Livingstone Lusinde awaporomoshea matusi wanaUKAWA

Livingstone Lusinde awaporomoshea matusi wanaUKAWA

Kigodoro

JF-Expert Member
Joined
Apr 25, 2014
Posts
1,665
Reaction score
1,686
Akiwa ameambatana na mgombea mwenza wa urais kule Bagamoyo kwa tiketi ya CCM mama Samia Suluhu, ndugu Lusinde ametumia muda wake wote kutoa matusi dhidi ya wanaUKAWA.

(1)Amesema Lowassa anatembea kama Robot na hawezi kutoa hotuba zaidi ya dakika 2
(2)Amesema Sumaye in kama Popo. Ametoa hadithi ya popo kwamba alikasirika kwavile ameumbwa kama ndege na kama mnyama. Hivyo ndo maana akaamua kuwa anasimama miguu juu kichwa chini ili amnyee mungu. Lakini kwa Bahati mbaya hiyo haja kubwa inamdondokea popo mwenyewe. Na akasema matusi ya Sumaye kwa ccm yatamrudia mwenyewe.
(3)Amesema ccm imejali jinsia ya kike kwa kumuweka Samia kuwa mgombea mwenza. Akasema kwa kuwa Chadema waliwahi kuwatuhumu CUF kuwa wanaunga mkono ushoga, yawezekana mmoja wao kati ya Duni na Lowassa ni mwanamke.
Lusinde ametumia dakika 10 zote alizopewa kuongelea UKAWA tu.
Lakini pia MAkonda, Wema na Ridhiwani walikuwepo lkn hakuna LA maana waliloongea.
 
Kigodoro

Kama ni kweli, basi Mh.Lusinde kauli za maneno yako siku si nyingi zitakurudi, KARMA Inahakikisha ecosystem na cosmos zipo salama, umenielewa mheshimiwa??? ??
 
Last edited by a moderator:
Umekuja na longolongo nyingi bila ushaidi huu nao ni ulofa lete hata picha basi

Mkuu nielekeze namna ya kutupia audio ninayo. Picha siyo ushahidi mzuri sana kwa hili. Nadhani audio ndiyo itathibitisha hili
 
“Ni jamii iliyochoka na kuchakaa; ni jamii iliyooza na kuchoma pua kwa harufu ya uvundo wa rushwa na kujaza nzi wakubwa wa rangi ya Kijani, Ni jamii yenye ufisadi na ukandamizaji; ni jamii isiyojua mbele wala nyuma, ni jamii iliyokosa dira”. Bunge lipo kwa jina tu kwa sababu limewekwa kwapani na watawala; Madaraka ya Rais ni makubwa kwa kiwango cha kupora demokrasia: Utajiri wa nchi upo mikononi mwa kikundi kidogo cha “wateule” na watawala kilichowageuza wananchi wadunda kazi wasiofaidi jasho lao. Na pale maandamano ya wanawake, wanaume na vijana wenye njaa yanapopita karibu na Makazi ya Wenye nacho,Malodilofa husimama ghorofani, wakawatazama na kuuliza, “kulikoni?”. Na walipoambiwa kwamba yalikuwa ya “malofa” wenye njaa waliokosa mkate wa kila siku, wao walijibu: “Kama ni hivyo, kwa nini wasile nyasi na mihogo?”Vijana wanaangamia kwa kukosa maarifa mashuleni na wanaishia kubwia "unga" ambao ni biashara pendwa ya Malodilofa,vijana wasanii wenye vipaji mbalimbali wanageuka ombaomba na wakati wa Kampeni wanakuwa "lulu" kwa kutumika kujaza “nyomi” katika mikutano,wakulima wanazeeka kwa kazi ngumu mashambani na kukosa pembejeo za kisasa na mazao yao yanaishia kukopwa kwa bei ndogo ajabu,wavuvi wanachomewa nyavu zao walizonunua kwa wafanyabiashara wajanja wenye meno,wawindaji wa vitoweo wanaambiwa ni majangili huku tembo wakiuwawa kwa tama ya meno yao na twiga wakipandishwa ndege kwenda ulaya na Asia..Dah! wagonjwa wanakufa huku wamelala mzungu wanne sakafuni mahospitalini kwa kukosa madawa,wakina mama wanajifungulia vichochoroni kwa ubovu wa barabara, Na wanapoona malofa wanawapigia kelele kwa madai yao sahihi wanaamuru majeshi ya ndugu zao wanyonge wawapige mabomu ya machozi na kuwaua na kuwasababishia vilema vya maisha na kuwatesa waandishi wa habari zao za kilofa.Watawala wetu hivi leo wanatuhumiwa kumiliki mabilioni ya fedha wanayomiliki huku wakiyaita ni “vijisenti”, au “fedha ya mboga”, wakati kipato cha Watanzania walio wengi ni chini ya shilingi mia nane kwa siku. Wananchi wanapopiga kelele kugugumia bei kubwa ya kivuko wanaambiwa “Wapige mbizi” na pale ndege ya Rais na rada chakavu inaponunuliwa kwa pesa nyingi zenye asilimia kumi za wajanja wanaambiwa “Ni heri wale nyasi”…Pamoja na mikakati mikubwa na yakutumia fedha na rasilimali nyingi za walala hoi kwa ajili ya kuvuruga "Mabadiliko" kwa kuwanunua wanasiasa uchwara na kuwakashfu kuwa ni “wapumbavu,malofa na mbumbumbu”. Wakati umefika,chama kilichokuwa na dhamana ya haya yote kipumzishwe,ili kijitafakari,kitakapokuja kwa mara nyingine (MUNGU akikijaalia) kije kikiwa kamili....Kwa wakati huu,nathubutu kusema,Naichagua UKAWA,...sio kwa sababu za uimara wa CDM,CUF,NLD,NCCR MAGEUZI ama Uimara wa UKAWA la hasha!!Ila ni kwa sababu ya udhaifu wa CCM na ahadi ilizoshindwa kuzitekeleza kwa miaka 54 mfululizo.“ALUTA Continua, Victoria Ascerta”.... “The Struggle Continues, Victory is Certain”; ...Mapambano yanaendelea, Ushindi unakuja!! ≠HapaNimakwenziTu!!
 
Hili la mgombea mwenza wa UKAWA kuwa nanihiii linajiruda rudia.

Litolewe ufafanuzi jamani. Mbona mnatuchanganya????

Queen Esther

Unapoona dume linajiita queen ni lazima ujue kuwa watu wanafungua buti ya vickswagen hapo!
 
Me nawambia kwa sasa CCM wamebakiza matusi ndo silaha ya mwisho. Jana nasikia bango la Lowasa pale Tazara limeibiwa likabakia la Magufuli pekeee
 
Wameishiwa sera! wanatukana limewashika pabayaaaa! “People think it must be fun to be a super genius, but they don't realize how hard it is to put up with all the idi-ts in the world.”
― Bill Watterson
 
Back
Top Bottom