Lissu: Yanayotokea Tarime mpango wa CCM

gambatoto

Senior Member
May 25, 2011
175
28
MBUNGE wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (CHADEMA), amesema kuwa kuna haja ya Watanzania kuungana ili kuzuia mbinu chafu za Chama cha Mapinduizi (CCM) za kugeuza nchi kuwa dola ya kipolisi.

Lissu alisema hayo mwishoni mwa wiki kwenye mkutano wa hadhara wa CHADEMA uliofanyika kwenye viwanja vya kata ya Majengo, Manispaa ya Moshi, mkoani Kilimanjaro.

Akizungumza kwenye mkutano huo, Lissu alisema yanayoendelea kutokea Tarime ni mfano mzuri kuwa lengo la CCM ni kuigeuza Tanzania dola ya kipolisi baada ya Rais Jakaya Kikwete na chama chake kushindwa kuongoza kwa hoja.

“Watanzania tusilifumbie macho suala la Tarime kwa sababu yanayotokea yanatuhusu sisi sote na mwisho ya siku yatahamia katika mikoa mingine kutokana na mipango inayofanywa na CCM kuhakikisha kuwa majimbo ambayo CHADEMA inapendwa yanachukiwa na ikiwezekana kuwaua watu bila sababu,” alisema Lissu.

“Tunachotaka ni kuzuia nchi hii isiweze dola ya kipolisi maana ndio agenda yao pekee iliyobaki, kuwapa polisi uhuru wa kuwaua raia,kuwatesa na kujeruhi,”alisisitiza.

Alisema wananchi hawatakiwi kukaa kimya pindi wanapoona mamlaka yanatumiwa vibaya wananchi wenye ambao ndo wenye mali wana haki ya kuichukua tena mamlaka yao.

Kwa upande wake Meya wa Manispaa ya Moshi, Japhary Michael alisema kuwa Rais anatakiwa kuwachulia hatua viongozi wanaokuwa kikwazo kwenye maendeleo ya nchi, huku akitolea mfano jitihada za CHADEMA kwenye suala la elimu bure kwa wananchi ambalo limekuwa likiwekewa vikwazo.

Source: Tanzania Daima
Lissu: Yanayotokea Tarime mpango wa CCM
 
nikwel lissu hayi unayozungumza ccm wana tabia chafu sana ila ww ngija iko day mambi yatakuwa mtata watakimbia wenyewe nchii hii
 
Nasuburi kwa hamu kusikia kama uongozi wa CHADEMA watatoa tamko kali dhidi ya vitendo hivi vya kiholela vya mauaji ya wananchi mikononi mwa vyombo vya dola.
 
Haya mauaji sioa bahati mbaya au ovyo ovyo
kwa nini yanatokea kwenye majimbo yenye upinzani na serikali tu?
hii ni kutisha wananchi ili waogope na kuchagua ccm kwa kuofoa vita,
Tafsili yangu kwa serikali ya Kikwete ni serikali inayoliwa na watanzania kwa
maisha magumu na sasa roho za watu.
ni raisi wa nchi gani ana kaa kimya kwa mara ya mbili baada ya wananchi wa nchi
yake kuuawa kwa risasi mchana kweupe, ana manufaa na hayo mauaji kweli? ili ni swali gumu
nakumbuka miezi kadhaa iliyopita serikali ya UK walitoa mamilioni ya pound kwa ajili ya kuokoa mtoto
aliyetekwa huko pakistani alipokwenda na wazazi wake kusalimu ndugu.
iweje yeye hao ni watu kumi wameuwa na serikali yake ndani ya miezi mitatu kaa kimya tu.

hakuna mwenye haki ya kuua mtu mwingine kwa sababu zozote zile, hata kama hawana vibali vya kuandamana na sijui nani alivianzisha hivyo vibali maana hiyo ni kubaka haki za binadamu lakini pia kuna njia nyingi za kuwakamata wahusika baada ya maandamano
kwa nini wengi wa polisi walioajiriwa ni machalii sana na na feli wa masomo?
wengi wao wanavuta bangi tu hapa FFU mzambarauni-ukonga busara hakuna kabisa
 
Kwa hali hii tuna kazi kubwa ya kufanya ili kufikia Demokrasia ya kweli.Serikali inapoteza muda mwingi kufikiria namna ya kuwadhibiti wapinzani badala ya kufikiri namna ya kuwapatia wananchi maisha bora ili wananchi haohao wawe na imani na serikali yao.
 
Nasuburi kwa hamu kusikia kama uongozi wa CHADEMA watatoa tamko kali dhidi ya vitendo hivi vya kiholela vya mauaji ya wananchi mikononi mwa vyombo vya dola.

Kama hawafuati sheria wafanywaje ? Lissu amepeleka watu wa kukodi kutoka singida kwenda tarime kufanya fujo mnataka dola iwaachie tu ? hilo haliwezekaniki na polisi wamefanya haki yao regardless Lissu au ni nani
 
mwisho wa police brutality unakaribia, hadi leo hii hapakuwahi tokea katika Africa hii nchi ambayo polisi wake wamepewa madaraka ya kufanya vitendo vya ovyo kama Egypt leo hii dola hiyo iko wapi? sio ndio hao wanaunguza makao yao makuu kupoteza ushahidi wa vitendo vya kinyama walivyokuwa wanavifanya kipindi cha Mubarak? si muda mrefu tutafikia huko tuko njiani
 
Soma historia, utawala wa egypt sio sawa na watanzania. Watanzania tunachagua rais kwa kufuata njia za kidemokrasia , na ndio maana hujaona nchi yeyote ile inayo hoji utawala wa tanzania tofauti na egypt. Tatizo la wapinzani wa Tanzania chama tawala kikishinda , wana sema sio demokrasia , ila kikishindwa ndio demokrasia
 
kwa nini fujo hizi hazitokei kwenye maeneo ambayo hakuna wawekezaji (wanyonyaji) wa madini? au majimbo ambayo si ya CDM?, kuna tatizo gani kama CDM wakitekeleza utawala wa dola?
 
Soma historia, utawala wa egypt sio sawa na watanzania. Watanzania tunachagua rais kwa kufuata njia za kidemokrasia , na ndio maana hujaona nchi yeyote ile inayo hoji utawala wa tanzania tofauti na egypt. Tatizo la wapinzani wa Tanzania chama tawala kikishinda , wana sema sio demokrasia , ila kikishindwa ndio demokrasia

hakuna tofauti yoyote ya utawala wa Egypt na Tz, kule hakukuwa na utawala wa sheria (rule of law), kule kulikuwa na matukio a ukiukwaji wa haki za binadamu hapa hali kadhalika, demokrasia unayozungumzia wewe ni ipi hii ya Tendwa?
 
Nasuburi kwa hamu kusikia kama uongozi wa CHADEMA watatoa tamko kali dhidi ya vitendo hivi vya kiholela vya mauaji ya wananchi mikononi mwa vyombo vya dola.

Kwani bado hujapewa hiyo kazi? Au ndio unawakumbusha? Wasamehe bure walikuwa busy na uchaguzi wa BAVICHA, wamekusikia sasa na wewe ule.
 
Katika Dunia ya leo Kifo chochote ni lazima kufanyiwa Uchunguzi (Coronary investigation) kutathmini chanzo na asili ya kifo. Vyombo vya ulinzi kama polisi na jeshi kwa msingi wa uwepo wake katika jamii havitegemewi kusababisha kifo chochote cha mwananchi. Hivi sasa katika kipindi ambacho bado tunatafakari kilichotokea Tarime tunapokea taarifa ya jeshi kusababisha kifo cha mwananchi Tabora. Hapa utagundua kwamba jeshi la polisi linaua na kwakua uchunguzi wa vifo haufanyiki na unapofanyika unawapendelea polisi ni kweli anayoyasema Lissu yataendelea kutokea kila mkoa wa nchi yetu. Kwakua tumeshindwa kuwachukulia hatua Polisi walioua raia ili kuwapora pesa (Zombe Case) na hakuna dalili ya kuwajibisha polisi kwa mauaji ya Tarime na Tabora ni wazi kwamba kila mwananchi wa Tanzania afahamu kwamba hayuko salama. "Wembe uliowanyoa" Wachimba Madini wa Ulanga, wananchi wa Tarime na Tabora unakufuata tia maji.
 
Asema vijana waliokufa Tarime waliitwa na POLISI.
Waliwaita wakachukue madini baada ya kutoa pesa.
Bahati mbaya wakafumaniwa,wakawageuka vijana.
Pia a toboa jinsi polisi wanavyoua wafanyabiashara.
Kisha huchukua mali zao na kusema ni majambazi.
Waliouawa kimyakimya bila maziko sasa wazidi 100.
"Ni kwamba polisi pamoja na maafisa wa mgodi huo wanamtindo unaojulikana kama MCHONGO.Wanapojua kua kesho mafundi watalipua baruti,huenda mjini kuchukua pesa kwa vijana,kama malipo ya kuwaruhusu kuchukua madini"
Source:SEMA USIKIKE.
 
Soma historia, utawala wa egypt sio sawa na watanzania. Watanzania tunachagua rais kwa kufuata njia za kidemokrasia , na ndio maana hujaona nchi yeyote ile inayo hoji utawala wa tanzania tofauti na egypt. Tatizo la wapinzani wa Tanzania chama tawala kikishinda , wana sema sio demokrasia , ila kikishindwa ndio demokrasia

Hivi kumbe wizi na uchakachuaji wa kura kwa tafsiri ya kifisadi ni demokrasia?
 
huo mtindo wa polisi kula njama na walinzi wa mgodi ni kweli kabisa,mererani kwenye machimbo ya tanzanite walinzi wanapewa hela na wachimbaji alafu usiku wanazama kwenda kupiga moto kivyao na wanapakua madini.tofauti na hayo ya nyamongo nikua huku walinzi ni wafanyakazi waajiriwa wa kampuni ya tanzanite one,huwa hawana haja yakukiuka makubaliano kwani hela wanayochukua ni nyingi sana si chini ya milioni thelathini mpaka hamsini alakini infomation inatakiwa iwe parfect kuwa mkiingia mgodini mkipiga chorongo moja tu mmekua mamilionea.kwahiyo lisu anaposema kua mapolisi wamekula dili na kuwageuka wenzao ni sahihi kabisa.polisi huwa si watu wa dili kabisa huwezi cheza dili na polisi ukafanikiwa hatasikumoja,sanasana atakugeuka akupekesi au akuue ndio dili wanayoweza.
 
hatua hua ziko hivi;
1.leadership crissis
2.rigging elections
3.supressing oposition (through police etc)
4.people awareness
5.overthrowing the system
6.new order
sisi tupo hapo kwenye namba 4
 
Matukio mengi ya kusikitisha yametokea ambapo polisi wameingilia mambo mengi ya siasa kwa kutumia nguvu iliyozidi kiasi na kusababisha mauaji mengi ya wananchi, kukamatwa na kufungwa kwa viongozi wa siasa na wananchi. Hali hii inatokea badala ya serikali kushindwa au kukataa kutatua migogoro kwa kufuata kanuni na misingi iliyowekwa. Je hali hii ya serikali kuzidi kutegemea vyombo kandamizi vya dola, inaashiria kuwa Tanzania inaendeshwa kipolisi na kuwa nchi ya kipolisi (police state)?
 
Kama hawafuati sheria wafanywaje ? Lissu amepeleka watu wa kukodi kutoka singida kwenda tarime kufanya fujo mnataka dola iwaachie tu ? hilo haliwezekaniki na polisi wamefanya haki yao regardless Lissu au ni nani

Mkuu Lisu hakukodi watu ila alikuwa na mbunge mwenzake pamoja na viongozi wengine wa Chadema. Au mkuu nchi hii, kiongozi wa Chadema akifuatana na Waziri kivuli ( Tundu Lisu) kwenda kuona yanayotokea tarime kwa kutumwa na chama chake ni kukodi watu? Au ni kosa? Nadhani mwanakijiji yuko sahihi Chadema lazima watoe tamko.
 
Back
Top Bottom