Lissu: Wanaotaka kuondoka CHADEMA ruksa

Lissu: Wanaotaka kuondoka CHADEMA ruksa

PISTO LERO

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2011
Posts
2,819
Reaction score
1,458
TUNDU-LISSU-SEP-06-620x307.jpg

MBUNGE wa Singida Mashariki na Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Tundu Lissu, amesema chama chao kinatarajia kupata wanachama wengi baada Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa kujiunga na chama hicho.

Lissu ametoa kauli hiyo baada ya kuwepo taarifa kwamba wapo wanachama wa Chadema ambao watakihama chama hicho kutokana na kutokubaliana na ujio wa Lowassa ndani ya Chadema.

Akizungumza leo na waandishi wa habari Lissu amesema, "Kama wapo watakao jiondoa Chadema, wengi zaidi watakuja. Tupo katika kipindi ambacho hatujawahi kuwepo tangu mfumo wa vyama vingi uanze.

Mfumo tawala unabomoka vipande vipande. Unapo bomoka, dalili zake ni watu ambao wamekuwa katika mfumo huo kuondoka kama alivyofanya Lowassa."

"Mabadiliko katika nchi yanatokea pale mfumo tawala unapo pasuka. Lowassa ni mfano mzuri.

Tunamkaribisha kwetu sio kwa sababu ni mwanasiasa msafi. Tumempokea kwa sababu tunaongeza nguvu kubwa kwa wale wanaotaka mabadiliko. Imetokea Zambia Mawawi, Nigeria na Kenya," amesema Lissu.

Akizungumza kuhusu Chadema kumtuhumu Lowassa kwamba "ni fisadi" kabla ya kujiunga na chama hicho Lissu amesema, "…hatukuwa na makosa hata kido kumweka Lowassa katika kundi la watuhumiwa wa Richmond. Mambo yalizungumzwa bungeni. Aliwajibika na amesema mwenyewe aliwajibika."

"Alijiuzuru uwaziri mkuu kwa sababu ya Richmond. Tulimweka katika orodha ya mafisadi kwa sababu ya Richmond. Na jana alisema alimwambia rais "tuvunje mkataba" rais akaataa. Angefanyeje?. hilo ni vumbi, litakapo tulia Chama Cha Mapinduzi na mfumo tawala utakuwa umeanguka, tutajenga nchini.Bila kuvunja mfumo tawala hakuna kusonga mbele," ameeleza Lissu.
 
Hajamaliza bado, and then what does he say/ his opinion?
 
Hajamaliza bado, and then what does he say/ his opinion?

"Collective responsibility" ndicho kilichompata Lowassa. Kwa kile kipindi asingeweza kusema maneno ya jana kuwa Bosi wake alitoa go ahead. Yalikuwepo mambo mawili raisi ajiuzulu uitishwe uchaguzi mpya au waziri mkuu ajiuzulu kuilinda serikali isianguke. Cha muhimu hapa kwa sasa ni kuindoa CCM madarakani.
 
"Alijiuzuru uwaziri mkuu kwa sababu ya Richmond. Tulimweka katika orodha ya mafisadi kwa sababu ya Richmond. Na jana alisema alimwambia rais "tuvunje mkataba" rais akaataa. Angefanyeje?. hilo ni vumbi, litakapo tulia Chama Cha Mapinduzi na mfumo tawala utakuwa umeanguka, tutajenga nchini.Bila kuvunja mfumo tawala hakuna kusonga mbele," ameeleza Lissu.
angekuwa na nia ya dhati angeyasema haya mapema.. tafuteni sababu nyingine...

mie nawatakia kila lakheri kwenye safari yenu ya matumaini... nitakuwa sehemu ya mabadiliko kwa namna nyingine.. sio kila kitu nishabikie maana tumeembiwa wengine nikinani wakati maprof madr wabunge ,kamati kuu wanajua zaidi wameshakubali wengine ni kinani kupinga huu uamuzi muhimu ni kukaa kando kutizama mchezo tu..wenye chama washaa amua...
 
Eti anasema nini fisadi kaingia sasa wameongeza mafisadi.
 
angekuwa na nia ya dhati angeyasema haya mapema.. tafuteni sababu nyingine...

mie nawatakia kila lakheri kwenye safari yenu ya matumaini... nitakuwa sehemu ya mabadiliko kwa namna nyingine.. sio kila kitu nishabikie maana tumeembiwa wengine nikinani wakati maprof madr wabunge ,kamati kuu wanajua zaidi wameshakubali wengine ni kinani kupinga huu uamuzi muhimu ni kukaa kando kutizama mchezo tu..wenye chama washaa amua...

Hawata kwenda kokote
 
Back
Top Bottom