Kufeli kwa Manure Sokoni au Chelsea sio kigezo wala sababu hata kidogo inayopaswa kutufanya sisi tusisajili kwa uhakika.
Kaka nakubali umekubaliana na sera za usajili kwasababu huna Option nyengine ndiyomana umeamua kukubali matokeo.
Kipindi wanasajiliwa kina Alison, Salah, Mane, VVD, Fabinho, Keita tukabeba Makombe naamini pia ulikubaliana na sera za usajili za wakati huo za kuingia sokoni.
Lakini kwa sasa hatusajili pia unakubaliana na sera zetu za usajili, tukianza tena kumwaga hela sokoni utakubaliana tena na sera za usajili.