Lissu: Wanaotaka kuondoka CHADEMA ruksa

Lissu: Wanaotaka kuondoka CHADEMA ruksa

Sijuwi nimemfahamu Lissu au vipi, inamana Lowassa atakuwa rais wa Ukawa??? itakuwaje kwenye kampeni ccm wakileta documents japo za kughushi kuhusu ufisadi kwa Lowassa?? na je Ukawa itapambana vipi na ufisadi ilhali Rais atakayesimamishwa kama ni Lowassa alishawahi kunaswa na harufu ya ufisadi?

Ukawa itakuwa na nguvu gani kupambana na hili na vipi bungeni wataweza kusimama tena kupinga ufisadi? Lissu ningependa zaidi angeogelea kwenye haya.

Tutakitumia chuma chakavu kuzalisha chuma kipya na imara zaidi. Chadema ni watamu sana wamewakamata sawasawa! Huu ni mpango wa Mungu. Endeleeni kuhamasisha tume iongeze machine maana mshaanza kuwa wapinzani mapemaaa!!
 
Sawa bakini na chama chenu,

Lakin Lissu kaa ukijua kile ni chama cha kina Mbowe na jana alisema tena usijione umefika
Kwa hiyo zile mil 300+ alizosema Slaa pia alishawajibika?

Ondoka tu ndugu kwani hakuna namna nyingine, utauachaje mtaji mkubwa kiasi hicho? Mabadiliko ni hatua. Huo ni uhuru wako lakini ukirudi CCM utakuwa umepoteza zaidi.
 
....watanzania ni watu wa kuogopwa sana kwa undumilakuwili wao.! Slogan ya "Safari ya matumaini" ilivyoanza walikuwa wa kwanza kuiponda kuwa "watanzania" wanahitaji "safari ya uhakika"! Hakijapita kitambo mara na wao wanasema "safari ya matumaini" itaendelea "huku"...! We fail because we don't stand by what we believe in! As a country tuko kwenye eneo kipindi cha ajabu sana ambapo watu minds zao zinabadilishwa kiurahisi namna hii...!
 
TUNDU-LISSU-SEP-06-620x307.jpg



MBUNGE wa Singida Mashariki na Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Tundu Lissu, amesema chama chao kinatarajia kupata wanachama wengi baada Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa kujiunga na chama hicho.

Lissu ametoa kauli hiyo baada ya kuwepo taarifa kwamba wapo wanachama wa Chadema ambao watakihama chama hicho kutokana na kutokubaliana na ujio wa Lowassa ndani ya Chadema.

Akizungumza leo na waandishi wa habari Lissu amesema, “Kama wapo watakao jiondoa Chadema, wengi zaidi watakuja. Tupo katika kipindi ambacho hatujawahi kuwepo tangu mfumo wa vyama vingi uanze.

Mfumo tawala unabomoka vipande vipande. Unapo bomoka, dalili zake ni watu ambao wamekuwa katika mfumo huo kuondoka kama alivyofanya Lowassa.”

“Mabadiliko katika nchi yanatokea pale mfumo tawala unapo pasuka. Lowassa ni mfano mzuri.

Tunamkaribisha kwetu sio kwa sababu ni mwanasiasa msafi. Tumempokea kwa sababu tunaongeza nguvu kubwa kwa wale wanaotaka mabadiliko. Imetokea Zambia Mawawi, Nigeria na Kenya,” amesema Lissu.

Akizungumza kuhusu Chadema kumtuhumu Lowassa kwamba “ni fisadi” kabla ya kujiunga na chama hicho Lissu amesema, “…hatukuwa na makosa hata kido kumweka Lowassa katika kundi la watuhumiwa wa Richmond. Mambo yalizungumzwa bungeni. Aliwajibika na amesema mwenyewe aliwajibika.”

“Alijiuzuru uwaziri mkuu kwa sababu ya Richmond. Tulimweka katika orodha ya mafisadi kwa sababu ya Richmond. Na jana alisema alimwambia rais “tuvunje mkataba” rais akaataa. Angefanyeje?. hilo ni vumbi, litakapo tulia Chama Cha Mapinduzi na mfumo tawala utakuwa umeanguka, tutajenga nchini.Bila kuvunja mfumo tawala hakuna kusonga mbele,” ameeleza Lissu.

Nadhan lisu yuko kwenye mwezi wake si bure.kwani list of shame ilizungumza habari za Richmond.mpuuzi kweli huyu kichaa wenu mnayemwamini.
 
(Quote)
Alisema alimwambia rais "tuvunje mkataba" Rais akakataa....
 
Lowassa kajiunga na UKAWA kwa kupitia chama cha Chadema.

Kungelikuwana sheria ya kugombea bila chama, ingelikuwa njema zaidi.

Ukawa ni dalili nzuri za kuja kuruhusu Wagombea wasio nq chama.....

Ndio maana hili la mgombea binafsi lilikataliwa katika katiba mpya, walijua kuna watu hawataridhika wakikatwa na kutafuta mlango mwingine.
 
Tuko pamoja kamanda lengo ni kuing'oa CCM, mengine yatafuata,.. Mtindo wa kushabikia vya kushindwa kila siku tumechoka,..
 
ok sawa naondoka maana hakuna aliyenilazimisha kuwepo ni maamuzi yangu sifungwi..

masikiiiini!!! sasa unaenda wp? maana mafisadi sasa yatakuwa yako kila chama, ccm bado yapo, chadema yanakuja, cuf yapo ACT yapo. Tukubaliane wooote kuwa mzizi wa tatizo ni mfumo wa CCM sio mtu mmojammoja. Binafsi mwaka 2005 imani yangu kwa Rais Kikwete ilikuwa kubwa sana hasa kutokana na kupitia jeshi hadi ngazi ya kanali, kuwa kijana na kuonyesha kukerwa na uuzwaji wa nyumba za serikali. mimi na familia na marafiki tukashawishiana kumpigia akapita kwa kishindo, hivyo sikutarajia kama chini ya utawala wake ningesikia kuwa tembo wanapungua, twiga wanabebebwa wazima wazima, richmond, escrow n.k. hivyo ndiyo nikaamini kuwa tatizo sio mtu wa kuwa rais au anayetuibia bali mifumo yetu ya chama tawala, serikali, katiba na sheria zetu. Bila kufanya marekibisho kwenye taasisi hizi hata tukimchagua nani tutalia tu. HIvyo kumshupalia Lowassa kuwa hafai ni kupoteza lengo. Na anayefikiria hivyo basi haoni mbele. Tatizo letu sasa limekuwa tutawezaje kuiondoa au kuibadilisha mifumo yetu hii ambayo ndo chanzo cha watu kuwa mafisadi? Jibu lilikuwa gumu sana kwakuwa ccm ilikuwa imara mno huku ikiwa na uwezo wa kuyatumia magari ya deraya, washawasha, mabomu, silaha za moto, virungu vya polisi, tume ya uchaguzi, uteuzi mbalimbali, bunge, mahakama viweze kutii matakwa yake dhidi ya upinzani. LAKINI sasa mungu si athumani bwana! mwaka huu ni tofauti sana, CCM imepata homa ya uti wa mgongo iko mahututi. Sasa kwa akili za kawaida tu hii ndo fursa pekee ambayo adui unaweza kuukanyaga mrija unaopeleka Oxygen kwa mgonjwa CCM ili hewa isifike kwake ili afe, na namna pekee ya kufanya hivyo ni kuwatumia wahudumu wa mgonjwa waliokuwa pia hawaridhishwi na tabia na matendo ya mgonjwa huyo (ccm). Hivyo miongoni mwa wahudumu hao ni akina Lowassa na wenzake ambao ndo wanamjua vema mgonjwa huyo na wanafahamu saa ya kumuona mgonjwa na saa manesi wanakuwepo wodini. Anayesema tuiache fursa hii ana lake jambo, hatutakii mema wapenda mabadiliko. Ajitafakari upya, maana joka likipona kwenye ugonjwa huu uliompata safari hii litajiimarisha vibaya sana na tutakuwa hatuliwezi tena.
 
Lowasa alikuwa kwenye kundi la wezi. Tayari alishatoka huko. Hakuna mwenye hati miliki ya urais wa nchi hii. Yeye siyo mwanasiasa mbumbumbu aseme basi baada ya jina lake kukatwa kule dodoma. Huyu ni nelson madela wa Tanzania. Lowasa baba chapa mwendo
 
Sijawahi Pata Furaha Kama Hii Baada Ya Kusikia Lowasa Kaingia Chadema,Ni Wakati Wa Mapinduzi,ukawa Ccm Byebye
 
Back
Top Bottom