Lissu: Wanaotaka kuondoka CHADEMA ruksa

Lissu: Wanaotaka kuondoka CHADEMA ruksa

Gracias-Asante Sana Bwana Lisu!
Merce'- Asante Sante;
Danke-Asante,
Thank You-Asante;
Shukrani:Asante.
Umeondoa Utando Uliokuwa umetandwa Juu Ya Watanzania Wengi,Eti Umekacha Chama;
Mh,Asante,Mungu Yu Nanyi Daima,
Peplesssssssss!
 
Hapa kaz tu, lumumba wanahaha kupandikiza chuki. Hatupasuki ng'o.
 
TUNDU-LISSU-SEP-06-620x307.jpg



MBUNGE wa Singida Mashariki na Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Tundu Lissu, amesema chama chao kinatarajia kupata wanachama wengi baada Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa kujiunga na chama hicho.

Lissu ametoa kauli hiyo baada ya kuwepo taarifa kwamba wapo wanachama wa Chadema ambao watakihama chama hicho kutokana na kutokubaliana na ujio wa Lowassa ndani ya Chadema.

Akizungumza leo na waandishi wa habari Lissu amesema, “Kama wapo watakao jiondoa Chadema, wengi zaidi watakuja. Tupo katika kipindi ambacho hatujawahi kuwepo tangu mfumo wa vyama vingi uanze.

Mfumo tawala unabomoka vipande vipande. Unapo bomoka, dalili zake ni watu ambao wamekuwa katika mfumo huo kuondoka kama alivyofanya Lowassa.”

“Mabadiliko katika nchi yanatokea pale mfumo tawala unapo pasuka. Lowassa ni mfano mzuri.

Tunamkaribisha kwetu sio kwa sababu ni mwanasiasa msafi. Tumempokea kwa sababu tunaongeza nguvu kubwa kwa wale wanaotaka mabadiliko. Imetokea Zambia Mawawi, Nigeria na Kenya,” amesema Lissu.

Akizungumza kuhusu Chadema kumtuhumu Lowassa kwamba “ni fisadi” kabla ya kujiunga na chama hicho Lissu amesema, “…hatukuwa na makosa hata kido kumweka Lowassa katika kundi la watuhumiwa wa Richmond. Mambo yalizungumzwa bungeni. Aliwajibika na amesema mwenyewe aliwajibika.”

“Alijiuzuru uwaziri mkuu kwa sababu ya Richmond. Tulimweka katika orodha ya mafisadi kwa sababu ya Richmond. Na jana alisema alimwambia rais “tuvunje mkataba” rais akaataa. Angefanyeje?. hilo ni vumbi, litakapo tulia Chama Cha Mapinduzi na mfumo tawala utakuwa umeanguka, tutajenga nchini.Bila kuvunja mfumo tawala hakuna kusonga mbele,” ameeleza Lissu.

Mwanaccm yeyote inatakiwa wamweshimu Lowassa kwani ameteseka kwa miaka kumi. Kama angeyasema haya anayoyasema Leo sidhani kama hao akina nape na wengine wangekuwepo ccm. Kikwete asingekuwa madarakani inamana uchaguzi ungefanyika. Lakini alivumilia kwa kuilinda serikali na chama chake ccm. Ni wachache sana ambao watamwelewa lkn Kikwete mwenyewe anajua na ipo siku tutasimuliwa haya. Lowassa anayo haki ya kuhama chama mwacheni. CCM wafanye siasa za kistarabu ili hata kama wanarudi madarakani warudi kwa haki. Na kama Upinzani wanachukua madaraka wachukue kwa haki kwani wote ni Watanzania na Tanzania ni yetu sote
 
Mwanaccm yeyote inatakiwa wamweshimu Lowassa kwani ameteseka kwa miaka kumi. Kama angeyasema haya anayoyasema Leo sidhani kama hao akina nape na wengine wangekuwepo ccm. Kikwete asingekuwa madarakani inamana uchaguzi ungefanyika. Lakini alivumilia kwa kuilinda serikali na chama chake ccm. Ni wachache sana ambao watamwelewa lkn Kikwete mwenyewe anajua na ipo siku tutasimuliwa haya. Lowassa anayo haki ya kuhama chama mwacheni. CCM wafanye siasa za kistarabu ili hata kama wanarudi madarakani warudi kwa haki. Na kama Upinzani wanachukua madaraka wachukue kwa haki kwani wote ni Watanzania na Tanzania ni yetu sote

Lakini ikumbukwe kwenye halmashauri kuu lowasa alimuuliza Kikwete"Ni nini usichojua kuhusu richmond?" Nasikia mzee Mkapa akaingilia na mkutano ukaendelea na mengine.
 
Time for another political party to take
Over as its been More than 35 yrs of CCM and no positive progress. Viwanda vya kurithi kutoka kwa mzungu vimefungwa, mashule gamekwisha....kila siku ni Escrow, mara Richmond mara NBC mwisho mtasema mlima kilimanjaro umeuzwa....tumechoka na CCM...wabunge wakuteuliwa kila siku na mawaziri kibao time for change....Chadema is the only way
 
Gazeti la RAIA mwema RFA wamesoma asubuhi hii kuwa ameandika barua ya kuachia ngazi za vyeo vyote Kwa sababu hajaridhika na kumpokea lowasa bila masharti yoyote.Tusubiri tuone
 
huu ni mwaka wa mabadiliko cwezi fanya mabaliko nikiwa mzee ! mm kama kijana nitapiga kula kuondo wingu/ giza la maendelea (CCM) tuko pamoja kamandaaaa
 
Kwa hiyo kusema tu aliambiwa na mamlaka ya juu tusivunje ndiyo inafuta tuhuma za ufisadi wake hadi Lissu na Chadema nzima kumuona anafaa kuwa sehemu ya wapinga ufisadi???
 
Nilifahamu mapema Tundu Lissu misimamo yake kwamba siyorahisi kukihama chama.Hila kwa sababu ya propaganda za watu ndio maana amethibitisha
 
Mkuu hapa cha msingi ni kwa vipi ccm watazileta hizo documents fake..maana watakuwa wanajivua nguo wenyewe na kutembea uchi..kwa nn hawakumpeleka mahakamani? Suala hapa ni credibility ya maccm kwa wananchi..kipi watakachoongea wananchi watakiamini wakati wao wenyewe ni mafisadi wa kutupwa na wamethibitisha hivyo toka 2008 alipojiuzulu EL..ufisadi umeongezeka mara dufu..ni mjinga tu atakayewaamili hata wakija na mlima wa madocuments..haitasaidia..its too late I guess! Jiandikisheni wananchi..tuwatoe wajinga hawa!

Je mtakuwa na moyo tena kusimama bungeni kupinga ufisadi ilahli rais wenu Ukawa (lowassa) ana tuhuma za ufisadi?? Ni sawa Lowasa hakwenda mahakamani juu ya kadhia ile lakini hili neno ''tuhuma'' ukawa haliwakeri? Nimeshuhudia viongozi kadhaa katika taasisi ya nchi zinazoendelea wanaachia ngazi na kuacha kushughulikia siasa kwa tuhuma tu au kwa namna moja taasisi yake imekutwa na ufisadi., je hili kwenu si tatizo?

kwamfano ata Rais wa FIFA juzi ametangaza kuachia ngazi ingawa yeye hajakutwa na hatia na tayari umeshaitishwa uchaguzi mpya wa Raisa wa FIFA, mnalichukuliaje jambo hili kuelekea uongozi bora na suala zima la uwajibikaji?

Kwan itakuwaje kama Lowassa angekuwa mbunge wa Chadema na Ukawa halafu akashiriki kikamilifu katika kampenzi za Ukawa kuelekea uchaguzi mkuu October mwaka huu?? Dr Slaa ama Lipumba wakaendelea mmoja kati yao kuwa mgombea urais wenu??
 
Kuna baadhi ya watu wanafikiri walizaliwa ili watutawale tu..
 
Back
Top Bottom