Live Updates: Press Conference CHADEMA Makao Makuu Leo tarehe 18/06/2013


Status
Not open for further replies.
CHADEMA

CHADEMA

Verified Member
Joined
Apr 13, 2013
Messages
428
Points
225
Age
26
CHADEMA

CHADEMA

Verified Member
Joined Apr 13, 2013
428 225
Ndugu Wananchi popote mlipo ndani na nje ya nchi yetu tuko hapa ofisi ya CHADEMA Makao Makuu Kinondoni Mtaa wa Ufipa kwa ajili ya kuwaletea Live updates za Mkutano na Waandishi wa Habari ambao unatarajiwa kuanza hivi punde. Tutakuwepo hapa kuwaletea live updates. Stay tuned.

Anasema haiingii akilini eti Polisi ambao ni Watuhumiwa wakuu eti waunde tume ya kujichunguza wao wenyewe!! Mnyika anasema tume hii ya IGP ni ya kinafiki na inalenga kuficha ukweli. Anasema mtu kama Mngulu na Chagonja ni waongo wa mfululizo katika tume mbalimbali ambazo wamekuwa wakiziongoza. Anashauri badala ya watu hawa kuendelea kupoteza fedha za wananchi. Anasema bomu lile kwa ushuhuda wa Wananchi waliokuwepo uwanjani akiwemo mototo mdogo ni dhahiri liliwalenga Viongozi wa Chama chetu. Anasema Serikali,CCM badala ya kuomboleza na wafiwa wao wanaendesha propaganda. Anasema IGP anapaswa kuambiwa na watanzania wote kwamba wajibike au awawajibishe makamanda wake
Anasema baada ya Maombelezo kuisha ni wakati wa kusema kuwa mauaji yametosha sasa. Anawakumbuka Mwangosi, Mbwana Masoud, Ally Zona, Mbwambo na wengineo kuwa wameuawa na hakuna hatua zozote hivyo wakati wa watu kuendelea kuuawa umekwisha sasa. YATOSHA SASA
Waandishi wanauliza maswali sasa. Swali la 1. Je mko tayari kupokea milioni 100 za serikali, 2. Mtarejea lini bungeni 3. mko tayari kukabidhi video polisi? 4. mnaweza kutupa waandishi wa habari hizo video tuwape Watanzania?
Polisi wamekamata vijana watatu wa CHADEMA na kuwapiga na kuwatesa ili wawape mkanda badala ya kuwachukulia kama raia wema. Hivyo kuwapa mkanda imetutia hofu. Lakini mkanda utatolewa baada ya Wanasheria wetu akiwemo Tundu Lissu, Mabere Marando, Prof. Safari kutathmini athari za kisheria baada ya mkanda huo kutolewa. Hatujajadili kuhusu kupokea Milioni za Lukuvi lakini kwa maoni yangu (Mnyika) Lukuvi kutoa dau kwa mauaji yaliyofanywa na polisi wao ni ufisadi mkubwa wa kutaka kufuja hela za serikali kwa kisingizio cha kupata taarifa kutoka kwingineko. Anashauri fedha hizo zielekezwe kwenye maendeleo. Anashangaa Rais kutokutoa rambirambi hata kwa mjane wa Mwangosi. Kuhusu kurudi Bungeni amesema tutarudi lakini Sekretarieti imekubaliana na kauli ya M/kiti na hivyo sasa ni kauli ya Chama kwamba hakuna Mbunge yoyote wa CHADEMA atakayeshiriki vikao vya Bunge hadi taratibu maombolezo yaishe. Anashangaa kwanini Bunge linaendelea wakati katika matukio mbal...imbali kama ya Mtwara n.k bunge limewahi kuahirisha vikao vyake lakini kwa hili la CHADEMA anashangaa bunge kuendelea na shughuli zake. Pia anashangaa kauli ya serikali kutolewa miongozo 4 wakati kanuni haziruhusu kauli ya serikali kuibua mjadala otherwise kauli hiyo inabidi ijadiliwe lakini jambo hilo halikufanyika. ni udhaifu wa Bunge. Anasema wakirudi Bungeni lazima Bunge lieleze kuanzia mauaji ya Arusha, Mwangosi, mateso ya Ulimboka, Kibanda kiasi cha Waziri Mkuu kusema uongo Bungeni. Anasema serikali imekuwa ikikamata watu hewa na kuwapeleka Mahakamani ili kulizuia Bunge lisijadili mambo hayo muhimu yanayowagusa Wananchi kama haya. Anasema watarudi kwa Wananchi na kuwaeleza yote. Anawaomba Wananchi wote walioguswa na misiba hii na iliyopita kushiriki kwenye mazishi kama wako karibu na misiba hiyo na kwa wale waliombali wamtumie ujumbe IGP kwenye namba yake aliyosambaza. Ujumbe wa maombolezo na wa kutaka uwajibikaji. Anasema serikali hii inayojiita sikivu haisikii na hivyo wananchi lazima wailazimishe kusikia kwani yenyewe ndio inayohusika kwenye kadhia zote hizi. Wananchi wanapaswa kuikataa CCM kwanza.
Asema kuna watu wanaamini kikwete ni msikivu lakini kwa hili la mauaji kikwete sio msikivu hata kidogo. na ndio maana amewapandisha cheo wakuu wa polisi wote waliohusika na mauaji. Anasema Serikali ina nafasi nyingine ndogo sana (finyu) kabla maombolezo hayajaisha. Nafasi hiyo ni kuunda tume ya kijaji kuchunguza mauaji haya kwani huko tunakoelekea ni kubaya sana. (NA TUMEFIKISHWA HAPA KWA UDHAIFU WA RAIS, UZEMBE WA BUNGE). Anaulizwa Je CHADEMA wanamkakati gani mwingine zaidi ya kuhusu haya mambo hasa huu uonevu wa Serikali kuhusu swala la Arusha. Kwani wanaua watu na serikali imekataa kutangaza hata kata wazi iliyoachwa na diwani wa CCM aliyehamia CHADEMA? Mnyika anasema watatoa taarifa baada ya maombolezo lakini ijulikane tu kwa sasa kuwa SASA IMETOSHA. "Asantheni kwa kunisikiliza" Anamaliza. Asantheni kwa kutufuatilia
 
mutabilwa

mutabilwa

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2011
Messages
305
Points
0
Age
35
mutabilwa

mutabilwa

JF-Expert Member
Joined Jul 11, 2011
305 0
thanx mtatujuza yatakayojiri!!!!!!!!
 
MAPUMA MIYOGA

MAPUMA MIYOGA

JF-Expert Member
Joined
Jan 30, 2013
Messages
3,469
Points
2,000
MAPUMA MIYOGA

MAPUMA MIYOGA

JF-Expert Member
Joined Jan 30, 2013
3,469 2,000
Patiently waiting.
 
Mzee wa Rula

Mzee wa Rula

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2010
Messages
8,180
Points
1,250
Mzee wa Rula

Mzee wa Rula

JF-Expert Member
Joined Oct 6, 2010
8,180 1,250
Tunasubiri kusikia mengi kutoka katika hiyo press conference
 
Ntale Wi Isumbi

Ntale Wi Isumbi

JF-Expert Member
Joined
Apr 4, 2012
Messages
479
Points
170
Ntale Wi Isumbi

Ntale Wi Isumbi

JF-Expert Member
Joined Apr 4, 2012
479 170
Tunasubiri kusikia yatakayojiri hapa
 
NAPITA

NAPITA

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2012
Messages
5,076
Points
1,250
NAPITA

NAPITA

JF-Expert Member
Joined Apr 2, 2012
5,076 1,250
kama ni majibu kwa tamko la jana la nape na chama chake mjibuni kwa hoja tunasubili...
 
Mvaa Tai

Mvaa Tai

JF-Expert Member
Joined
Aug 11, 2009
Messages
6,177
Points
2,000
Mvaa Tai

Mvaa Tai

JF-Expert Member
Joined Aug 11, 2009
6,177 2,000
Ndugu Wananchi popote mlipo ndani na nje ya nchi yetu tuko hapa ofisi ya CHADEMA Makao Makuu Kinondoni Mtaa wa Ufipa kwa ajili ya kuwaletea Live updates za Mkutano na Waandishi wa Habari ambao unatarajiwa kuanza hivi punde. Tutakuwepo hapa kuwaletea live updates. Stay tuned.
Tuko pamoja, tushikamane sana wakati huu, kwani kilichofanyika Arusha ni dalili tosha kwamba CCM sasa wamefikia karibu na Mwisho.
 
Ritz

Ritz

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2011
Messages
42,245
Points
2,000
Ritz

Ritz

JF-Expert Member
Joined Jan 1, 2011
42,245 2,000
Kama kawaida matamko yasiyokuwa na tija kwa taifa ngoja tusubiri.
 
Lizaboni

Lizaboni

JF-Expert Member
Joined
Feb 21, 2013
Messages
33,841
Points
2,000
Age
35
Lizaboni

Lizaboni

JF-Expert Member
Joined Feb 21, 2013
33,841 2,000
Ndugu Wananchi popote mlipo ndani na nje ya nchi yetu tuko hapa ofisi ya CHADEMA Makao Makuu Kinondoni Mtaa wa Ufipa kwa ajili ya kuwaletea Live updates za Mkutano na Waandishi wa Habari ambao unatarajiwa kuanza hivi punde. Tutakuwepo hapa kuwaletea live updates. Stay tuned.
hiyo press conference itaongozwa na nani? tayari mmeshamaliza kuwazika watu wenu mliowaua?
 
CHADEMA

CHADEMA

Verified Member
Joined
Apr 13, 2013
Messages
428
Points
225
Age
26
CHADEMA

CHADEMA

Verified Member
Joined Apr 13, 2013
428 225
Mkurugenzi wa Habari na uenezi wa CHADEMA Mh. John Mnyika ameshachukua nafasi yake na anasema lengo la Press ni kuzungumzia kauli mbalimbali zilizotolewa ikiwamo ya kauli ya Rais, Lukuvi, Nape na nyinginezo. Mnyika anaanza kwa kuzungumzia rambirambi za Rais kupitia Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu. Anasema anashangaa Rais kusema kuwa shambulio lile lilifanywa watu wasioitakia mema Tanzania wakati kuna ushahidi wa video kuwa aliyehusika nia askari polisi
 
Lizaboni

Lizaboni

JF-Expert Member
Joined
Feb 21, 2013
Messages
33,841
Points
2,000
Age
35
Lizaboni

Lizaboni

JF-Expert Member
Joined Feb 21, 2013
33,841 2,000
Kama kawaida matamko yasiyokuwa na tija kwa taifa ngoja tusubiri.
mkuu, hawa jamaa wameishiwa sasa. kila siku wanatoa matamko ambayo hayana lolote zaidi ya kujiumbua kutokana na mipango yao ya kidhalimu
 
utaifakwanza

utaifakwanza

JF-Expert Member
Joined
Feb 1, 2013
Messages
14,175
Points
2,000
Age
49
utaifakwanza

utaifakwanza

JF-Expert Member
Joined Feb 1, 2013
14,175 2,000
mtueleze pia mkakati wenu kuhusu bomu umefanikiwa au imekula kwenu
 
Lizaboni

Lizaboni

JF-Expert Member
Joined
Feb 21, 2013
Messages
33,841
Points
2,000
Age
35
Lizaboni

Lizaboni

JF-Expert Member
Joined Feb 21, 2013
33,841 2,000
Mkurugenzi wa Habari na uenezi wa CHADEMA Mh. John Mnyika ameshachukua nafasi yake na anasema lengo la Press ni kuzungumzia kauli mbalimbali zilizotolewa ikiwamo ya kauli ya Rais, Lukuvi, Nape na nyinginezo. Mnyika anaanza kwa kuzungumzia rambirambi za Rais kupitia Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu. Anasema anashangaa Rais kusema kuwa shambulio lile lilifanywa watu wasioitakia mema Tanzania wakati kuna ushahidi wa video kuwa aliyehusika nia askari polisi
hapo sasa mnyika anaonyesha kuchanganyikiwa. kweli akili ndogo huwa na fikra finyu
 
CHADEMA

CHADEMA

Verified Member
Joined
Apr 13, 2013
Messages
428
Points
225
Age
26
CHADEMA

CHADEMA

Verified Member
Joined Apr 13, 2013
428 225
Anamtaka Rais alihutubie Taifa kwani yeye ni Amiri Jeshi Mkuu na aeleze ni nani aliyemtuma askari huyo kulipua bomu, askari waliotawanya wananchi na askari aliyeficha kifaa cha mlipuaji.
 
Philip Dominick

Philip Dominick

JF-Expert Member
Joined
May 26, 2013
Messages
1,022
Points
1,195
Philip Dominick

Philip Dominick

JF-Expert Member
Joined May 26, 2013
1,022 1,195
hawa ccm wataumbuka sana mwaka huu
 
Lizaboni

Lizaboni

JF-Expert Member
Joined
Feb 21, 2013
Messages
33,841
Points
2,000
Age
35
Lizaboni

Lizaboni

JF-Expert Member
Joined Feb 21, 2013
33,841 2,000
Tuko pamoja, tushikamane sana wakati huu, kwani kilichofanyika Arusha ni dalili tosha kwamba CCM sasa wamefikia karibu na Mwisho.
hawa jamaa kazi ya kuzurura tu. bungeni wamesusia baada ya waziri mgimwa kuwazidi kwa kila angle na sasa wanaamua kuendeleza porojo kwa mambo wanayojua kuwa yametokeaje
 
Status
Not open for further replies.

Forum statistics

Threads 1,284,210
Members 493,998
Posts 30,817,472
Top