NAMBA TISA:
Mapenzi mapenzi mapenzi...nakuita mara tatu, kwanini umeniadhibu hivi, kwanini mimi...msomi, mrembo, niko na pesa, natoka familia decent, why mapenzi yanitese hivi, sijawahi kupata jibu walahi....
Nikawa nimepata nguvu na nilishaanza mazoezi ya hapa na pale, katika kitu sikuhitaji ni kuharibu shape yangu....nilijua ni mrembo na nilikua naona fahari Ile kuangaliwa na kupewa compliments , uko mzuri, hakuna feeling tamu ya kua mwanamke kama kujifahamu kua wewe ni mwanamke mrembo

...ila pamoja na hayo yote moyo wa yule mwanaume Karim ulikua unakuja halafu unakataa kwangu.
Mama aliniweka kikao siku chache baada ya kupata nguvu, kile kikao si kama vikao vingine vilivyopita, ile siku yule mwanamke alikua mpole sana, na unaona maumivu yake kama mama. Alianza kwa kuniuliza Leon ni nani kwangu, nikamwambia ni mwanaume wangu wa zamani kabla sijakutana na Karim, akaniuliza pia ujauzito ni wa nani? nikamwangalia mama kwa mshangao, kwanini awaze hivyo? mi ni mchumba wa Karim official napataje ujasiri wa kubeba mimba ya mtu mwingine, nikamwambia mama ni ya Karim, you knew it from the beginning.
Mama akaniambia Bella, my beautiful girl, Karim yuko wapi hadi sasa? anafahamu kua umejifungua , nikamwambia mama anafahamu, tunawasiliana, na leo tumewasiliana, akaniambia Bella Kuna kitu unanificha mwanangu...Karim ni nani? Kwanini hajatokea katika wakati huu mgumu, vipi nisingemudu kufika mwanangu, ina maana Leon ndio angekua ndugu pekee kwa wakati huu?
Nilijikuta tu naangusha machozi, mama akaniambia kwa leo binti angu hata sitokukumbatia, nataka uniambie ukweli, nini kinaendelea na maisha yako ya mahusiano, is Karim real loves you? nikamwambia mama nisamehe tu, hatuwezi muongelea Karim...nisamehe mama, niliingia chumbani nikalia for hours, aisee nililia mnooo, nachokumbuka ni mama kuniambia kua , yeye Kama mzazi anatamani kuniona niko na furaha, na pia nisiwaumize wengine wakati wa kutafuta furaha yangu,kama ni kweli niliyemchagua ni Karim, Basi nikae na Leon nimwambie ukweli kua ninampenda mtu mwingine, just release that boy Bella, alikesha nami hospitali na bado anaendelea kusumbuka na maisha yako, let him go, unamtesa kijana wa watu.
Sio Kama sikua na ya kumwambia mama kuhusu Karim ,yalikuwepo tena mengi, ila sikuona kama ni busara maana mama angu namfahamu, angemchukia Karim na lile jambo lingefika kwa mzee kila kitu kingeishia hapo, my dad loves me walahi, sijui ni vile nilikua mtoto wa kwanza na pia nilikua wa kike pekee, sikutaka wamchukie Karim kabisaaaaa, na hapo kumbuka dogo niliyeenda nae hospitali kumfata Karim kwa mara ya kwanza hadi leo bado hajawahi mkubali Karim, kwani mashemeji mna nini jamani daaah.
Niliyabeba moyoni maumivu ya Karim, ni kama alikua amenitelekeza, nilidanganya tu kwa mama kua tunawasiliana, ila ukweli Karim hakunichek kwa zaidi ya miezi mitatu sasa. Nilijitahidi kujipendekeza wapii, nikamtumia picha za ultra sound ya mwisho kabla ya kujifungua lakini wapi, siku chache kabla ya kujifungua nilimtumia ujumbe kua nimebakisha siku chache sana, kama utaweza kuja nitafurahi mnoo, ule ujumbe haukujibiwa ,yaani kwa kifupi Karim ghosted me.