Loliondo pananuka mauti | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Loliondo pananuka mauti

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Logo, Mar 28, 2011.

 1. Logo

  Logo JF-Expert Member

  #1
  Mar 28, 2011
  Joined: Jan 26, 2011
  Messages: 588
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Tulishasema jaman hapo mwanzoni kuwa Loliondo patakuwa makaburini, ooh! watu wakaanza kututukana mara nyie mmetumwa ooh mara hili! Sasa mapema kabisa ukweli umekuwa wazi! Ukweli la suala la Loliondo ni la kiimani, na ni gumu kulitafsiri lakini inakuwaje yawe makaburi ya watu?? roho ya mauti hatari sana! Mungu hawezi kuwaponya hao watu kwa neno mara moja mpaka wafe wanasubiri kikombe?? Naogopa kusema sio kazi ya Mungu ila jiulize. Yeremia 5:29-31!!
  Tafakuru yangu:-
  1. Hivi shetani hawezi kuja akijifananisha kama Mwana wa Nuru?
  2. Hivi kweli kumbe watu wanaweza kufa wakisubiria tiba ya Mungu?
  3. Hivi kumbe Mungu anaweza kuzidiwa kuhudumia watu aliowaumba?
  4. Hivi kumbe Mungu anaweza kuzuia watu wasiongezeke hadi amalize kuwahudumia waliotangulia?
  5. Ahaaaa kumbe Loliondo unaweza kuwa mtego wa shetani kumaliza watu wetu?

  Nimetosha, lakini sihukumu sijui kama Babu katumwa na mungu au la? ninachoweza kusema tafakari mambo hayo matano!
  Nawasilisha

  View attachment 25816
   
 2. BornTown

  BornTown JF-Expert Member

  #2
  Mar 28, 2011
  Joined: May 7, 2008
  Messages: 1,716
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Mazunge! Usikurupuke maiti unazozisema Loliondo ni wale wagonjwa waliokuwa mahututi waliotoroshwa na ndugu zao kwenye Mahospitali waliyokuwa wamelazwa ndio wanaofia njia kuelekea kwa babu. Jaribu kufuatilia vyombo vya habari vinavyosema soma magazeti sio ya UDAKU utajua ukweli uko wapi.
  Ngugu wengi sana wamekuwa wakitorosha jamaa zao waliomahututi ili waje kupewa tiba na babu badala yake wanafariki wakiwa njiani ame kwenye foleni so hilo sio kosa la babu ni kosa la watoroshaji wagonjwa mahospitalini hivyo usipoteshe umma kwa mambo usio kuwa na uhakika nayo!!

  TAFAKARI KWANZA KABLA YA KUANDIKA!
   
 3. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #3
  Mar 28, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  karibu ukweli utajulikana

  Bwana apewe sifa
   
 4. Logo

  Logo JF-Expert Member

  #4
  Mar 28, 2011
  Joined: Jan 26, 2011
  Messages: 588
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Tafakari kwanza kabla ya kujibu
   
 5. Logo

  Logo JF-Expert Member

  #5
  Mar 28, 2011
  Joined: Jan 26, 2011
  Messages: 588
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Unatakiwa kupanua wigo wa mtazamo ndugu yangu!
  1. Asingekuwepo Babu Loliondo ni nani angetorosha mgonjwa kwenda huko?
  2. Nina testimony za watu zaidi ya watatu ambao wamefariki na walikuwa tayari wamekunywa dawa ya babu! Taarifa zinasema watu hao walikufa baada ya kuzidiwa kutokana na kuambiwa wasitumie dawa za kurefusha maisha hali ambayo iliwafanya wakadhoofika ghafla na kujikuta wakifa!
  Fikiria tu tena kwa upana! Angalia tatizo na ikibidi ulisolve kwa Problem Based Tree! kama unaijua hii kitu anza kwa kuangalia Roots, shina na matunda!
   
 6. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #6
  Mar 28, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  sasa unadhani kwa nn wanawatorosha wagonjwa wao? wana imani.hata yule mgonjwa aliepelekwa kwa yesu wakampitisha darini ili amponye ni kwa sababu ya imani yao.Utawahukumu kwa Imani yao? labda ulaumu serikali kwa kuruhusu magari mengi na watu wengi kwa wakati mmoja bila kuzingatia miundo mbinu na uwezo wa babu kuhudumia.Hao marehemu hata kama wasingekunywa dawa kwa babu wengekufa tu na kamwe babu hamwambii mtu aistumie ARV bali kawaambia wapime baada ya siku 7....Naona mada yako haina akili nadhani pia we ni mmoja wa wanaotegema mkate kwa kudanganya waumini kuwaponya ili mfaidi zaka na sadaka huku mkiwahadaa kwa maombi ya uwongo.
   
 7. LeopoldByongje

  LeopoldByongje JF-Expert Member

  #7
  Mar 28, 2011
  Joined: Apr 28, 2008
  Messages: 373
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Napenda sana watu ambao wana mawazo pevu. Nionavyo mimi watu watenganishe Kifo na Tiba ya Babu. Kifo ni hatima hakuna awezaye kuzuia kifo ila Mwenyezi Mungu peke yake tu. Babu yeye keshawaelezeni kuwa yeye anatoa tiba kwa mgonjwa anayeamini; ili hatoi kinga ya maradhi na kwa jinsi hiyo kifo. Wapo wengi wameenda kupatiwa tiba kwa babu na Wamesema kuwa wamepona. Wapo wengi wamekunywa kikombe na bado hawakupona. Wapo wengi wanakufa na watakufa wakiwa kwenye foleni kupata kikombe.

  Tufahamu mahali penye watu wengi wanaoumwa mauti kutokea si ajabu. Angalia Hospitali zetu za Muhimbili, Mwananyamala, Bugando, KCMC Moshi n.k. kila uchao utasikia watu kadhaa wamekufa. Kama unabisha fungua Redio wakati wa matangazo ya vifo. Utasikia wanatangaza kifo cha fulani kilichotokea Hospitali fulani. Na siku za karibuni tunasikia wanangaza kifo cha fulani kilichotokea safarini Loliondo. Hivyo wanajanvi hili ni jambo la kawaida kutokea kila mahala panapoitwa Hospital. Kwa Babu nayo ni Hospitali pia. Hivyo vifo vitegemewe.
   
 8. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #8
  Mar 28, 2011
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,918
  Likes Received: 2,068
  Trophy Points: 280
   
 9. BornTown

  BornTown JF-Expert Member

  #9
  Mar 28, 2011
  Joined: May 7, 2008
  Messages: 1,716
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
   
 10. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #10
  Mar 28, 2011
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Kwani kaka yao kina Martha (sijui ni Lazaro) hakufa akiwa anamsubiri Yesu aje? Alipokuja ndio akamfufua? Je hakufa akiwa anasubiri tiba ya Yesu?
  Soma kitabu cha Wafalme, ile jeshi la Syria lilipozingira Mji wa Yerusalemu. Watu wakawa wananunua hadi mavi ya ndege. Je, walipojua kuwa kuna chakula nje, yule jemedari hakufia pale mlangoni? Unadhani ni yeye tu aliyekufa kutokana na stampede?
  Saa nyingine usitafute mistari inayo-support view yako mwenyewe tu.
   
 11. Logo

  Logo JF-Expert Member

  #11
  Mar 28, 2011
  Joined: Jan 26, 2011
  Messages: 588
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ngoja njitahidi kuchora problem tree nitaiattach nikimaliza! Mi nadhani hujatumia busara hapo kwenye red! Unakasirika nini sasa? jiulize hao saba wakati walikuwa hospitalini walikuwa wanakufa hivyo? Unapolaumu serikali haijasimamia miundombinu unafukiri uko sahihi? Serikali unaihusudu kwa lipi? hehehe haya bwana inaonekana jazba imepanda! Siwezi kuhukumu sijajua babu kama katumwa na Mungu au La! Fikiria hizo pointi tano hapo juu!
   
 12. Logo

  Logo JF-Expert Member

  #12
  Mar 28, 2011
  Joined: Jan 26, 2011
  Messages: 588
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kama unajua Lazaro alikufa na akaja kufufuliwa na bado unatoa mfano hivi kweli hujiulizi wewe mwenyewe?? Kwanini sasa alifufuliwa? Halafu huo mfano mwingine wewe unauvuta tuu sehemu hiyo hautafiti hata!
   
 13. Logo

  Logo JF-Expert Member

  #13
  Mar 28, 2011
  Joined: Jan 26, 2011
  Messages: 588
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
   
 14. Logo

  Logo JF-Expert Member

  #14
  Mar 28, 2011
  Joined: Jan 26, 2011
  Messages: 588
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
   
 15. Logo

  Logo JF-Expert Member

  #15
  Mar 28, 2011
  Joined: Jan 26, 2011
  Messages: 588
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hoja safi! Nakubali kuwa una upevu mkubwa wa kutoa hoja! Bado ni maswali haya:- Kama hali hii ya kufa watu itaendelea wakati babu amesema hao watu ni tone tu wakija wale aliosema watafika je wangapi watakufa zaidi? Huoni kuwa patakuwa pananuka mauti? Sidhani kama Mungu naweza kuendesha kazi yake kwa ushujaa wake katika maeneo ya kunuka mauti kiasi hicho!
   
 16. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #16
  Mar 28, 2011
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,502
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Babu hajakataza watu kutumia dawa za kurefusha maisha.....

  Babu anasema dawa yake inafanya kazi na mtu atapona kuanzia wiki mbili au zaidi....

  Katika kipindi hiki, mtu inatakiwa kutumia dawa za kawaida.

  Anasema ukiumwa kichwa, kunywa Panado, ukiumwa homa kunywa ................

  Acheni kudanganya watu bana........... Angalia hii video ya Wakenya umsikie Babu mwenyewe.

   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 17. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #17
  Mar 28, 2011
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,502
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Acha UONGO wewe. Umeandika kwenye heading Pananuka na mwisho unaandika PATAKUWA PANANUKA.
   
 18. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #18
  Mar 28, 2011
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,921
  Likes Received: 453
  Trophy Points: 180
  Huenda hata wewe unakurupuka, fikiria kabla ya kutafakari, vitu vingapi vinatokea loliondo ambavyo hawataki kusikia??vitu vingapi vinapotoshwa na media na hayo magazeti usiyoyaita ya udaku??kwahiyo we akili yako 100 percent imelalia kwa vyombo vya habari tu?wala hata kwenda kuona ukweli hujatamani? haya sasa TBC ishaanza kuonyesha miili ya watu inaoza msituni..ni jana tu!! sijui media zipi unataka kuziamini.
  Bila uwepo wa babu hakuna mgonjwa ambaye angehamishwa hospitalini, mbona madaktari wanashauri sana kwamba hata kama mkienda kwa babu msiache dozi za hospital...
  Mi nipo india, kuna dogo mmoja nipo nae ana kisukari cha kurithi, alijigundua wakati yupo sekondari, maza ake keshamtumia tiket ya ndege mapema arudi ili ampeleke kwa kwa babu, jana nimepiga nae stori nimesikitika alichoniambia...!! maza ake baada ya kupiga kikombe kwa wiki kadhaa alijisikia fresh(ana kisukari) lakini sasa hivi hali yake inatetereka sana, na ashamwambia dogo kwamba hajapona bado kisukari kipo palepale, dogo nae kachanganyikiwa huku...think twice
   
 19. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #19
  Mar 28, 2011
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  alikufa akisubiri au hakufa akisubiri? wewe umesema kuwa watu wanakufa wakisubiri tiba ya babu. Kana kwamba sehemu nyingine hawafi wakisubiri tiba. Babu yeye kapewa idara tofauti ya kuangalia. anyway...it seems u wont understand!
   
 20. Logo

  Logo JF-Expert Member

  #20
  Mar 28, 2011
  Joined: Jan 26, 2011
  Messages: 588
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Acheni kupamba hoja zilizowazi! Hairuhusiwi kunywa ARV ukinywa dawa ya Babu haya ndiyo masharti ya awali labda kama mmeyachakachua sawa!
   
Loading...