Communist
JF-Expert Member
- Jun 1, 2012
- 5,400
- 1,186
Mkuu hebu nielimishe, sijakusoma, nimekua mjinga hapa.Nakereka na wasiojua kusoma, ITV sio TV
Mkuu hebu nielimishe, sijakusoma, nimekua mjinga hapa.Nakereka na wasiojua kusoma, ITV sio TV
Naona una like ya DR Slaa ,nataka kujua je DR Slaa aliwahi kuwa mbunge kupitia CCM manake tunaambiwa alipotaka kugombea alipendekezwa na jina likakatwa Dodoma ndipo alipogombea kupitia chadema
if you didnt know.!
LEMA ni moja kati ya majembe wa taifa hili.!
chukua hiyo
Katika kipindi cha UZALENDO ambacho huwa kinarushwa kila alhamis-ITV, jana wapipata ugeni kutoka chama cha Demokrasia na maendeleo Chadema ambapo katibu mkuu wa chama hicho DR SLAA alikuwepo na pia upande wa pili alikuwepo makamo mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi(CCM) Mh Mangula.
Mhe Dr Wilbrod Slaa ambaye aliwahi pia kuwa mbunge wa CCM na kujing'atua baada ya kutokuridhishwa na mambo yaliyokuwa yakiendelea ndani ya chama hicho ameeleza kwenye kipindi hicho kuwa alipokuwa mbunge alikuwa aliishi na mtu wa usalama wa taifa katika ofisi yake akiwa kama katibu wake ambaye ndiye alikuwa akiratibu shughuli zote za ofisi yake kwa muda wa miaka 14 ambapo aligundua wadhifa wa katibu wake huyo baada ya kutofautiana na waajiri wake kwa kutokulipwa posho hivyo kuhitaji msaada wa dr slaa.
Dr wilbrod slaa alizungumza hayo alipokuwa akijibu swali la mtangazaji wa kipindi hicho lililouliza kwanini wabunge wa CHADEMA wamekuwa wakizungumza mambo nyeti sana bungeni badala ya kufuata taratibu. Dr Slaa alisisitiza pia kuwa si jambo la kiungwana kuwaacha viongozi walihujumu taifa kwa kisingizio cha kulindwa na usalama wa taifa, lakini pia watu wa usalama wa taifa ndio wahujumu uchumi no 1 huku akichukulia mfano wa wizi wa EPA ambapo kiongozi mkubwa wa usalama wa taifa alihusika kulihujumu taifa.
Ama kwa hakika ninaweza nikasema DR SLAA CCM walimshindwa tangu kitambo kwani pamoja na kutuma watu wa usalama kumchunguza lakini bado wahakuibuka na hoja yoyote ya kummaliza alipokuwa akigombea URAIS mwaka 2010
Umeligundua hilo?Sio siri Jaman Dr Slaa ni mtu wa watu, Mangula zama zake zimeisha kama CCM ilivyokwisha
Tumesoma tumeelewa ITV, juzi saa moja usiku.Someni vizuri tangazo, hapo juu kabisa kumeandikwa itv
Tanzania Daima ni gazeti la UDAKU...
Tanzania Daima ni gazeti la UDAKU...
Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Wilbrod Slaa amelishutumu Jeshi la Polisi na Idara ya Usalama wa Taifa akidai kuwa zinatumika kukilinda Chama Cha Mapinduzi.[/QU
Akizungumza katika mjadala uliomhusisha yeye na Makamu Mwenyekiti wa CCM na kurushwa na kituo cha televisheni cha ITV juzi jioni, Dk Slaa alidai kuwa anao waraka kutoka halmashauri kuu ya CCM unaolihimiza Jeshi la Polisi kuvishughulikia vyama vya upinzani.
Ukweli ni kwamba wigo wa ushindani wa siasa hauko sawa, kwa sababu kila wakati polisi wanatumika na si bahati mbaya.Tuna waraka mkononi uliotoka NEC ya CCM unaoelekeza polisi kushughulikia vyama vya upinzani," alisema Dk Slaa na kuongeza:
"Kuanzia sasa natangaza na anayetaka aje nitamwonyesha, hata polisi waje niwaonyeshe. Kwamba polisi sasa wanatii maagizo ya Halmashauri Kuu ya CCM, hawafanyi kazi kwa mujibu wa sheria za nchi. Bahati mbaya sheria ya polisi ilitungwa mwaka 1959, imefanyiwa marekebisho kidogo 1960/61 na mwaka 2000. Toka wakati huo, sheria za polisi zimekuwa za kikoloni."
Dk Slaa aliongeza kuwa CCM kimetoa waraka kwa watumishi wa umma kutojihusisha na vyama vya upinzani.
"Hivi karibuni baada ya mkutano huo wa Halmashauri ya CCM, imetolewa ‘secular' kwa wafanyakazi wa Serikali. Kwa sasa hivi wanafuatiliwa wana mrengo gani.Akionyesha kuwa ana mwelekeo wa kuiunga mkono Chadema anashughulikiwa," alidai Dk Slaa.
Kuhusu Idara ya Usalama wa Taifa,Dk Slaa alisema kuwa haipaswi kuwa na siri hasa inapohusishwa na uhalifu.
Alitoa mfano wa idara za kijasusi za Marekani (CIA na FBI) akisema kuwa hazina siri zaidi ya utendaji wao.
"Marekani wamemwondoa bosi wa FBI kwa kuwa na uhusiano wa mapenzi na mwanamke. Wizi ni mbaya zaidi kuliko uhusiano wa kimapenzi. Wizi unaathiri, hautakiwi serikalini, kwa taarifa yako siyo usalama wa Taifa tu, hata Mwenyezi Mungu angeiba tungemkemea, kwa bahati mbaya Mungu haibi," alisema.
Aliongeza kuwa, zamani idara hiyo ilikuwa na usiri mkubwa lakini Bunge limekuwa likifanya marekebisho ya sheria zake na bado sheria ya Usalama wa Taifa inahitaji marekebisho makubwa.
Hata hivyo madai hayo yalipingwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM, Philip Mangula aliyekuwa katika kipindi hicho akisema kuwa ushindani wa siasa uko sawa.
Akizungumzia Idara ya Usalama wa Taifa Mangula alisema ni utovu wa nidhamu kuzungumzia mambo yake hadharani.
"Ni utovu wa maadili na wa nidhamu, huwezi ukatoa mambo yako ya ndani. Hata nyumbani kwako, yapo mambo ya kuzungumza chumbani na yapo ya kuongea hadharani. Ukitoka na mambo ya chumbani kuyaongea sebuleni nadhani watu watakushangaa, nadhani siyo tabia nzuri,"
Kuhusu ushindani wa vyama vingi vya siasa, Mangula alisema kuna wigo mpana wa kushindana.
"Wigo wa ushindani ni mpana,tuna vyama 22 sasa vya siasa, lakini tofauti kati ya chama kimoja na kingine siyo rahisi kuisema kwa sasa. Ajenda ya chama kimoja inaanzia na kuishia wapi ni ya chama kujua. Sisi tunayo ilani yetu na sera zetu ambayo tunatakiwa kuitafsiri," lisena Mangula.
Msajili wa vyama vya siasa
Kwa upande mwingine, Dk Slaa akizungumzia vurugu zinazotokea katika mikutano ya chama hicho, alisema kuwa chama chake kimeshapeleka malalamiko kwa Msajili wa vyama vingi, John Tendwa lakini hayafanyiwi kazi.
Tumelalamika mara nyingi, tumezungumza mara nyingi lakini hakuna linaloendelea.
Kumbuka Msajili huyohuyo ananipigia simu ananiambia kuwa Godbless Lema (Mbunge wa Arusha mjini) asiende Arumeru Mashariki kulitokea tishio la vurugu. Maana yake ni kwamba chama kiache kazi yake kwa sababu kuna Watanzania wanatisia kuua, huyo msajili yuko huru?" alisema na kuongeza:
"Msajili huyohuyo ndiye aliyetuandikia tusitishe kwa siku 14 shughuli zetu za siasa kwa sababu sensa inaendelea. msajili huyo ni mwanasheria, anajua sensa haizuii kazi kuendelea. Sisi Chadema hatumuhesabu kuwa mlezi na ndiyo maana kamati kuu ya chama iliamua kuwa hatutashirikiana na msajili wa vyama vingi mpaka aondolewe."
Hata hivyo kwa upande wake Mangula alikanusha kuwepo kwa upendeleo huo huku akisema vyama vyote vina haki sawa.
"Hilo siyo la kweli kabisa, chama chochote kilichosajiliwa kina haki sawa, ndiyo maana tuna vikao kama hivi vya vyama vyote vilivyo na wabunge Bungeni. Hilo lilitokana na CCM na CUF. Katika mwafaka tuliofikia 2001 tulikubaliana tuwe na jukwaa ambalo vyama vya siasa viwe vinatoa dukuduku zao, hoja zao. Badala ya kukaa pembeni na kunung'unika, unasikiliza yale ambayo hutaki masikio kwako,"
Akizungumzia utendaji wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, Dk Slaa alitetea jinsi wabunge wanavyolipuka kwa jazba akisema ndiyo Bunge la Upinzani linatakiwa liwe.
"Hilo ni suala la ‘exposure', kujua nchi nyingine wanafanyaje… Nikiwa Bungeni nakumbuka mwaka 2008 au 2009. Kuna Spika wa Kenya alikuja Bungeni na kusena kuwa bunge letu ni la mapadre, wachungaji na mashehe. Siku mtakapofika mmerushiana viti… ndipo mtakuwa mmepata Bunge," alisema .
Dk Slaa alilalamikia upendeleo unaofanywa na maspika wa Bunge hilo na kusema kuwa haki haiombwi bali inapiganiwa.
Kuhusu utekelezaji wa ilani za vyama, Dk Slaa alisema kwa kuwa hakushinda uchaguzi amebaki kuisukuma Serikali ya CCM kutekeleza ahadi zake.
"Mimi nilitoa ahadi kwa mategemeo kwamba nitaingia madarakani…. Kama CCM watatekeleza, sisi hatuoni wivu kwa sababu watakaonufaika na sera ya CCM, vifaa vya ujenzi vikishuka watakaofaidika ni wananchi kwa kusukumwa na Chadema. Tutaweza kubuni sera nyingine, ndiyo manufaa ya mfumo wa vyama vingi," alisema.
Kwa upande wake Mangula alisema kuwa CCM kina sera na mikakati yake zinazotekelezwa kwa wakati uliopangwa.
SLAA na MBOWE wakiendekeza umbea wa kila siku huenda CHADEMA ikafia mikononi mwao.