Lissu vs Tume -Both Decisions Will Add More Credits to Him

Kwenu wapendwa wa mtaa wa Lumumba,

Hakuna kitu kama hicho cha Tundu Lissu kuenguliwa, lazima agombee.

Mlisema hatakuja, kaja toka Belgium.

Mlisema msaliti hana mvuto wa kisiasa, imebainika siyo kweli.

Mlisema siku ya Sikukuu ya Nane Nane Ofisi ya Tume ya Uchaguzi Dodoma itakuwa imefungwa, Tundu Lissu alikuta ipo wazi.

Mlisema hati yake ya Kiapo haitasainiwa na Jaji wa Mahakama Kuu Dar es Salaam , jana fomu zake za kiapo zimesainiwa.

Mmepanga kumuita Kisutu tarehe 26 August 2020, Tundu Lissu hawezi kutokea kwa udhuru wa jambo muhimu ktk mchakato wa kuelekea uchaguzi 2020.

Mnasema tarehe 26 August 2020 hatatambuliwa kama mgombea rasmi wa Urais kupitia CHADEMA 2020, Tundu Lissu atatambuliwa na Tume ya Uchaguzi ya Taifa na ndiyo itakuwa siku ya kusitisha tuhuma zote za mahakamani mpaka baada ya uchaguzi tarehe 28 Oktoba kumalizika.

Wagombea wanaotambuliwa na Tume ya Uchaguzi 26 Agosti tuhuma za mashtaka yao yatasitishwa kwa kinga maalum ili sisi waTanzania tuweze kushiriki kumpigia kura maana tuhuma ya kesi siyo kigezo cha kumuondolea haki yake kuchaguliwa kwani tuhuma siyo ukweli mpaka pale tu atakapo hukumiwa ndiyo sifa inakosekana.
 
Ccm wakimkata Lissu itakuwa ina jizarau sana ,Mambo yote iliofanywa ndani ya miaka mitano ni mengi na makubwa sana Hakuna awamu iliofanya kazi kama awamu ya Tano sasa wanayumbishwa na Mberigiji inauma sana.
 
Hakuna wakati mgumu wanapitia watumishi wa tume kama huu. Tangu kuanza kwa mfumo wa vyama vingi haijawahi kupata mgombea machachari kama Tundu Lissu.

Mgombea anayewakemea waziwazi tena kabla hawajafanya maamuzi ya mwisho ya kupitisha wagombea wa urais. Mgombea anayejua sheria vizuri tena huenda kuliko baadhi ya wanatume wenyewe.

Lakini kubwa zaidi linalowapa uchovu ni maamuzi ya mwisho ya ama apite ama wamkate. Sababu maamuzi yote mawili yana same score kwa Tundu Lissu, ambayo ni kumuongezea credits zaidi kwake.

Sasa ndio mtajua nyakati huwa hazina ngao. Zikifika zimefika huwezi kuzizuia. Tundu Lissu ni kama maji, usipoyaoga lazima utayafulia, usipoyapikia lazima utayanywa.

Zikifikaga nyakati kama hizi ndipo huwa uzalendo unatakiwa uwekwe mbele zaidi. Kama upo kwenye nafasi ya kufanya maamuzi usiangalie maslahi ya kiumbe yeyote hata awe ndugu yako bali maslahi ya taifa kwanza.

Tukutane August 26 kujua tume wataamua kumpeleka TL upande upi.
Ninachojua, Watanzania watamchagua tena Ndugu John Pombe Joseph Magufuli kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 2020-2025!
 
Alikatwa Lowassa na maisha yakaendelea, akafanya Jecha yake na Maisha yakaendelea, Who is Lissu Buda?. Kitu pekee ambacho wakataji wanapaswa kuwa na uhakika ni Kama Membe, Zitto, Maalim, Lipumba, Sipunda na Mbatia wataendelea kushiriki uchaguzi baada ya jamaa kukwanguliwa, watakuwa wamemaliza kazi. Watanzania sisi tunajijua, kwetu sisi Mchuma Janga hula na wakwao!
Huu ni mziki mwingine mkuu,sio ule uliouzoea.
Amini usiamini,huyu Magu wako hali yake ni mbaya kuliko unvyofikiria.

Acha kuishi kwa mazoea,wananchi walisha choka na huu ujinga wa Jiwe
 
Hakuna wakati mgumu wanapitia watumishi wa tume kama huu. Tangu kuanza kwa mfumo wa vyama vingi haijawahi kupata mgombea machachari kama Tundu Lissu.

Mgombea anayewakemea waziwazi tena kabla hawajafanya maamuzi ya mwisho ya kupitisha wagombea wa urais. Mgombea anayejua sheria vizuri tena huenda kuliko baadhi ya wanatume wenyewe.

Lakini kubwa zaidi linalowapa uchovu ni maamuzi ya mwisho ya ama apite ama wamkate. Sababu maamuzi yote mawili yana same score kwa Tundu Lissu, ambayo ni kumuongezea credits zaidi kwake.

Sasa ndio mtajua nyakati huwa hazina ngao. Zikifika zimefika huwezi kuzizuia. Tundu Lissu ni kama maji, usipoyaoga lazima utayafulia, usipoyapikia lazima utayanywa.

Zikifikaga nyakati kama hizi ndipo huwa uzalendo unatakiwa uwekwe mbele zaidi. Kama upo kwenye nafasi ya kufanya maamuzi usiangalie maslahi ya kiumbe yeyote hata awe ndugu yako bali maslahi ya taifa kwanza.

Tukutane August 26 kujua tume wataamua kumpeleka TL upande upi.
TAL in 2020....tume ya NEC wasituzingue this 2020. Nitapiga kura kwa TAL kwa hasira sana.....nimemaliza chuo since 2015 hadi sasa future haileweki....wallah wallah sawa acha tuone
 
Back
Top Bottom