Hakuna kesi dhaifu kama hii ya Liyumba; hata wakiweza kumkuta na hatia (which I doubt) kesiyake haiwezi kusimama kwenye rufaa. So.. natabiri mahakama itamkuta hana hatia kwani mzigo wa ushahidi ulikuwa uko kwa serikali. Mtu aliyetakiwa kufikishwa mahakamani alikuwa ni Ballali. So.. kama kesi ya Zombe.. mshtakiwa mwenyewe hayupo! Tatizo serikali itasema inataka kukata rufaa "haijaridhika".. hii ni preview tu ya kesi za Yona, Mgonja na Mramba.
.
Mzee Mwanakijiji, hili nilishalisemea kule nyuma kuwa Liyumba, anaonewa bure!. Haikuhitaji mtu kujua sheria, kuona makosa ya wazi kwenye kesi ya msingi ambayo the charge was defective ab inition (toka mwanzo). Huwezi kumshtaki mtu for the full value ya Twin Tower wakati majengo yapo yale yamesimama na tunayaona kwa macho.
The right forum ilikuwa ni kufanyika kwa thathmini ya thamani halisi ya majengo hayo, halafu unaangalia kiasi kilicholipwa, ndipo Liyumba angeshitakiwa kwa diference btn thamani halisi na cha juu walichoongezea kugawana.
Japo sitetei ufisadi wa aina yoyote, lakini kwa wapenda haki, wangependa kuona Liyumba anatendewa haki, baada ya kukaa jela miaka miwili leo ataachiwa na mawakili wake wataishitaki serikali na atalipwa mamilioni ya fidia.
Kesi ya Kina Mramba, Yona na Mgonja ni hivyo hivyo. Serikali yetu imejaa wanasheria duni, matokeo yake ni kuharakisha defective charges mahakamani at the end of the day, serikali inashindwa.
Niliposema enzi zile kuwa kesi zote hizi pamoja na za EPA, hakuna kitu humo, nilionekana ni mtu wa ajabu, lakini angalau sasa ukweli ndio huu unakuja kudhihirika.