Liyumba akutwa na simu gerezani, How? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Liyumba akutwa na simu gerezani, How?

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Retreat, Sep 8, 2011.

 1. R

  Retreat JF-Expert Member

  #1
  Sep 8, 2011
  Joined: Dec 14, 2010
  Messages: 211
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Hivi hii kesi nyingine ya Liyumba ya kukukwa na simu gerezani mbona mi sielewi, inakuwaje anakutwa na simu gerezani? Yaani iliingiaje na hiyo simu? Au kuna wafungwa wengine hawakaguliwi wakitoka na kuingia tena gerezani labda kama alienda Mahakamani! Halafu mbaya zaidi nasikia Mh. Rais ndiye aliyehoji baada ya kupokea simu kutoka kwa Liyumba akiwa gerezani (Kama ni kweli).
   
 2. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #2
  Sep 8, 2011
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,144
  Likes Received: 2,104
  Trophy Points: 280
  hee!!! hivi alifungwa? nilikuwa nimesha 4get kabisa. alipigwa mvua ngap ndugu huyu aliyetolewa kafara na serikali ya CCM?
   
 3. hashycool

  hashycool JF-Expert Member

  #3
  Sep 8, 2011
  Joined: Oct 2, 2010
  Messages: 5,899
  Likes Received: 442
  Trophy Points: 180
  mvua chache sana 2 tu
   
 4. Lutala

  Lutala JF-Expert Member

  #4
  Sep 8, 2011
  Joined: Jun 17, 2010
  Messages: 845
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  Tatizo ni kuwa kafara huwa haisaidii sana. Ndo maana mzimu wa Liyumba unaendelea kuitafuna serikali. Na utaendelea kuitafuna milele. Kesi ya msingi ya matumizi ya bilioni 221 alishinda wakaishia kumfunga kwa matumizi mabaya ya ofisi ambayo asilimia 90 ya watendaji wetu ndo wako hivi. JK mwenyewe anaongoza kwa matumizi mabaya ya ofisi ndo maana kaishia kuchagua mawaziri ambao hawana tija kwa taifa. watendaji wanaongoza kwa mipango mibovu ambayo inafanya taifa liyumbe kwa kukosa umeme, mafuta, sukari, madarasa mabovu ya shule za msingi, barabara mbovu, makazi mabovu na mengineyo mengi. Kwahiyo, kuendelea kunyanyasa Liyumba eti kwa kuwa alipiga Vicky Kamata ambacho ni kiburudisho cha mzee haisaidii sana. Kesi za wanawake haziwezi kuwa jamabo la msingi kwa taifa wakati watuhumiwa mbalimbali kama kina Chenge, Lowassa, Rosatam Aziz, nk wanapeta mtaani. Heri Liyumba ametuachia majengo pacha ya BOT. Hao wengine mabilioni yetu wameamua kuyalimbikiza nje ya nchi amabayo yanafaidisha mataifa mengine wakati sisi tunataabika. Tanzanians lets change. Lets look issues critically and not superficially. Ukweli ni kuwa Liyumba ni mmoja kati ya maelfu ya wafungwa wetu wanaomiliki vitu mbalimbali magerezani. Kwahiyo ni wazi system ya magereza yetu ni mbovu, ndo maana kabla ya kuwakamata watuhumiwa wa EPA serikali ilitoa mamilioni kukarabati maeneo ya kuwahifadhi watu kama hawa.
   
 5. R

  Retreat JF-Expert Member

  #5
  Sep 8, 2011
  Joined: Dec 14, 2010
  Messages: 211
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Duh! Kwa jinsi nilivyokusoma ina maana hapa ni ishu ya kisasi sasa, Kwa kuwa Liyumba alipiga Vicky basi akatolewa kafara? Halafu sasa hiyo simu yenyewe imegundulika baada ya kumpigia Mh. Rais. Inaonekana nazungumzo hayakumfurahisha Mh. na ndio maana akahoji inakuwaje Liyumba awe na simu gerezani? Eti magereza ndio wakashtuka, hivi inawezekana tukajua waliongea nini? TCRA wanaweza kutusaidia kwa hilo au maongezi na Mh ni confidential?.
   
 6. Lutala

  Lutala JF-Expert Member

  #6
  Sep 8, 2011
  Joined: Jun 17, 2010
  Messages: 845
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  TCRA hawawezi kusema na pengine ukasikia kuwa Liyumba hajawahi kuwa siliana na Rais ili kumaliza utata. Kuna ishu hapa nchini zinatumalizia muda wetu mwingi sana na ambazo hazina tija kwa Taifa. Kosa la Liyumba ni matumizi mabaya ya ofisi na kupiga mademu mbaliambali wakiwemo wa wakubwa wake. Thats all! Kuna watu kibao wametuibia fedha zetu ambazo zingeweza kujenga miundombinu ya nchi na kuifanya nchi yetu kama Rwanda, Botswana, Namibia, Zimbabwe ya zamani, Angola inayochipukia. Watanzania tuna haki ya kuishi maisha bora lakini hilo limekuwa ndoto. Kwangu mimi ingekuwa jambo la msingi kusema kuwa Kamishna wa Magereza Tanzania amefukuzwa kazi kwa kushindwa kusimamia majukumu yake, hilo ndo lingekuwa la msingi
   
Loading...