Loliondo na Uhalali wa Mitishamba ktk BIBLIA

Kuna wachungaji wa mshahara wanapotosha watu kuhusu mitishamba!!

Mtaani kwetu
Leo asubuhi nimemsikia mchungaji mmoja wa kanisa flani akikashifu dawa ya Loliondo, alikuwa akitoa muongozo wa maandiko kwa mpangaji wake, amesema;

"Miti yote ina pepo, na watu wote wana mapepo ambayo yanawaongoza kutumia miti na matunda kama dawa badala ya kutumia kama chakula."

Akaendelea kusema,

"Mapepo yalio ndani ya watu ndio yalio waongoza watu 6000 kwenda kunywa dawa Loliondo."

Mpangaji akanywea. Inawezekana wanazuoni hamtapata nafasi ya kupitia aya, hivyo ili kurahisisha mambo nitatupa mbili.

1. Ezekiel 47:12- Na karibu na mto, juu ya ukingo wake, upande huu na upande huu, utamea kila mti wa chakula, ambao majani yake hayatanyauka, wala matunda yake hayatatindika kamwe; ...matunda yake yatakuw ni chakula na majani yake yatakuwa ni dawa.

2. Ufunuo 22:2- katika njia kuu yake. Na upande huu na upande huu wa ule mto, ulikuwapo mti wa uzima, uzaao, matunda aina kumi na mbili,wenye kutoa matunda yake kila mwezi; na majani ya mti huo ni kuwaponya mataifa.

Wazungu watu wabaya sana, wametufanya tuamini kwamba kila kitu chetu ni uupuzi. Jamani hata dawa kutika katika majani? Bila hata uthibitisho unasema DECI wakina kakobe muogopeni Mungu.

Ili mradi hakuna ibada ya mizimu, kupiga ramli, na uchawi, mitishamba inakubalika katika maandiko.

Hivi jaman amjui kua hata izo ARV zimetokana na mitishamba? Mkiletewa dawa na wazungu mnafakamia kubugia,ila ndugu yetu amevumbua kwa uwezo wa Mungu mnampiga vita! Mbona ARV zinasemekana zinaeffect bado tunatumia? Msipinge kitu kama hamkijui. NO RESEARCH NO RIGHT TO SPEAK!
 
Watu wanasahau birika la sloamu...maraika elitibua watu walozama wakapona
 
Hivi mnategemea nini kwa mtu anayejiita kipindupindu??? Akili zake lazima zifanane na jina. Just ignore him/her msije mkaonekana wajinga kwa kubishana na mjinga.
 
Ndugu zangu, tusimdhihaki Mungu wetu. Kile mtu aaminicho ndiyo uponyaji wake. Kuna mtu aliyefuata mtu kumwomba pesa ya kwenda kwa babu?? Kwani mnadharau watu wengine?? Yakimfika anayepinga atamtafuta babu na wala wakati huo hatomwona.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom