Livingstone Lusinde: Kwa spidi hii ya Magufuli, 2020 tunaweza tusiwe na uwakilishi wa upinzani

endesha

JF-Expert Member
Dec 9, 2015
1,112
1,455
"Nampongeza Rais Magufuli,amewafanya wapinzani wa nchi hii hawana hoja ya msingi.Ndio maana wakisimama hapa hawana hoja yoyote ya Msingi.Rais Magufuli akiendelea na spidi hii 2020 hatutakua na mbunge wa upinzani hapa."

Haya ni maneno ya Mbunge wa CCM jimbo la Mtera Livingstone Lusinde akichangia bungeni jana.

My take:
Hivi Dodoma hasa mtera,ukosefu wa lishe umewafanya wadumae kiakili mpaka kukosa mtu wa kuwawakilisha bungeni?Dodoma shtukeni mtakuja kukumbuka shuka kumekucha
 
Huo ni kama ushauri wa nguvu za giza!

Anaetoe pongezi yeye mwenyewe anahitaji kupewa semina juu ya siasa ni kitu gani na zaidi elimu ya majukumu ya mbunge Bungeni.
 
Upinzani hawana dira, hawajui wafanye ninj kwa sasa.

Lakini pia ndani ya chama chetu kuna wabunge ambao ni sehemu ya matatizo. Lusinde ni mmoja ya wabunge hao, yeye hana msimamo, alitetea hoja nyingi za ufisadi bungeni lkn leo nae anajifanya yupo na rais.

Wabunge hawa maslai ndani ya CCM mwisho wao 2020.
 
Binafsi sijawahi kumsikia huyu jamaa akiongea jambo la kuisaidia serikali au kuongea jambo linalowagusa wananchi zaidi ya mipasho isiyo na maana.sasa najiuliza nani hana hoja ya msingi kati ya yeye na wapinzani??
Elimu na hekima yake ndiyo inayomuongoza kutenda hayo
 
Hata Mtera mwaka 2020 watahitaji mbunge mwingine aliye makini na mwenye maono kama watataka kupiga hatua.Lakini mbunge wa namna hii, hawezi kutoka kijani na njano.Na jamii ya ukanda ule wana safari ndefu ya kuyataka mabadiliko.
 
Yeye mwenyewe anatamba coz anajua kule ni shamba la bibi.watu hawajafunguliwa kifikra.
 
Niliwahi kuuliza hapa Huyo JASI ya Makyfuli ni IPI ? Hakuna aliyenijibu hadi leo?
NikauliZA ni jambo gani jipya alilolianzisha !kimya ?
 
Utaratibu wa kigezo cha kujua kusoma na kuandika kama ndio kigezo kikuu cha kuwa mbunge kinapaswa kufanyiwa marekebisho mara moja maana tuna wabunge wasioelewa majukumu ya bunge kama mhimili unaojitegemea.

Ukiiona mbunge anapiga vijembe wabunge wenzake kwa kusifia muhimili mwingine(dola), juwa kwamba huyo sio mwakilishi wa wananchi bali kubaraka wa serikali.
 
"Nampongeza Rais Magufuli,amewafanya wapinzani wa nchi hii hawana hoja ya msingi.Ndio maana wakisimama hapa hawana hoja yoyote ya Msingi.Rais Magufuli akiendelea na spidi hii 2020 hatutakua na mbunge wa upinzani hapa."

Haya ni maneno ya Mbunge wa CCM jimbo la Mtera Livingstone Lusinde akichangia bungeni jana.

My take:
Hivi Dodoma hasa mtera,ukosefu wa lishe umewafanya wadumae kiakili mpaka kukosa mtu wa kuwawakilisha bungeni?Dodoma shtukeni mtakuja kukumbuka shuka kumekucha

Huyo Mr Zero hajui kwamba wiki moja katika siasa ni kama muongo mmoja au karne! Asije kushangaa kama kasi ya Magufuli inaweza geuka laana kwa CCM na neema kwa UKAWA akajikuta yeye mwenyewe hana jimbo na CCM ikahamishiwa ICU au kufutika kama KANU ya Kenya!
 
"Nampongeza Rais Magufuli,amewafanya wapinzani wa nchi hii hawana hoja ya msingi.Ndio maana wakisimama hapa hawana hoja yoyote ya Msingi.Rais Magufuli akiendelea na spidi hii 2020 hatutakua na mbunge wa upinzani hapa."

Haya ni maneno ya Mbunge wa CCM jimbo la Mtera Livingstone Lusinde akichangia bungeni jana.

My take:
Hivi Dodoma hasa mtera,ukosefu wa lishe umewafanya wadumae kiakili mpaka kukosa mtu wa kuwawakilisha bungeni?Dodoma shtukeni mtakuja kukumbuka shuka kumekucha

Big up comred Lusinde. Wapeeeeee
 
Eti kasema wapinzani "sindano imeingia...." hahah. Baada ya hapo akaongezea kusema "moto ukiwaka bungeni wapinzani wanakimbia kutoka nje" Na mpaka kufika 2020 hawatakuwepo!! Big Up Lusinde! Wewe ni hazina ya chama!
 
Back
Top Bottom