Lissu: Yanayotokea Tarime mpango wa CCM

Lissu: Yanayotokea Tarime mpango wa CCM

Tamko la nini? Waende mbali zaidi ... Nguvu ya umma itumike kumuondoa agp saidi mwema, haiwezekani watu wanakufa tunasikia matamko for what... Hebu chukueni maamuzi stahiki .... Nguvu ya umaa- watu kukashinde hapo ofisini kwa mwema mpaka kieleweke wakati huo tundulisu na wenzio waburuzeni hawa jamaa mahakamani mwena na nahodha wanachekacheka tu katiba inavunjwa... Tamko halina haja kuna tamko na report ya kituo cha haki za binadamu wametoa kila kitu jeshi la polisi linavyouwa watu ovyo nguvu ya umma itumikee
 
Kama hawafuati sheria wafanywaje ? Lissu amepeleka watu wa kukodi kutoka singida kwenda tarime kufanya fujo mnataka dola iwaachie tu ? hilo haliwezekaniki na polisi wamefanya haki yao regardless Lissu au ni nani

Sasa hapo ni nani ambaye hafuati Sheria CDM au CCM!
Unauhakika kama Lissu alikodisha watu???
Je!aliwalipa kiasi gani KOFIA,T-SHIRT, CHAKULA NA VINYWAJI + USAFIRI kama wafanyavyo CCM au njia gani Lissu alitumia kuwalipa hao aliowakodi.... halafu tangu lini ulisikia CDM wanakodisha watu??
Polisi wamefanya haki yao ya kuuwa watu ovyo?? ama ndio sheria ya nchi inasema polisi wawe wanauwa wananchi ovyo!??
 
Matukio mengi ya kusikitisha yametokea ambapo polisi wameingilia mambo mengi ya siasa kwa kutumia nguvu iliyozidi kiasi na kusababisha mauaji mengi ya wananchi, kukamatwa na kufungwa kwa viongozi wa siasa na wananchi. Hali hii inatokea badala ya serikali kushindwa au kukataa kutatua migogoro kwa kufuata kanuni na misingi iliyowekwa. Je hali hii ya serikali kuzidi kutegemea vyombo kandamizi vya dola, inaashiria kuwa Tanzania inaendeshwa kipolisi na kuwa nchi ya kipolisi (police state)?

Kutumia vyombo vya dola ni dalili moja ya CCM kuwa mahututi. CCM hawafanyi tena kazi ya siasa. iko wapi CCM Jabali? sasa ni jabali la kuiba kura, ni jabali la kuegemea majeshi ya ulinzi na usalama: hilo si jabali tena bali ni mpira wa miguu usiokuwa na upepo ndani yake. Kolimba alisema huko nyuma kwamba CCM haina dira, wakamjia juu. walitakiwa wakae chini na kutafakari. kila kukicha ushahidi unazidi kujitokeza kwamba CCM ni kama gari ambalo halina breki na dereva ameshasepa. sasa abiria inabidi "tuchanganye na akili zetu" tusije angamia wote.
 
Katika sayansi ya siasa, polisi (coercive instruments) ni mifumo (structures) zinazoundwa kwa ajiri ya kuwalinda (to protect) watawala (ruling class)i.e ellites,politicians,businessmen n.k na masrahi (interests) zao na mifumo hii are oppressive in nature dhidi ya watawaliwa (ruled class)...

Kwahyo kwa wanayoyafanya polisi huna haja ya kushangaa,hawapo kwa ajiri ya raia bali wako kwa ajiri ya watawala.
 
Tuanzishe mapambano na polisi hapo tutajikomboa si hivyo watatumaliza.
 
Tumeona kila mara maamuzi ya polisi Tanzania na yote haya yanatokana na sisi wananchi kutokutafakari maneno ya katiba ya ccm. Tumekua tunasikitika kukitokea jambo fulani na kushangaa kwamba polisi wa Tanzania hawana tofauti na wale polisi wa Egypt kipindi cha Mubarak. Kumetokea majanga mangapi Tanzania ambapo polisi wamechukua orders kutoka kwa kikwete yeye mwenyewe na wafuasi wake na kuwaua wananchi? Leo sipendi kuzungumia vitu vingi toka administration zilizopita ila yanatutosha kuzungumzia kipindi hiki cha kikwete (Tanzania dark period).

Tukizungumzia jinsi gani Polisi wanaua wananchi na kutokuwepo kwa any open investigations au accountability katika nchi, tunaona yapo maswala mengi ya kudiscuss. Tuangalie jinsi swala la mauaji huko Tarime, jinsi gani wananchi wamepigwa risasi za vichwa na tunajua hili ni jambo la mwezi huu huu. Polisi wakajichukulia hatua hata kutaka kuzuia any kind of investigations kwenye miili ya waliouliwa. Hapa ni nani anatakiwa kuzungumzia jinsi ya vyombo vya polisi badala ya kusaidia kuhakikisha kuna justice and security kwa wafiwa na familia zao wao wamekuja na kutetea wauaji na kudhubutu hata kutupa maiti za wananchi barabarani. Haya maamuzi yanaonekana mojo kwa moja yanatoka kwenye ngazi za juu makao makuu ya polisi na kushirikiana na kikwete mwenyewe.

Tukichunguza swala jingine la violations kwa watanzania, mauaji ya Arusha ambako wananchi walikuwa barabarani kuandamana kudai haki zao. Siku kabla ya maandamano tumegungua mkuu wa polisi makao makuu aliingilia kati na kupinga maamuzi ya mkuu wa polisi Arusha na kilichotokea ni mipango ya kuzima midomo wananchi na kibaya zaidi kutokea kwa mauaji ya kutisha Arusha. Tena na tena polisi wametumia deadly forces kuwaua wananchi wasio na silaha na kudai hawakutakiwa kuandamana kinyume na katiba yao mwenyewe walivyoiandika. Tukiangalia matukio ya magala ya silaha Mbagala na Gongo la Mboto, yote yametokea chini ya waziri Mwinyi na kikwete mwenyewe. ccm haioni umuhimu wowote ule wa justice na security ya Watanzania ila wanajiimarisha security yao kujilinda na kuhakikisha hakuna Mtanzania yeyote yule ataquestion madai yeyote kuhusu nchi yao. Hizi pattern za violations za decent human being lazima tuzifanyie kazi kama wananchi wa nchi zingine wanavyofuata taratibu UN Human Rights na Organizations zingine duniani. Watanzania tuna evidences na motives za kutosha kukomboa wananchi wenzetu leo na sio kusubiri mauaji mengine yatokee.

Nimefanya uchunguzi kuhusu Martial aws Egypt na Baharen na nimeona pattern of simillarities. Martial law za Egypt na Baharen lengo kubwa ni kuwadhibiti wananchi na kupinga any kind of revolt kutoka kwa wananchii. Wananchi wa Egypt na Baharen wananyimwa haki zao kuuliza maswali yeyote kuhusu uongozi wa nchi na hasa maswali yanahusu corruptions za viongozi wa nchi.
Egypt's generals impose martial law
Tumeona tangu Mubarak aondolewe madarakani wamisri wameweza kupata freedom of press na hasa kuweza kujiandaa kuchagua viongozi kwa kutumia katiba ya usawa bila upendeleo. Huko Baharen tangu Martial law ipitishwe wananchi wanauliwa kwa kupinga utawala wa mfalme.
Bahrain declares martial law as protesters clash with troops | World news | The Guardian
Je Tanzania tunauliwa kwa kupinga ccm? Hii ni wazi kabisa matukio ya mauaji Tanzania yanalengo la kuwamaliza wapinzani na kuwanyamizisha wapinzania na wananchi kwa kutumia hidden Martial law
HUMAN RIGHTS: An Outbreak of Martial Law - TIME
International Journal of Leadership Studies - Democratic Leadership: The Lessons of Exemplary Models for Democratic Governance
List of Issues

"Martial law can be used by governments to enforce their rule over the public. Such incidents may occur after a coup d'état (Thailand 2006); when threatened by popular protest (China, Tiananmen Square protests of 1989); to suppress political opposition (Poland in 1981); to stabilize insurrections or perceived insurrections (Canada, The October Crisis of 1970)"​
 
Tunasubiri tamko la chadema! Serikali ipo likizo naona,inasubiri 2015 ianze kampeni tena..

..ole wao wanaominya haki za raia,kwani hawataweza kudumu. Na siku jamii ikichoka hawatarudi nyuma mpaka kieleweke.
 
Kama hawafuati sheria wafanywaje ? Lissu amepeleka watu wa kukodi kutoka singida kwenda tarime kufanya fujo mnataka dola iwaachie tu ? hilo haliwezekaniki na polisi wamefanya haki yao regardless Lissu au ni nani

Mbona unatumia uwongo kuhalalisha mauaji ya raia wenzako? Ugenius wako wa kuchakachua tu kilaza mkubwa wee
 
Hivi mshindi wa Urais wa uchaguzi wa oktoba ni nani vile ?

Humjui?? nasikia eti nchi imemshinda kabisaaaaaaaaa, maana watu wanachinjwa kama jogoo, mbuzi, njiwa n.k. huku yeye anachekelea tu! loooooo! enzi yangu mimi tulikuwa wakali sana na dhuruma, nililinda na kutetea haki na kuondoa unyanyasaji aina zote.
 
MBUNGE wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (CHADEMA), amesema kuwa kuna haja ya Watanzania kuungana ili kuzuia mbinu chafu za Chama cha Mapinduizi (CCM) za kugeuza nchi kuwa dola ya kipolisi.

Lissu alisema hayo mwishoni mwa wiki kwenye mkutano wa hadhara wa CHADEMA uliofanyika kwenye viwanja vya kata ya Majengo, Manispaa ya Moshi, mkoani Kilimanjaro.

Akizungumza kwenye mkutano huo, Lissu alisema yanayoendelea kutokea Tarime ni mfano mzuri kuwa lengo la CCM ni kuigeuza Tanzania dola ya kipolisi baada ya Rais Jakaya Kikwete na chama chake kushindwa kuongoza kwa hoja.

“Watanzania tusilifumbie macho suala la Tarime kwa sababu yanayotokea yanatuhusu sisi sote na mwisho ya siku yatahamia katika mikoa mingine kutokana na mipango inayofanywa na CCM kuhakikisha kuwa majimbo ambayo CHADEMA inapendwa yanachukiwa na ikiwezekana kuwaua watu bila sababu,” alisema Lissu.

“Tunachotaka ni kuzuia nchi hii isiweze dola ya kipolisi maana ndio agenda yao pekee iliyobaki, kuwapa polisi uhuru wa kuwaua raia,kuwatesa na kujeruhi,”alisisitiza.

Alisema wananchi hawatakiwi kukaa kimya pindi wanapoona mamlaka yanatumiwa vibaya wananchi wenye ambao ndo wenye mali wana haki ya kuichukua tena mamlaka yao.

Kwa upande wake Meya wa Manispaa ya Moshi, Japhary Michael alisema kuwa Rais anatakiwa kuwachulia hatua viongozi wanaokuwa kikwazo kwenye maendeleo ya nchi, huku akitolea mfano jitihada za CHADEMA kwenye suala la elimu bure kwa wananchi ambalo limekuwa likiwekewa vikwazo.

Source: Tanzania Daima
Lissu: Yanayotokea Tarime mpango wa CCM

Mzunguko wa pesa kutoka migodini kwenda CCM upo?😛ound:
 
Kama hawafuati sheria wafanywaje ? Lissu amepeleka watu wa kukodi kutoka singida kwenda tarime kufanya fujo mnataka dola iwaachie tu ? hilo haliwezekaniki na polisi wamefanya haki yao regardless Lissu au ni nani

Mkuu
Kwa heshima kubwa sana naomba nitoe wazo langu kwamba "Jina unalolitumia haliendani na post unazozitoa hapa jamvini", huo ni mchango wa mawazo tu siyo kwamba ninadhalau mawazo na topic zako.
 
Back
Top Bottom