Lissu vs Tume -Both Decisions Will Add More Credits to Him

Ha ha ha ha, hao ndio walisema wanakwenda ICC 2015, but where did it end!? Mkuu. Narudia wanachopaswa kufanya wakataji ni kuhakikisha ACT, CUF, NCCR na Mzes Rungwe they are in! Baada ya hapo sisi Watanzania tunamwachia kila mtu ale na wakwao!

Uko sahihi kabisa kwamba watanzania watakaa kimya. Ila madhara yake yatakuwa makubwa sana huko tuendako. Itatokea siku akaingia madarakani mtu mbaya kisha akafanya atakavyo na akagoma kutoka madarakani. Ukishakuwa na nchi isiyoheshimu sheria, bali matakwa ya walioko madarakani, ni lazima nchi hiyo itaingia machafukoni. Iwapo Lisu atakatwa kama matamanio ya wanaccm wengi yalivyo, wapiga kura watakuwa wachache sana, hiyo itazaa serikali iliyo kisheria, lakini isiyo na uhalali wa umma. Wanajeshi watakapoanza kuona raia wanaweza kukaa madarakani bila njia ya kura, tegemea na wao watajiongeza. Ama mtandao wa watu wachafu wanaweza kununua madaraka na kuendesha nchi kimafia bila ridhaa ya umma.

Furahia mambo ya kipuuzi leo, kisa Magufuli hawezi siasa za ushindani, bila kujua itajengeka precedence mbaya. Kuna kundi la wanamtandao lilijijenga kiutani utani hivi hivi, likawa na nguvu na liliweza kupata nguvu, kama sio kitisho cha cdm na Dr. Slaa leo hii tungekuwa chini ya kundi hatari. Sasa hivi mchezo unaanza kujirudia kwa Magufuli, kunaanza kujengeka utaratibu wa kuwa na kiongozi anayetawala kwa hisia zake bila kufanyika uchaguzi halisi, huku kundi la wapambe wanaofaidi wakiona ni sawa kiongozi kutawala kwa utashi wake, bila kujua tunatengeneza saratani moja mbaya kabisa. Muda ni mwalimu mzuri wa huu ushabiki wako.
 
Ha ha ha yeye mwenyewe anaita kimbunga. Anaita tsunami. Sasa wakuacha kwa kawaida kimbunga hua hakitabilili. Kinaweza kikavuma mpk kikawashinda.... Ha ha ha kwa muda mfupi tu huyu jamaa kaja kabadilisha upepo wa kisiasa kabisa nchini. Na upande wa kijani wamekua kimya wakifanya mambo ya kimya na kuzichanga karata zao kimya na kwa utulivu. Maana ata vijana mitandaoni hawaonekani kurusha makombora sn. Juu ukimya una kitu. Lkn safari Hii kz ipo.... Kikubwa tuombee amani tu
Mkuu tukiacha ushabiki na kujipa imani hakuna namna Lissu anaweza kumshinda Mwamba wa Chato.
 
Hakuna wakati mgumu wanapitia watumishi wa tume kama huu. Tangu kuanza kwa mfumo wa vyama vingi haijawahi kupata mgombea machachari kama TL.

Mgombea anayewakemea waziwazi tena kabla hawajafanya maamuzi ya mwisho ya kupitisha wagombea wa urais. Mgombea anayejua sheria vizuri tena huenda kuliko baadhi ya wanatume wenyewe.

Lakini kubwa zaidi linalowapa uchovu ni maamuzi ya mwisho ya ama apite ama wamkate. Sababu maamuzi yote mawili yana same score kwa TL, ambayo ni kumuongezea credits zaidi kwake.

Sasa ndio mtajua nyakati huwa hazina ngao. Zikifika zimefika huwezi kuzizuia. TL ni kama maji, usipoyaoga lazima utayafulia, usipoyapikia lazima utayanywa.

Zikifikaga nyakati kama hizi ndipo huwa uzalendo unatakiwa uwekwe mbele zaidi. Kama upo kwenye nafasi ya kufanya maamuzi usiangalie maslahi ya kiumbe yeyote hata awe ndugu yako bali maslahi ya taifa kwanza.

Tukutane August 26 kujua tume wataamua kumpeleka TL upande upi.
Ndio shida ya nchi yenye rais dictator..

They use the same formula...

Weaken all institutions,wewe tu ndio uwe na madaraka yote....

Anaegombea na wewe,hakikisha jina haliendi kwenye sanduku....

Dictatorship is a curse na Africa tumelogwa na hii takataka
 
Alikatwa Lowassa na maisha yakaendelea, akafanya Jecha yake na Maisha yakaendelea, Who is Lissu Buda?. Kitu pekee ambacho wakataji wanapaswa kuwa na uhakika ni Kama Membe, Zitto, Maalim, Lipumba, Sipunda na Mbatia wataendelea kushiriki uchaguzi baada ya jamaa kukwanguliwa, watakuwa wamemaliza kazi. Watanzania sisi tunajijua, kwetu sisi Mchuma Janga hula na wakwao!
Pengine hujui siasa kwa kiwango zaidi ya ushabiki na kupiga kura. Kwa taarifa ya wasomaji, kuna jambo (kete) moja ambalo halijawahi kutokea katika siasa za uchaguzi za Tanzania.

Tofauti na enzi za siasa za akina Mrema na Lowasa, ambao ni mazao ya CCM, Tundu ni zao la Upinzani perse. Augustine Mrema hakuwa na guts za kupeleka wafuasi wake barabarani. Aidha, Lowasa aliwasihi sana vijana wasiende barabarani licha ya kuamini kuwa kura zake ziliibiwa kupitia hacking, mradi ulioongozwa na Shamte pamoja na January Makamba.

Vijana, Kwa amri ya Mbowe walisitisha shinikizo na kisha kuacha kabisa mpango wao wa kuingia barabarani.

Kama kuna asiyejua, tishio la vijana kuingia barabarani ndio sababu kuu ya Magufuli kupiga marufuku mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa. Matokeo ya vijana kuingia barabarani kila mtu anayajua. Magufuli alijua Kwa uhakika kuwa aliingia Ikulu Kwa kura za kuiba. Waligushi kupitia hacking. Maandamano yangemuondoa ila haikuwa hivyo kwa sababu waliyekusudia kumsaidia kudai haki yake (Lowasa) alikuwa amegoma, hakuwa tayari kudai haki hiyo kupitia maandamano yasiyokoma.

Hiyo ndio kete ya Lissu. Anaungwa mkono. Ana uwezo wa kuamuru vijana waingie barabarani iwapo ataona na wafuasi wake wataamini kuwa ameonewa.

Sisi na wao hakuna asiyejua mwisho wa siasa za barabarani. Watu kadhaa watakufa, lakini kutawaondolea raia hofu ya kupambana na waovu wa Dola. Utawala wa CCM hautasalia madarakani.

Tumekwishakujifunza kutoka Mali, Sudan, Madagascar na kwingineko, Afrika na duniani.
 
Pengine hujui siasa kwa kiwango zaidi ya ushabiki na kupiga kura. Kwa taarifa ya wasomaji, kuna jambo (kete) moja ambalo halijawahi kutokea katika siasa za uchaguzi za Tanzania.

Tofauti na enzi za siasa za akina Mrema na Lowasa, ambao ni mazao ya CCM, Tundu ni zao la Upinzani perse. Augustine Mrema hakuwa na guts za kupeleka wafuasi wake barabarani. Aidha, Lowasa aliwasihi sana vijana wasiende barabarani licha ya kuamini kuwa kura zake ziliibiwa kupitia hacking, mradi ulioongozwa na Shamte pamoja na January Makamba.

Vijana, Kwa amri ya Mbowe walisitisha shinikizo na kisha kuacha kabisa mpango wao wa kuingia barabarani.

Kama kuna asiyejua, tishio la vijana kuingia barabarani ndio sababu kuu ya Magufuli kupiga marufuku mikutano ya vyama vya siasa. Matokeo ya vijana kuingia barabarani kila mtu anatajua. Magufuli alijua Kwa uhakika kuwa aliingia Ikulu Kwa kura za kuiba. Waligushi kupitia hacking. Maandamano yangemuondoa Ila haikuwa hivyo Kwa sababu waliyekusudia kudai haki take (Lowasa) alikuwa amegoma kudai haki hiyo kupitia maandamano yasiyokoma.

Hiyo ndio kete ya Lissu. Anaungwa mkono. Ana uwezo wa kuamuru vijana waingie barabarani iwapo ataona na wafuasi wake wataamini kuwa ameonewa.

Sisi na wao hakuna asiyejua mwisho wa siasa za barabarani. Watu kadhaa watakufa, lakini kutawaondolea raia hofu ya kupambana na waovu wa Dola.

Tumekwishakujifunza kutoka Mali, Sudan, Madagascar na kwingineko, Afrika na duniani.
Eti unajua siasa halafu unaleta habari za kusimuliwa hapa. Hivi unajua mwaka 2010 mlisema Dr.Slaa alimshinda Kikwete, halafu 2015 Dr.Slaa akiwa ametoka kumshinda Rais aliyekuwa madarakani( kwa mjibu wenu) na akiwa ameongezeka umarufu na CDM ikiwa imeimarika zaidi na CCM ikiwa imegawanyika na wamempitisha mtu asiye Maarufu mkamtosa mtu aliyemshinda Rais aliyeko Madarakani mwaka 2010 mkachukua mtu aliye kuwa na siku mbili chamani na mtu mliyemtukuna miaka mingi. Narudia hizo ni habari za vijiweni jifunze kutumia kichwa chako kuchanganua mambo Buda!
 
Mgombea anayewakemea waziwazi tena kabla hawajafanya maamuzi ya mwisho ya kupitisha wagombea wa urais. Mgombea anayejua sheria vizuri tena huenda kuliko baadhi ya wanatume wenyewe.

Hiyo kauli imenikera sn

Mkuu Tundu Lissu anajua sheria kuliko hata mwanasheria mkuu wa serikali sio baadhi ya wanatume
Itabidi aombe radhi kwa kweli, hata mimi nadhani level za lisu hapa bongo ni akina mtemi chenge na mkono maana hao nasikia hawajambo sana kwenye hii fani

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Eti unajua siasa halafu unaleta habari za kusimuliwa hapa. Hivi unajua mwaka 2010 mlisema Dr.Slaa alimshinda Kikwete, halafu 2015 Dr.Slaa akiwa ametoka kumshinda Rais aliyekuwa madarakani( kwa mjibu wenu) na akiwa ameongezeka umarufu na CDM ikiwa imeimarika zaidi na CCM ikiwa imegawanyika na wamempitisha mtu asiye Maarufu mkamtosa mtu aliyemshinda Rais aliyeko Madarakani mwaka 2010 mkachukua mtu aliye kuwa na siku mbili chamani na mtu mliyemtukuna miaka mingi. Narudia hizo ni habari za vijiweni jifunze kutumia kichwa chako kuchanganua mambo Buda!
Pengine unadhani kila anayendika humu anashabikia siasa za chakula. La hasha. Hebu soma nilichoandika with substantive clues na wewe rudia hearsay yako uome tunatofautiana wapi. Wewe unakijua kikosi cha Shamte kulikuwa na assignment gani wakati wa uchaguzi mkuu 2015?
 
Alikatwa Lowassa na maisha yakaendelea, akafanya Jecha yake na Maisha yakaendelea, Who is Lissu Buda?. Kitu pekee ambacho wakataji wanapaswa kuwa na uhakika ni Kama Membe, Zitto, Maalim, Lipumba, Sipunda na Mbatia wataendelea kushiriki uchaguzi baada ya jamaa kukwanguliwa, watakuwa wamemaliza kazi. Watanzania sisi tunajijua, kwetu sisi Mchuma Janga hula na wakwao!
Unatafuta mtelemko eeh
 
Hakuna wakati mgumu wanapitia watumishi wa tume kama huu. Tangu kuanza kwa mfumo wa vyama vingi haijawahi kupata mgombea machachari kama Tundu Lissu.

Mgombea anayewakemea waziwazi tena kabla hawajafanya maamuzi ya mwisho ya kupitisha wagombea wa urais. Mgombea anayejua sheria vizuri tena huenda kuliko baadhi ya wanatume wenyewe.

Lakini kubwa zaidi linalowapa uchovu ni maamuzi ya mwisho ya ama apite ama wamkate. Sababu maamuzi yote mawili yana same score kwa Tundu Lissu, ambayo ni kumuongezea credits zaidi kwake.

Sasa ndio mtajua nyakati huwa hazina ngao. Zikifika zimefika huwezi kuzizuia. Tundu Lissu ni kama maji, usipoyaoga lazima utayafulia, usipoyapikia lazima utayanywa.

Zikifikaga nyakati kama hizi ndipo huwa uzalendo unatakiwa uwekwe mbele zaidi. Kama upo kwenye nafasi ya kufanya maamuzi usiangalie maslahi ya kiumbe yeyote hata awe ndugu yako bali maslahi ya taifa kwanza.

Tukutane August 26 kujua tume wataamua kumpeleka TL upande upi.
Atakatwa kawaida kabisa
Na Jana la kufanya
Hii nchi ni zaidi ya Lisu!
 
Mamvi alikatwa akiwa ndani ya chama chake. Hakukatwa na NEC. Sema mambo ya Jecha ndio yalikua balaa. Lkn tuache ushabiki kidogo wa kiitikadi. Unafikiri itakua ni rahisi tu kumkata huyu mgombea wa cdm? Huyu mgombea uelewa wake juu ya mambo ya sheria na kanuni na taratibu za uchaguzi anazifahamu vp hasa? Maana huyu mgombea sio mbugila mbugila km Mimi. Watakuja na sbbu gani hasa ya kumkata? Jana alitinga mahakama kuu kula kiapo na alitinga akiwa na Kibatala. Kibatala nafikiri unamuelewa ktk fani ya sheria. Sasa hivi vichwa viwili unavipa sbbu gani ya kumkata TL?
Lissu anakili sana kaisha wazidi akili ccm bado waatumia windo 5 kwenye vichwa vyao chadema wanatu windo 11 wapi na wapi mwaka huu lazima ccm wakalishwe chini hakuna option
 
Na kitu kimoja hao wanatambua kua misimamo ya TL ni mtu mwenye uelewa mkubwa na msema ukweli. Pia ni mtu asiekubali kushindwa. Na ni mtu wa kupambana kusimamia haki yake. Hii misimamo yake wanaifahamu vzr. Kwahiyo wanajua kabisa kz ipo
Jana uelewa wote zaidi ya kuwa mropokaji
Bro, Mambo ya nchi siyo mchezomchezo, Kama ungekuwa ni kitu rahisi Maalim Seif amekuwa Rais wa Zanzibar kitambo
 
CCM wana uhakika kabisa hawawezi kumshinda LISSU kwenye sanduku la kura licha ya wao kufanya siasa kwa miaka yote tangu 2016 ndio maana ya uwepo wa mipango na mihemuko miovu ya kutaka kumwengua. Hiyo ni hofu ya kushindwa.... na wanajua hawana ubavu wa ushindani wa kistaarabu na hivyo kuchagua Uharamia wa kisiasa ( political piracy).
 
Msijitoe ufahamu, Lissu ni Makamu Mwenyekiti wa chama chake. Wakati wowote na muda wowote ule hakuna sheria inayomzuia kuwasiliana na Wanachama wake kama ilivyo kwa polepole, mangula, bashiru na wengineo wanavyofanya. CCM acheni bange.
Wala sio bange wengi wao ni wajinga wengi Cdm ilishaliona hilo mapema sana
 
Alikatwa Lowassa na maisha yakaendelea, akafanya Jecha yake na Maisha yakaendelea, Who is Lissu Buda?. Kitu pekee ambacho wakataji wanapaswa kuwa na uhakika ni Kama Membe, Zitto, Maalim, Lipumba, Sipunda na Mbatia wataendelea kushiriki uchaguzi baada ya jamaa kukwanguliwa, watakuwa wamemaliza kazi. Watanzania sisi tunajijua, kwetu sisi Mchuma Janga hula na wakwao!
Hivi huwa unaamini kuwa Lowassa alishinda Urais?
 
Hakuna wakati mgumu wanapitia watumishi wa tume kama huu. Tangu kuanza kwa mfumo wa vyama vingi haijawahi kupata mgombea machachari kama Tundu Lissu.

Mgombea anayewakemea waziwazi tena kabla hawajafanya maamuzi ya mwisho ya kupitisha wagombea wa urais. Mgombea anayejua sheria vizuri tena huenda kuliko baadhi ya wanatume wenyewe.

Lakini kubwa zaidi linalowapa uchovu ni maamuzi ya mwisho ya ama apite ama wamkate. Sababu maamuzi yote mawili yana same score kwa Tundu Lissu, ambayo ni kumuongezea credits zaidi kwake.

Sasa ndio mtajua nyakati huwa hazina ngao. Zikifika zimefika huwezi kuzizuia. Tundu Lissu ni kama maji, usipoyaoga lazima utayafulia, usipoyapikia lazima utayanywa.

Zikifikaga nyakati kama hizi ndipo huwa uzalendo unatakiwa uwekwe mbele zaidi. Kama upo kwenye nafasi ya kufanya maamuzi usiangalie maslahi ya kiumbe yeyote hata awe ndugu yako bali maslahi ya taifa kwanza.

Tukutane August 26 kujua tume wataamua kumpeleka TL upande upi.
Mkuu hivyo ni vitisho tu, kama hakufuata sheria lazima akatwe tu.
 
Mkuu tukiacha ushabiki na kujipa imani hakuna namna Lissu anaweza kumshinda Mwamba wa Chato.
Nakubaliana na wewe 100pc. Hata Lisu anajua huu ukweli na pengine anafanya hayo anayofanya ili tume imkate apate umaarufu. Natamani tume imwache ili acharazwe uwanjani. Kwani pale terminal 3 si aliachwa na siku ikapita.
 
Uko sahihi kabisa kwamba watanzania watakaa kimya. Ila madhara yake yatakuwa makubwa sana huko tuendako. Itatokea siku akaingia madarakani mtu mbaya kisha akafanya atakavyo na akagoma kutoka madarakani. Ukishakuwa na nchi isiyoheshimu sheria, bali matakwa ya walioko madarakani, ni lazima nchi hiyo itaingia machafukoni. Iwapo Lisu atakatwa kama matamanio ya wanaccm wengi yalivyo, wapiga kura watakuwa wachache sana, hiyo itazaa serikali iliyo kisheria, lakini isiyo na uhalali wa umma. Wanajeshi watakapoanza kuona raia wanaweza kukaa madarakani bila njia ya kura, tegemea na wao watajiongeza. Ama mtandao wa watu wachafu wanaweza kununua madaraka na kuendesha nchi kimafia bila ridhaa ya umma.

Furahia mambo ya kipuuzi leo, kisa Magufuli hawezi siasa za ushindani, bila kujua itajengeka precedence mbaya. Kuna kundi la wanamtandao lilijijenga kiutani utani hivi hivi, likawa na nguvu na liliweza kupata nguvu, kama sio kitisho cha cdm na Dr. Slaa leo hii tungekuwa chini ya kundi hatari. Sasa hivi mchezo unaanza kujirudia kwa Magufuli, kunaanza kujengeka utaratibu wa kuwa na kiongozi anayetawala kwa hisia zake bila kufanyika uchaguzi halisi, huku kundi la wapambe wanaofaidi wakiona ni sawa kiongozi kutawala kwa utashi wake, bila kujua tunatengeneza saratani moja mbaya kabisa. Muda ni mwalimu mzuri wa huu ushabiki wako.
Uko sahihi
 
Back
Top Bottom