Kimbunga
Platinum Member
- Oct 4, 2007
- 14,941
- 9,947
Hatimaye aliyawahi kuwa raisi wa liberia ndugu charles taylor baada ya kutiwa hatiani na mahakama ya kimataifa ya haki za binadamu, leo hii amehukumiwa kutumikia kifungo cha miaka hamsini (50) gerezani.
Suala la kutafakari hapa ni, je adhabu aliyopewa inalingana na kosa alilolifanya kwa nchi na raia wa liberia kwa ujumla?
Je angekuwa ni kiongozi wa nchi za magharibi kama vile marekani angetiwa hatiani na kupewa adhabu hiyo?
Je mahakama hii ya kimataifa ni kwa ajili ya viongozi wa kiafrika tu?
Je kuna haja ya watu wanaotuhumiwa kwa makosa kama ya charles taylor kufunguliwa mashtaka katika mahakama za nchi husika?
Mapendekezo/maoni/ushauri/mitazamo yenu ni muhimu sana.
Siiiungi mkono hii mahakama hata kidogo. Ni mahakama ya kinafiki kweli kweli. Taylor alikamatwa na kufungwa Marekani lakini Marekani wakamwachia (ati alitoroka toka gereza la Marekani!!!!) kwa kazi maalumu. Huo ndio ukawa mwanzo wa vita. Taylor alikuwa akifanya kazi za wamarekani na baada ya kumtumia wakaamua kumtosa. Wao ndio walipanga mpango Taylor apewe hifadhi Nigeria na kisha wao hao hao wakamkamata na kumpeleka kwa Ocampo.
Naamini silaha zinazotumika Afrika zinatoka ulaya magharibi na mashariki. Wanasema Taylor alikuwa akiwapatia RUF ya Fadoy Sankoh silaha baada ya kubadilishana silaha na madini ya almasi; hizo silaha zilikuwa zikitoka wapi? Naamini zilitoka Ulaya. Je hao walaya (wazungu wa ulaya) hawana mikono yao kwenye hiyo vita? Huu ni usanii mtupu. Wantuuzia silaha tunauana kwa maelfu halafu wanamchukua mmoja wanaenda kumpumzisha the Heague.
Hivi Bush kwa viwango vyovyote si muuaji?