Liwe ni fundisho kwa yaliyowapata Ben Saanane na Mpoki Mwambulukutu(Mchambuzi)

Kama Ansbert Gulumo alivyoacha kazi akaenda kujichimbia kijijini Kamachumu.Nasikia anafahamu misiba yote inayotokea jimbo zima pamoja na sherehe.
 
Vijana wa dotcom wanadhani kuitetea chama kwenye mitandao ili viongozi wakuone ndo utapata ubunge,wewe umekaa dar unataka kugombea kijijini kwenu sitimbi halafu kampeni unaifanyia Facebook na JF,wakati kuna watu wapo karibu na jamii husuka mda wote.
 
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimebuni mbinu mpya ya kudhibiti mamluki wanaochukua fomu za kugombea kupitia chama hicho kisha kutokomea nazo mitini.

Sasa watakaopitishwa na kupewa fomu za chama hicho kugombea ubunge au udiwani, watatakiwa kusaini fomu maalumu mbele ya mahakama ili wakitokomea bila kurejesha fomu Tume ya Uchaguzi (NEC), wapandishwe mahakamani.

Kauli hiyo imetolewa leo na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Willbrod Slaa kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Viwanja vya Magomeni, Jijini Mwanza.

“Mwaka huu hakuna kupita bila kupingwa, wagombea wetu wote tutawasainisha mahakamani na wakishindwa kurudisha fomu, tutawashughulikia mahakamani,” amesema Dk. Slaa na kuongeza;

najaribu kufikiria validity ya hizo fomu
 
Daaaah, kwa hiyo ile slogan yetu ’TWENDE BUNGENI NA BEN SAANANE’ ndo imeishia ROMBO?? Aseee, naanza kuifananisha na ile ’SAFARI YA MATUMAINI’ iliyoishia DODOMA.Sasa kuhusu ile michango inakuwaje? Maana braza alikuwa anaichanga kwelikweli ili aende bungeni.
Mkuu,
Malipo ya kisiasa ni mazuri ukipata na mabaya sana ukikosa!

Hata hivyo, Ben Saanane atakuwa kwa sasa ameishazoea kuwa dissappointed! Imekuwa hivyo kutokea kwenye Umwenyekiti wa BAVICHA mara mbili, Ujumbe wa Kamati Kuu na sasa Ubunge.

Hata ninampongeza sana kwa kuwa na nguvu za kuendelea kutafuta anachokitaka.
 
Mkuu,
Nimewapa pongezi lakini ni makosa kuingia katika uchaguzi katika msingi wa kujaribu!

Nani kakuambia kuwa walikuwa wanajaribu? Si kwamba waliingia kushindana na wengine na ktk kushindana kuna kushindwa na kushinda, au?

Kwa nilivyokusoma na kukuelewa ni kana kwamba hawa jamaa zetu ilikuwa ni lazima washinde ktk uchaguzi huu wa awali ndani ya chama chao!!

Walikuwa wengi na kwa namna yoyote ni lazima apatikane mshindi mmoja na personaly, ninavyokufahamu wewe Ng'wamapalala hata kama wangeshinda ungekuja na hoja zingine kuwaponda!

Na sbb ya hili ni moja tu, wana CHADEMA!!
 
Kwani wamekwambia walitumia umaarufu wa JF kuwabeba??

Au walikwambia wanahitaji likes za JF kushinda??

Umejuaje kama huko walikogombea wanajulikana? au kosa kuwa JF??

Akili yako ina masizi mwehu wewe hata kufikiri kunakushinda!!!!
 
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimebuni mbinu mpya ya kudhibiti mamluki wanaochukua fomu za kugombea kupitia chama hicho kisha kutokomea nazo mitini.

Sasa watakaopitishwa na kupewa fomu za chama hicho kugombea ubunge au udiwani, watatakiwa kusaini fomu maalumu mbele ya mahakama ili wakitokomea bila kurejesha fomu Tume ya Uchaguzi (NEC), wapandishwe mahakamani.

Kauli hiyo imetolewa leo na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Willbrod Slaa kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Viwanja vya Magomeni, Jijini Mwanza.

“Mwaka huu hakuna kupita bila kupingwa, wagombea wetu wote tutawasainisha mahakamani na wakishindwa kurudisha fomu, tutawashughulikia mahakamani,” amesema Dk. Slaa na kuongeza;

Katibu Mkuu ni nani kama huyu ni naibu?
 
Rombo hatari sana. Hawa angalii umaarufu wa mtu. Kumbuka bwana thirty alimgalagaza two shillings vibaya bila kujali umaarufu wa bwana two shillings. Huyu two o'clock hakuwekeza vya kutosha Rombo.
 
Ubunge unatokea JF tangu lini!?
Ubunge unatokea kwenye shughuli za kijamii. Jinsi gani umejitoa maisha yako kwa jamii husika.
The likes of AFANDE SELE, PROF. JAY
 
Kama Ansbert Gulumo alivyoacha kazi akaenda kujichimbia kijijini Kamachumu.Nasikia anafahamu misiba yote inayotokea jimbo zima pamoja na sherehe.

Imebidi nicheke tu. Yaani watu wana mikakati hasa. Namtakia kila raheli atimize lengo lake.
 
Back
Top Bottom