KENZY
JF-Expert Member
- Dec 27, 2015
- 35,744
- 86,370
Ilikuwa ni siku ya mimi na yeye, tukiwa ndani tukirabahuka kwa muziki na pombe kwa mahaba na huba, kwenye playlist yangu nikawa nimetupia huo wimbo!..
Nikaona mwenzangu kanyanyuka mikono juujuu kama mateka!, punde namuona anaanza kucheza kwa madaha!, kiuno kikipelekwa kushoto na kulia huku akigeuka geuka!. kusema kweli ilikuwa ni picha nzuri iliyonivutia maana hakuna ambapo hapakushawishi kuangalia!, na hakuna ambapo palikosea step yoyote ya uchezaji!.. kivazi chake chakulalia kilimkaa vyema!, kikiwa kama kinataka kumtosha na hapohapo kisimtoshe!.
Sikuwahi kudhani ni mchezaji kiasi hicho ila wimbo huu ulifanya nimjue yeye ni nani katika uchezaji!.. Nilibaki nikimtazama huku nikivutiwa zaidi na kile alichokuwa akikifanya!, penye kubinuka alibinuka na penye kujikunja alijikunja!.
Hii ilikuwa ni kama kampeni!, mgombea akijinadi mbele yangu!, aliendelea kukatika ila mara hii aliniangalia lile jicho la "njoo tucheze!".
Huku nikiwa mwingi wa tabasamu lenye hamu lakini lililokosa nidhamu, nami nikatia dimbani.
kwa mikono yake akanikaribisha nikishike kiuno chake bila ajizi nami nikakishika ndipo hapo niligundua ule muda wote aliokuwa anacheza peke yake nilikosa uhondo!.
Akiwa kama hataki na anataka alivingirisha kiuno kufuata mirindimo ya mziki huu mzuri kila paliposemwa "L.o.v.e y.o.u" nikama alikuwa akikitetema kiuno chake kwa mbali!. hakika nilikutana na dahali ya raha!.
Hakuishia hapo pale anapoanza ku rap Eve ndio akaamua kunimaliza!, maana alinigeukia ikawa tunacheza kwa taratibu huku akiliangua tabasamu tamu ikawa kama tunacheza salsa ile ya taratibu huku tukifuata mrindimo huu wa dancehall ukiwa umechanganywa na R&B, wenyewe huita blend!.
Hakika mtoto huyu alijua kunimaliza kwenye huu wimbo hata sasa nausikiliza, namkumbuka natamani ijirudie siku ile kuna viumbe vinajua kutoa raha bila karaha!.. 🎶 🎶 🎶