Live..mdahalo shivji,kingunge...itv

Tunajiandaa kuwekezwa!!!

wawekezaji, au ni wawekezaji waporaji KISHERIA.

JAMBO LA MSINGI,
TUFANYEJE??
TUENDELEE KUONGEA NA KUONA HURUMA?
HAWA WANAZUONNI WANA HAKI KUONGEA, JE SISI TUNAFANYAJE?
 
Hivi nyie viwavi wa cdm mbona mambo ya ndani ya ccm yanawakuna

kama ni mambo ya ndani ya ccm,why mbunge wenu ayalete kwenye public?hatupo hapa kichama ila tunachotaka ni mabadiliko ya mfumo uliopo na watu wenye uchungu na nchi yetu.gamba ww!
 
Shivji:
Hatukuanza kumsaliti mwalimu juzi, ni miaka 25 iliopita, tulipotoa fursa ya soko huria, sasa tunavuna matunda,
viongozi wote upinzani, na tawala, wanaongozwa na siasa za nje, hatujitegemei kifikra kwa faida ya tanzania

swala si umesoma wapi, umepikwa wapi, bali ni mfumo mzima uliopo, nao unagaliwe
 
Tunaowaita wafadhili, na wawekezaji sasa wao 'kina shivji waliwaita mabepari
 
Nimempenda dogo kutoka makongo fm3 kaongea critically mpaka kashangaza crowd..dogo ni mkali
 
mawazo ya wazee kamwe hayawezi shabihiana na na ya vijana wa sasa.. never.. Tusubiri tu waondoke.. iingie "cream" isiyotokana na ccm
 
Mfuma wa kibepari wa kimataifa unaporomoka, sisi bado tunafikiria wao ndio wakombozi wetu,

sera ya kilimo kwanza: Maana yake ni nini?
Waziri mkuu alienda brazil, tunasema wakulima wadogo wanakunywa pombe, wavivu, hawawezi kujiendeleza, hio ndio kilimo kwanza,
je is that the future?
Investers kutoka nje, mamilioni ya hectares,
hii ni americanization of africa
 
Azimio halikuzungumzia utawala bora, bali uongozi bora, utawala bora ni term kutoka world bank, ndio msamiati mpe,
kuna sera inataka kutungwa, ili mtanzania asiwe na sauti kabisa na ardhi, ili raisi alie madarakani, aweze kumilikisha ardhi kwa anavyotaka,

je ubepari wa kitaifa unakubalika?
 
Majumuisho (yanaendelea...)

2. Prof Issa G. Shivji: Mwalimu alikuwa ni kiongozi mzuri mwenye maadili. Alijaribu kusimamia mfumo japokuwa hakufanikiwa kujenga UJAMAA. Zamani kulikuwa na mabeberu ambao sasa wanaitwa "wawekezaji." Kwa sasa tunaenda kutafuta uongozi toka kwao. Tumeanza kumsaliti Mwalimu tulipoanza mfumo wa Kiliberali mamboleo, tukaleta uwekezaji. Tatizo la sasa ni mfumo. Someni Mwongozo wa CCM wa mwaka 1981 kwamba limejitokeza tabaka jipya dhidi ya Ujamaa, tabaka hilo litashinda. Hakuna Mwongozo mzuri kama huo, utafuteni muusome. Sasa tumeanza kutambua baada ya kuanza Uliberali Mamboleo, miaka 20 sasa, kwamba wakombozi wetu sio wawekezaji. Kilimo Kwanza: PM alienda Brazili, vijana wetu tumewafanya kuwa wavivu. Je, wakulima wetu tunapouza ardhi tunawapeleka wapi? Sisi tunazungumzia juu ya UTAWALA BORA, mimi sipendi UTAWALA BORA bali Azimio la Arusha lilizungumzia juu ya UONGOZI BORA. UTAWALA BORA ni wazo la World Bank. Je, utakuwa na Ubepari wa Kitaifa chini ya Ubeberu? Kuna mabadiliko makubwa ya Sheria ya Ardhi yanakuja ambayo yataleta uwekezaji...
 
kINGUNGE:
NI VIZURI VIJANA WANAANZA KUZUNGUMZIA UJAMAA
ILA INABIDI KUSOMA SANA, KUSOMA, NA KUJUA THEORIES HUSIKA, KUJADILIANA, KUONDOA JAZBA
 
Kuna watu ambao hawana faida kabisa katika jamii yetu zaidi ya kutafuna rasilimali zetu tu kama huyu Kigagula Gobole mwitu,hana cha maana anachosaidia katika nchi hii na yupo tu bado anakula jasho letu,huwa nikimuona nahisi maumivu makali moyoni kwa jinsi ninavyomchukia
 
Majumuisho yanaendelea:

3. Mzee Kingunge Ngombale Mwiru: Nafurahi kwamba kwa sasa watu wanazungumzia Ujamaa kwa sasa......................... Naona uvivu hata kuandika anayozungumza huyu mzee, naona amepitwa na wakati!
 
Nimeipenda hii mzee. kingunge anasema ts better to create our own bourgousies than import foreign bourgousies..
 
Majumuisho (yanaendelea...)

2. Prof Issa G. Shivji: Mwalimu alikuwa ni kiongozi mzuri mwenye maadili. Alijaribu kusimamia mfumo japokuwa hakufanikiwa kujenga UJAMAA. Zamani kulikuwa na mabeberu ambao sasa wanaitwa "wawekezaji." Kwa sasa tunaenda kutafuta uongozi toka kwao. Tumeanza kumsaliti Mwalimu tulipoanza mfumo wa Kiliberali mamboleo, tukaleta uwekezaji. Tatizo la sasa ni mfumo. Someni Mwongozo wa CCM wa mwaka 1981 kwamba limejitokeza tabaka jipya dhidi ya Ujamaa, tabaka hilo litashinda. Hakuna Mwongozo mzuri kama huo, utafuteni muusome. Sasa tumeanza kutambua baada ya kuanza Uliberali Mamboleo, miaka 20 sasa, kwamba wakombozi wetu sio wawekezaji. Kilimo Kwanza: PM alienda Brazili, vijana wetu tumewafanya kuwa wavivu. Je, wakulima wetu tunapouza ardhi tunawapeleka wapi? Sisi tunazungumzia juu ya UTAWALA BORA, mimi sipendi UTAWALA BORA bali Azimio la Arusha lilizungumzia juu ya UONGOZI BORA. UTAWALA BORA ni wazo la World Bank. Je, utakuwa na Ubepari wa Kitaifa chini ya Ubeberu? Kuna mabadiliko makubwa ya Sheria ya Ardhi yanakuja ambayo yataleta uwekezaji...

ndo maaana nasema haya mawazo ni ya kizeee.. vijana wanasinzia tu.. nonsense.. sikia pumba anazoongea 'mwiru ngombale"
 
Alisema nyeyrere 'tunahitaji maarifa na juhudi kuleta maendeleo'
ndio kinachotushinda sie, 'kutumia maarifa katika shughuli zetu'
maarifa ndio mbinu kisayansi na kiteknolojia

waasia wlielewa haraka nguvu ya wakoloni enzi zile ilikuwa maarifa, wakaanza kutumia maarifa katika kutafuta maendeleo na ona waliko sasa,
sisi afrika tulifikiria nguvu ya wazungu ilikuwa kwenye rangi yao, basi ndio tuko hapa.
 
Mbona huyu dingi sielewi anachoongea? Mhhh, namzungumzia Kingunge, eti weupe wa Mzungu ndio nguvu yake.....wakati sisi tunaendesha mambo kwa ushirikina (CCM)
 
majumuisho yanaendelea:

3. Mzee kingunge ngombale mwiru: Nafurahi kwamba kwa sasa watu wanazungumzia ujamaa kwa sasa......................... Naona uvivu hata kuandika anayozungumza huyu mzee, naona amepitwa na wakati!

mimi nadhani ana point japo za kuchambua
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom