List ya Waliomwagwa Uwaziri+Unaibu

List ya Waliomwagwa Uwaziri+Unaibu

si sawa bali ni ufisadi wa kuharibu fund za raia kuhudumia mtu asie na paermanent responsbility. Ni kumlinda tu. Jamaa mgonjwa kwa nini asipishe wengine ajitibie kwanza?
 
Mie nashindwa kumwelewa JK sijui ni mtoto, mwoga au vipi??

Mwandosya anaumwa, angemwacha tu... ajiuguze kwanza, kama ni kwa ajili ya kumsaidia akiumwa ingekuwa akiwa nje

ya uwaziri"".

My Take: Kama kuumwa kingekuwa kigezo cha mtu kinyimwa nafasi za uteuzi, pasingekuwa na anayestahili kuteuliwa nafasi hizo...hebu cheki siha za waheshimiwa wetu..wengi wana utojazo (obesity) uliopitiliza kuashiria wana maradhi ya utapiamlo. Au jipime mwenyewe kabla ya kuwahukumu wengine..Una afya timamu?
 
baada ya kutemwa nini kinafuati? DPP ataintervine? au ushahidi hautajitosheleza kuwapeleka mahakamani au wataachwa wapumzike baada ya utumishi uliotukuka kama Mr BWP alvyoachwa baada ya urais. hapa pia nataka kusikia kauli mbiu kutoka kwa mzee wa kaya juu ya hili baraza jipya lililowekewa viraka. kabla ya kulivunja tena kwa utendaji mbovu!
 
huwezi kuona lolote toka kwa chama kile kile, mtu yule yule, falsafa ile ile na mawazo yale yale. Kama Maghembe alishindwa Pembejeo atawezaje MAJI?
 
Jamani mwenye CV ya waziri wa Fedha atumwagie hapa tafadhali.
 
Plate namba ya gari lake (lazima litakuwa jipya) itasomeka W AW (Waziri Asiye na Wizara)! Sijui jengo la wizara yake litakuwa wapi na wizara sijui itakuwa na watumishi wangapi. Sanaa bana!

Asprin,
yote tisa, kumi sijui hao watumishi wake watakuwa wanafanya kazi gani!!! Kweli sisiemu haina huruma na kodi za wavujajasho.....
 
Last edited by a moderator:
Kwa utaratibu mbovu wa kitanzania, habari ndo kwisha. Ndo maana tunaambiwa Lowassa ni Waziri Mkuu Mstaafu ilihali alijiuzuru kutokana na ufisadi wake ktk RICHMONDS. Hadi Maghembe aliebugi kwenye Pembejeo za Kilimo still kapewa Maji.
 
Mwandosya anaumwa, hakustahili hata kuitwa waziri. Au jamaa kaamua kumtunzia heshima bosi wake wa zamani. Hii serikari ya kishikaji hiiiiii, mweeeeeee!!!!!!!!!!!!
nakwambia hivi huyu ni mshauri mzuri sana ila tu kwa sasa angepumzika na wangemtumia kiushauri zaidi
 
plate namba ya gari lake (lazima litakuwa jipya) itasomeka w aw (waziri asiye na wizara)! sijui jengo la wizara yake litakuwa wapi na wizara sijui itakuwa na watumishi wangapi. sanaa bana!

kazi yake kubwa itakuwa ni kuhudhuria warsha na mikutano ndani na nje ya nchi! kikweteeeeeee!!!!!!!!
 
Hivi Mkisema hatua kali mna maana gani ni ndani ya utawala wa sheria au nje? I do not like this kind of msemo "hatua kali" zipi? Mtu akikosa si anatakiwa kushtakiwa na hukumu inategemea penal code inasemaje kwa kosa husika sasa hii hatua kali kali kali... lugha za wanasiasa ambao mpaka leo hawaheshimu mhimili wa Mahakama!

Nawasilisha!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom