LOOO! Hatimaye chanjo ya UKIMWI yapatikana.

Nzowa Godat

JF-Expert Member
Jun 15, 2011
2,783
819
Utafiti uliofanywa pamoja na
majaribio katika kinga mpya
umedhihirisha kuwa kinga hii
mpya imefanikiwa kukinga
tumbiri asiambukizwe virusi
vinavyosababisha ukimwi na
kutokana na hilo kutowa ishara
kwamba kuna uwezekano
mpya wa kukabili kinga ya
maradhi ya ukimwi.
 
 
Umepata wapi hizi taarifa?

Kiongozi wa mradi huo
Profesa Louis J Picker, wa
taasisi ya tiba ya kinasaba huko
Oregon, anazilinganisha seli
hizi na askari imara wa kulinda
doria.
"ni mfano wa askari
wanaorejea kambini na
kutelekeza silaha zao, kwa
imani kuwa wenzao
wanaendeleza kazi bila
wasiwasi," Profesa Louis
Picker aliambia BBC.
Aliongezea kusema kuwa kuna
ushahidi kwamba kinga hiyo
iliteketeza dalili zote za
ukimwi (SIV) katika tumbiri
wote, sababu aliyoielezea
kama inayowezekana kwa
ukimwi wa binadamu.
Mashaka Wataalamu walio nje
na wanaoendelea na uchunguzi
walifurahia matokeo haya,
lakini wakaonya kuwa sharti
usalama uzingatiwe kabla ya
kufanya majaribio kama haya
kwa binadamu.
Hata hivyo Profesa McMichael
wa Chuo Kikuu cha Taifa
nchini Australia alisema kuwa
ni mfano huo wa SIV uliomo
katika nyani na tumbiri
uliosababisha HIV, kwa hiyo
majaribio haya kwa nyani na
tumbiri yanaonyesha dalili
nzuri.
 
Ukimwi siyo mpaka kuzini mkuu,ajari,kuambukizwa kutoka kwa mama,kuambukizwa kwa sababu ya kushare vitu kama sindano,wembe etc
 
 
ukimwi siyo mpaka kuzini mkuu,ajari,kuambukizwa kutoka kwa mama,kuambukizwa kwa sababu ya kushare vitu kama sindano,wembe etc

mpaka hiyo kinga ifike hapa labda wajukuu zetu ndo wataipata.arv,zenyewe zipo kimagumash.vile vipimo vya hiv kuna mahali wanavificha.huku tabata kuna hosp ya serikali pale shule nimeenda mala 3 kutaka kupima nazungushwa tu.na kuna dispensary nyngne inaitwa malecela ni ya serikali pia huku tabata ni mtindo huohuo!nimegairi kupima.
 
wazinzi mrudieni Bwana Mungu wenu, zinaa haina maana.

Unaweza kuupata saloon ukinyolewa mweye au ndevu, kwenye ajali ya gari au popote pale ambapo uwezekano wa mtu mwenye jeraha kugusana na damu au majimaji yenye virusi.
 
Iyo kinga ikianza kutumika litakuja gonjwa lingine ambalo litakuwa kali kuliko ngoma!
Cha msingi kwa wanaoendekeza ngono zembe wamrudie Mola tuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…