Londa ampigia kampeni JK msikitini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Londa ampigia kampeni JK msikitini

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Zak Malang, Sep 11, 2010.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  Sep 11, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0

  * Hamad Rashid apigwa butwaa

  Katika hali ya kushangaza, aliyekuwa Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Dar es Salaam, Salum Londa, jana aliwagawa waumini wa dini ya Kiislamu, baada ya kupiga kampeni msikitini akiwataka waumini hao wamchague mgombea urais kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Jakaya Kikwete.

  Londa alitoa kauli hiyo mara baada ya kukaribishwa katika ibada ya sherehe za Idd el Fitr iliyofanyika katika Msikiti wa Al farouq, Kinondoni, Dar es Salaa na kusisitiza Waisilamu kutofanya makosa kwa kupigia kura, kama walivyofanya mwaka 2005.

  Londa amabaye alikuwa mgeni rasmi katika swala hiyo, alisema ipo haja ya Waisilamu kutofanya makosa na wajue umuhimu wa kuchagua viongozi kama miaka yote iliyopita.

  Baada ya kutoa kauli hiyo, kundi la Waisilamu lilinyanyuka na kuondoka huku wengine wakilalamika kitendo hicho na kusema hakiendani na utamaduni wao kutumia nyumba za ibada kufanya kampeni za uychaguzi kwa viongozi wa siasa………...


  ……….Akizungumza na Tanzania Daima mara baada ya kumalizika hotuba hiyo, Mbunge wa Wawi (CUF) amabaye pia ni kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni anayemaliza muda wake, hamad Rashid alisema hakupendezwa na kitendo cha kiongozi wa siasa kupiga kampeni msikitini, kwani kufanya hivyo ni kuharibu utaratibi katika nyumba za ibada.

  “Mimi nilipigwa na butwaa kwa kitendo hiki, kitendo cha mwanasiasa kusimama kwenye nyumba za ibada kumpigia kampeni mgombea fulani, kamwe hakikubaliki,” alisema Hamad.


  Wana JF: Hiyo ni sehemu tu ya stori ukurasa wa mbele katika Tanzania Daima ya leo.
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Sep 11, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Londa ana ma'frustrations ya ufisadi wa ardhi Kinondoni, sasa anajaribu kwa kila njia kuosha uso wake mbele ya JK na wanaccm, akitegemea KUKUMBUKWA mbele ya safari!
  Sasa hivi ukimpa mtu jukwaa dogo tu utashangaa jinsi atakavyolitumia kujifaidisha!

  All in all, amefulia huyu, hana jinsi ya kuondoa kashafa!
   
 3. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #3
  Sep 11, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,173
  Likes Received: 892
  Trophy Points: 280

  Wanaohubiri wananchi wasiwe na udini ndo haohao wanaohubiri udini.
   
 4. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #4
  Sep 11, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Huyu Bwana kafanya hujuma na wizi mkubwa sana Manispaa ya Kinondoni kiasi kwamba ingekuwa kuna utawala bora na kuwajibika, wakati huu asingekuwa msikitini anafanya kampeni, bali lupango akila dona. Anamfanyia kampeni JK kwa sababu anajua fika kwamba ni yeye tu ndiye atakayemlinda kutokwenda jela, kama vile JK anavyowalinda wezi wengine wengi ndani ya CCM!

  Nani katika mafisadi wakuu -- hasa wale papa -- wanaweza kuthubutu kumkampenia Dr Slaa? Hawawezi, kwani kufanya hivyo ni kujipalia makaa.
  Lakini cha kushangaza zaidi ni jinsi tutakavyoona taasisi kuu ya kusimamia uchaguzi -- NEC -- itakavyokaa kimya kuhusu hili!
   
 5. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #5
  Sep 11, 2010
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Safi sana ndugu zangu waislamu, mngempiga makofi kabisa ili iwe fundisho kwa wengine wanaongeuza Misikiti/makanisa sehemu ya kampeni hasa Lowasa,Rostam....
   
 6. BinMgen

  BinMgen JF-Expert Member

  #6
  Sep 11, 2010
  Joined: Jun 18, 2008
  Messages: 1,816
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Hongera Waislam
   
 7. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #7
  Sep 11, 2010
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 14,559
  Likes Received: 1,648
  Trophy Points: 280
  Nadhani haukuwa msikiti wa ndugu zangu answari sun, Laiti ingekuwa huko angetoka na manundu, lazima angechezea bakora!
   
 8. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #8
  Sep 11, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Hivi ingekuwa ndo mchungaji mmoja kafanya hivyo kanisani, kina Malaria Sugu na aliases zake zote wangeibuka humu na ku-fire through all cylinders!!!
   
 9. h

  hagonga Senior Member

  #9
  Sep 11, 2010
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 141
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
 10. Negotiator

  Negotiator JF-Expert Member

  #10
  Sep 11, 2010
  Joined: Aug 9, 2010
  Messages: 303
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  aibu yao milele. Wamegeuza msikiti chumba cha kampeni?
   
 11. P

  PUNJE JF-Expert Member

  #11
  Sep 11, 2010
  Joined: Jul 30, 2008
  Messages: 334
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 45
  ..Londa amefanya hivyo na inaonekana ni KOSA, je kitafuata nini kutoka kwa vyombo vinavyosimamia kanuni na sheria za uchaguzi? Au hadi mtu ajitokeze kutoa malalamiko?
   
 12. njiwa

  njiwa JF-Expert Member

  #12
  Sep 11, 2010
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 11,065
  Likes Received: 1,803
  Trophy Points: 280
  Mtume wetu alifanya msikiti nyumba ya ibada na pia kuendesha vikao!... SIASA MSIKITINI Ndio mahala pake waislamu wanajidili nani tuumchaguwe!! CUF ndio wanatupotezea! ..:mad2:
   
 13. BelindaJacob

  BelindaJacob JF-Expert Member

  #13
  Sep 11, 2010
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 6,060
  Likes Received: 475
  Trophy Points: 180
  Tu machi,lol!..Mwaka huu watajibeba sana!!!
   
 14. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #14
  Sep 12, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Kwani ndio wameanza au wameamua sasa kufanya live? na hutasikia mtu akikemea. Lakini thubutu lifanyike kanisani......zitaimbwa hadithi za amani na utulivu hizo? Haya bana ngoja na sisi twende kesho kanisani tukamwage ugali maana wamemwaga mboga
   
Loading...