliuzwa kwake ili ajenge commercial complex, nusura wachukue na kota za polisi. Diwani alisainin lakini mbunge wa wakati huo wa Arusha mjini(Mrema) aligoma kusainin ni kikawa ndicho chanzo cha kutoelewana kwao.
  na nyinginezo nying saaaaaaaannnaa tunazifahamu.
  sasa anaposema Dr hazijui siasa za Bongo, na sisi tunayafahamu maovu yake mengi tu, Tunasubiri muda na wakati wa saa ya kuamua kulipuka na ndipo tutalipuka nae.
   
 13. kuti kavu

  kuti kavu Member

  #13
  Nov 8, 2010
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 68
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 13
  Kama yeye anazijua siasa za Tanzania vizuri ya kuwa umati wa watu mikutanoni hau ashirii idadi ya watu wataopigia kura muhusika wa mkutano huo... ni vyema akatueleza kilichotokea jimbo la Arusha mjini...vipi fomyula zake zilikataaa nini???...na kama fomyula hizo zilishindwa A-TOWN hadi akalazimika kwenda kujaribu kulazimisha mambo na bado yakabuma, ana uhakika gani kwamba yale ya Arusha na majimbo mengine yaliojiondoa mikononi mwao sio mwanzo wa mabadiliko ya hayo mazoea ya Mh huyu kuwa nguvu ya umma iko chini ya utabiri wao????

  Mi naona anasahau kuwa nyakati zimebadilika na kwamba ile Tanzania aliyoizoea si ya leo...Hiki ni kizazi cha watu wanaouliza maswali na kutaka kujua kwa kiasi gani viongozi wanatimiza yale walyi ahidi...

  Ni vyema viongozi wakajifunza kusoma nyakati, ole wao kama wataendelea kukariri kuwa muamko tulioua safari ni jambo la kupita au ni nguvu ya bia...
   
 14. bucho

  bucho JF-Expert Member

  #14
  Nov 8, 2010
  Joined: Jul 13, 2010
  Messages: 4,547
  Likes Received: 429
  Trophy Points: 180
  kama kweli ni fisadi mbona asifikishe mahakamani kama wakina mramba ? na mbona ananguvu sana na anajiamini sana ? huyu jamaa ni mchapa kazi sana sio mzembe hata kidogo, ndio maana hakuna mtoto anafaulu monduli kwenda sekondari alafu akashindwa kwenda shule kwa kukosa ada . kama kweli ni fisadi hatafika mbali lakini kama alisingiziwa atatoboa mbali sana . anyway mungu ndio anajua ukweli.
   
 15. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #15
  Nov 8, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Lowasa is so full of primitive ideas as so long
   
Loading...