Live Updates: Press Conference CHADEMA Makao Makuu Leo tarehe 18/06/2013

Status
Not open for further replies.

CHADEMA

JF-Expert Member
Apr 13, 2013
488
2,468
Ndugu Wananchi popote mlipo ndani na nje ya nchi yetu tuko hapa ofisi ya CHADEMA Makao Makuu Kinondoni Mtaa wa Ufipa kwa ajili ya kuwaletea Live updates za Mkutano na Waandishi wa Habari ambao unatarajiwa kuanza hivi punde. Tutakuwepo hapa kuwaletea live updates. Stay tuned.



Waandishi wanauliza maswali sasa. Swali la 1. Je mko tayari kupokea milioni 100 za serikali, 2. Mtarejea lini bungeni 3. mko tayari kukabidhi video polisi? 4. mnaweza kutupa waandishi wa habari hizo video tuwape Watanzania?


 
kama ni majibu kwa tamko la jana la nape na chama chake mjibuni kwa hoja tunasubili...
 

Tuko pamoja, tushikamane sana wakati huu, kwani kilichofanyika Arusha ni dalili tosha kwamba CCM sasa wamefikia karibu na Mwisho.
 

hiyo press conference itaongozwa na nani? tayari mmeshamaliza kuwazika watu wenu mliowaua?
 
Mkurugenzi wa Habari na uenezi wa CHADEMA Mh. John Mnyika ameshachukua nafasi yake na anasema lengo la Press ni kuzungumzia kauli mbalimbali zilizotolewa ikiwamo ya kauli ya Rais, Lukuvi, Nape na nyinginezo. Mnyika anaanza kwa kuzungumzia rambirambi za Rais kupitia Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu. Anasema anashangaa Rais kusema kuwa shambulio lile lilifanywa watu wasioitakia mema Tanzania wakati kuna ushahidi wa video kuwa aliyehusika nia askari polisi
 
Kama kawaida matamko yasiyokuwa na tija kwa taifa ngoja tusubiri.

mkuu, hawa jamaa wameishiwa sasa. kila siku wanatoa matamko ambayo hayana lolote zaidi ya kujiumbua kutokana na mipango yao ya kidhalimu
 

hapo sasa mnyika anaonyesha kuchanganyikiwa. kweli akili ndogo huwa na fikra finyu
 
Anamtaka Rais alihutubie Taifa kwani yeye ni Amiri Jeshi Mkuu na aeleze ni nani aliyemtuma askari huyo kulipua bomu, askari waliotawanya wananchi na askari aliyeficha kifaa cha mlipuaji.
 
Tuko pamoja, tushikamane sana wakati huu, kwani kilichofanyika Arusha ni dalili tosha kwamba CCM sasa wamefikia karibu na Mwisho.

hawa jamaa kazi ya kuzurura tu. bungeni wamesusia baada ya waziri mgimwa kuwazidi kwa kila angle na sasa wanaamua kuendeleza porojo kwa mambo wanayojua kuwa yametokeaje
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…