Loliondo na Uhalali wa Mitishamba ktk BIBLIA

Lawkeys

JF-Expert Member
Nov 16, 2009
1,118
287
Kuna wachungaji wa mshahara wanapotosha watu kuhusu mitishamba!!

Mtaani kwetu
Leo asubuhi nimemsikia mchungaji mmoja wa kanisa flani akikashifu dawa ya Loliondo, alikuwa akitoa muongozo wa maandiko kwa mpangaji wake, amesema;

"Miti yote ina pepo, na watu wote wana mapepo ambayo yanawaongoza kutumia miti na matunda kama dawa badala ya kutumia kama chakula."

Akaendelea kusema,

"Mapepo yalio ndani ya watu ndio yalio waongoza watu 6000 kwenda kunywa dawa Loliondo."

Mpangaji akanywea. Inawezekana wanazuoni hamtapata nafasi ya kupitia aya, hivyo ili kurahisisha mambo nitatupa mbili.

1. Ezekiel 47:12- Na karibu na mto, juu ya ukingo wake, upande huu na upande huu, utamea kila mti wa chakula, ambao majani yake hayatanyauka, wala matunda yake hayatatindika kamwe; ...matunda yake yatakuw ni chakula na majani yake yatakuwa ni dawa.

2. Ufunuo 22:2- katika njia kuu yake. Na upande huu na upande huu wa ule mto, ulikuwapo mti wa uzima, uzaao, matunda aina kumi na mbili,wenye kutoa matunda yake kila mwezi; na majani ya mti huo ni kuwaponya mataifa.

Wazungu watu wabaya sana, wametufanya tuamini kwamba kila kitu chetu ni uupuzi. Jamani hata dawa kutika katika majani? Bila hata uthibitisho unasema DECI wakina kakobe muogopeni Mungu.

Ili mradi hakuna ibada ya mizimu, kupiga ramli, na uchawi, mitishamba inakubalika katika maandiko.
 
Ndo kasumba hizo kaka. Binafsi ni mpenzi sana wa dawa za asili. Aloevera chungu ni dawa ya malaria, na ninao mche wake nyumbani. Kwanini nikanywe midawa mseto ambayo sasa hivi watakuambia hazifai kama walivyosema kwa fansidar, chloroquine na SP.
 
acha umbumbu wewe.kwani dawa mseto,SP,Chloroquine zimetoka wapi?dawa nyingi zimetoka kwenye majani ya asili.
 
acha umbumbu wewe.kwani dawa mseto,SP,Chloroquine zimetoka wapi?dawa nyingi zimetoka kwenye majani ya asili.

Ww kipindupindu ndio MPUMBAVU wa kwanza,japo zimetokana na majani ila zimechanganywa na kemikali kibao! Jamaa yupo sahii kutumia pure mimea na ww mpumbavu,kilaza usiejua kama chloroquine imechanganywa na chemicals funguka!
 
LUGHA ZITUMIKAZO.....wazee hupenda kutuasa vijana kuwa hii ni tatizo la kupelekwa suna hospitali....!
 
Ww kipindupindu ndio MPUMBAVU wa kwanza,japo zimetokana na majani ila zimechanganywa na kemikali kibao! Jamaa yupo sahii kutumia pure mimea na ww mpumbavu,kilaza usiejua kama chloroquine imechanganywa na chemicals funguka!

wewe ndio tepe kabisa taja hizo 'chemicals' zilizoko kwenye chloroquine na sio kutoa shutuma kama mpiga debe wa stendi.dawa ya babu ni feki,wapuuzi kama nyinyi ndio mnaoamini inatibu.
 
Jamani msitoane macho kwa babu hiari kwenda haulazimishwi hii dawa imetibua dili nyingi NGO za kuhudumia waathirika na makanisa yanayotaka upande mbegu (fedha) ili upokee uponyaji sasa nawapa mbinu ni bora wakawawekea mazingira mazuri waumini wao ya kufika kupata kikombe ili warudi kwa pamoja kuendelea na ibada kwani babu hawaambii watu wajiunge na kanisa lake ni lazima watu warudi kwenye makanisa .
Lakini single dose ya babu imetulia sana
 
acha umbumbu wewe.kwani dawa mseto,SP,Chloroquine zimetoka wapi?dawa nyingi zimetoka kwenye majani ya asili.

Mbumbumbu babako mzazi! Wewe umesoma phamarcy ya wapi hata ukajua dawa za magharibi zinavyotengenezwa, unajua chemical composition yazo? Mimi naamini mitishamba kwa kuwa nina uhakika ni halisi kwa asilimia mia. Mara ngapi tumeambiwa dawa zimeleta madhara kwa watumiaji, alovera natural never did that you sucker! Au unamiliki duka la dawa mnazojichukulia hospitali za serikali? Afu sio kwa vile una domo ndo uchangie kila kitu kaka, unakuwa kama Kibonde bwana?
 
ama kweli usilolijua litakusumbua. mwajifanya wasomi kumbe ni ngazi ya kupatia mishahara tu. huko makanisani ni wapingaji wakuu wa dawa zetu za asili, hili likiwa ni zao la mkoloni. labda baada ya vita ya maji maji kushindwa. Hata"Babu" naamini ktk utumishi wake alikuwa akipinga dawa zetu. Lakini ktk Biblia tuna mifano mingi mno ya dawa zetu. Elisha alitibua maji yenye sumu kwa chumvi yakawa matatu mno, pia soma 2Wafalme 4:38-41 hapa alitumia unga kuondoa sumu chakulani hakwenda kwenye maabara za TFDA, nk. yote haya wachungaji wanasahau wanapokuwa wakizipigia debe dawa za wazungu. famasi mtu anaona bora anunue metakelfin ya kenya kuliko ya keko (ambayo ni nzuri mno). Sasa Yahu (Mungu) amewarudi viongozi wa dini zote kuwaonyesha kuwa wanayoyahubiri kwa watu ni uongo. kama sivyo Babu asingetoa dawa. Ushauri, Heshimuni kazi zote za muumba wetu maadamu ni kwa ajili ya utukufu wake. Zaburi 18. Tujikumbushe ya askofu kule mbeya kukutana na waumini wake kwa mganga wa kienyeji ...
 
Watu tunaangamia kwa kukosa maarifa. Dawa namba moja ya miili yetu ni vyakula tena vile vya asili. Na kwa sababu tumezoezwa kuiharibu asili, sasa tunavuna uharibifu kwa kwenda mbele. Kila kitu kimechakachuliwa.
.
 
mifano tunayo ya kutosha kuamini mitishamba ndio dawa sahihi na salama zaidi kuliko dawa zote za kimaabara lakini kwa sababu tumeathiriwa akili zetu na wazungu na kuona kila kilicho chetu ni uchafu na upuuzi mtupu. angalia babu zetu walivyoishi hakukuwa na dawa za hospital wala maabara ya kucheck malaria na waliishi kwa muda mrefu kwa sababu walitumia vyakula vya asili ambavyo vinafanya kazi maradufu. mosi kama chakula cha kuupa mwili nguvu na pia kama kinga kwa mwili kutokana na maradhi mbalimbali ambayo waliyapata so waliumwa na mbu but hawakufa kwa malaria. angalia kizazi hiki kinaishi kwenye ulimwengu wenye kila aina sayansi lakini ndio waathirika wakubwa wa kila magonjwa so hata bila kutumia msaada wa kibiblia au kiimani dawa za asili zinaplay role kubwa sana, ni tu uelewa wetu kuhusu hizo dawa na mapokeo ndivyo vinavyotusumbua.
 
wewe ndio tepe kabisa taja hizo 'chemicals' zilizoko kwenye chloroquine na sio kutoa shutuma kama mpiga debe wa stendi.dawa ya babu ni feki,wapuuzi kama nyinyi ndio mnaoamini inatibu.

Ngoja uugue wakati hayupo ndo utaona umuhimu wa hiyo dawa. Umetukana maelfu ya watu pamoja na viongozi kwa kuwaita wapuuzi kwa kuamini dawa na kwenda kuinywa. Tuwe tunaangalia nini tunaandika na siyo kuropoka
 
Mbumbumbu babako mzazi! Wewe umesoma phamarcy ya wapi hata ukajua dawa za magharibi zinavyotengenezwa, unajua chemical composition yazo? Mimi naamini mitishamba kwa kuwa nina uhakika ni halisi kwa asilimia mia. Mara ngapi tumeambiwa dawa zimeleta madhara kwa watumiaji, alovera natural never did that you sucker! Au unamiliki duka la dawa mnazojichukulia hospitali za serikali? Afu sio kwa vile una domo ndo uchangie kila kitu kaka, unakuwa kama Kibonde bwana?

Ndugu yangu, come down mweleweshe tu vizuri atakuelewa tu. Ya nini kutumia maneno makali? After all hakuna anayelazimishwa kwenda kwa babu.
 
1. Ezekiel 47:12- Na karibu na mto, juu ya ukingo wake, upande huu na upande huu, utamea kila mti wa chakula, ambao majani yake hayatanyauka, wala matunda yake hayatatindika kamwe; ...matunda yake yatakuw ni chakula na majani yake yatakuwa ni dawa.

2. Ufunuo 22:2- katika njia kuu yake. Na upande huu na upande huu wa ule mto, ulikuwapo mti wa uzima, uzaao, matunda aina kumi na mbili,wenye kutoa matunda yake kila mwezi; na majani ya mti huo ni kuwaponya mataifa.

Kuwa makini unapofanya nukuu usije poteza watu. Hizo passages zote zinamzungumzia Kristo na si miti shamba kama unavyotaka kuwaaminisha watu. Kwa sasa siwezi kuandika zaidi ila tu soma vifungu vifuatavyo:
Mwanzo 2:9, 3:22-24
Yohana 4:7-14
Yohana 7:37,38
Yohana 6:63

SEE YOU LATER

Proverbs 15:4 "a wholesome tongue is a tree of life"
Colossians 4:6 "let your speech be alway with grace, seasoned with salt, that ye may know how ye ought to answer every man"
 
1. Ezekiel 47:12- Na karibu na mto, juu ya ukingo wake, upande huu na upande huu, utamea kila mti wa chakula, ambao majani yake hayatanyauka, wala matunda yake hayatatindika kamwe; ...matunda yake yatakuw ni chakula na majani yake yatakuwa ni dawa.

2. Ufunuo 22:2- katika njia kuu yake. Na upande huu na upande huu wa ule mto, ulikuwapo mti wa uzima, uzaao, matunda aina kumi na mbili,wenye kutoa matunda yake kila mwezi; na majani ya mti huo ni kuwaponya mataifa.
Kwa ma-rastameni hizo aya ulizozinukuu ndio zinahalalisha uvutaji wa bange (mjani)! Nawasilisha.
 
Watu wanasahau yesu alichanganya tope na kumpaka mtu macho akafunguka....kila tiba ina rituals zake.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom