Lissu usimjibu Albert Msando, mimi Namjibu

Lissu usimjibu Albert Msando, mimi Namjibu

Po
leo katika vyombo vya habari, wakili wa kujitegemea na Diwani wa Kata ya Mabogini (cdm) ametoa kasoro za kisheria kwa Mwanasheria Mkuu wa cdm juu ya hukumu ya kitila mkumbo na zitto kabwe. Msando alisema katiba ya cdm inaeleza kuwa kiongozi yeyote hatachukuliwa hatua za kinidhamu kabla ya kupewa mashtaka kwa maandishi na mamlaka husika na kupewanafasi ya kujibu mashtaka hayo kwa maandishi, mwisho wa kunukuu.

napenda kumwambia Msando akasome katiba ya cdm vizuri hicho kifungu anachosema ni kwa viongozi yeyote wale wa kuchaguliwa, wa mabaraza, wenyeviti wastaafu, wawakilishi wa madiwani na wabunge ndio inawapaswa kufanya ivyo na sio wajumbe wa kuteuliwa kama wakina Kitila MKUMBO. kifungu ambacho kinawapa mamlaka ya kuwavua nyazifa ni hiki hapa.


7.7.16 Kazi za Kamati Kuu zitakuwa:-
(v) Kumwachisha ujumbe wa Kamati Kuu mjumbe mteule ambaye ataenda kinyume nakatiba, kanuni na maadili au kushindwa kukidhi matakwa ya kuteuliwa kwake.

Mkuu hapa kwenye (V), Tueleweshane vizuri, Kamati kuu in mamlaka ya kumvua uongozi mwanachama kwa KAMATI hi pekee au hata kwa kamati nyingine zote???

Binafsi mimi naona hiki kifungu ni kwa ajili ya Wajumbe wa kamati kuu tu!! Je kuhusu Wajumbe wa kamati nyingine CC pia inaweza kuwaachisa uongozi??

Fafanua vizuri ili twende kazi!!!



Mkuu Manyi,Michango yako humu inatudhalilisa watu wa Mbozi, acha kujitoa ufahamu.
 
hivyo wewe msando kwa akili zako unajua sheria kuliko lisu?
 
Hawa maCDM hata jina la diwani wake halijuwi anakurupuka na kujibu hoja ati Albert Kisando? Huyu ni Msando ex speaker pale UDSM!

Nyie vijana wa CDM mbona mbembwe nyingi sana lakini umakini mnakosa? Kukosea jina la mtu ni mbaya sana kisheria! We umesoma wapi? Kile chuo cha mapadri cha mwanza? Maana nao wanafunzi wao wanatupa shida sana hapa maofisini!

Next time proof read kazi yako before you post ndio uungwana! No hurry in academia!
sijui lb7 mnajua maana unashindwa hata kuandika mbwembwe.
 
samahani wana jf ni ALBERT MSANDO na si ALBERT KISANDO kwy Heading hapo juu.
katiba inasemaje kuhusu kiongozi km Zitto? na nukuu ya Bw. Msando haimo kabisa ktk katiba ya Chadema?
 
walichofanyiwa Zitto,Kitila, na Mwigamba ni kuvuliwa NYADHIFA ZAO ZOTE NDANI YA CHAMA!Kifungu kinazungumzia kuhusu kuachishwa Ujumbe wa Kamati kuu, na si Uongozi. Sasa Msando anaweza kuwa sahihi katika suala la kuvuliwa uongozi kama katiba ya chama inavyosema!tusishabikie tuu bila kuwa makini kuhusu sheria zinasemaje. huwezi ku-construe hicho kifungu kwa kutaka kimaanishe pia kuwafukuza/kuwavua uongozi ndani ya chama.Kifungu kipo wazi tuu kuwa ni Ujumbe wa Kamati kuu na si Uongozi!nashauri kuwa wewe unayemjibu Msando ukae chini ukisome hicho kifungu vizuri kwa mapana yake!Ukija hivyo mahakamani,ukanikuta mimi kama hakimu, nakupiga chini mapema ukasome sheria vizuri!
sasa kitila mkumbo ni kiongozi wa wapi?
 
Ndiyo maana nasema ilikudhihilisha kwamba yeye nibinadamu kama wengine na kwamba yeye ni moja ya wanachama

wengi ni budi kumfukuza 100% kuondoa kiburi chake na wale wanaomtuma. Bila hivyo heshima ya cdm

itashuka sana.
Kwa mabli nakubaliana na wewe mkuu maana choko choko hazitaisha iwapo atabaki chadema... kila siku atataka awe kwenye headlines za magazeti ... kama noma na iwe noma ... afukuzwe moja kwa moja na hao wafuasi wake wote ... mimi naamin approach waliyotumia akina mkumbo ya kuandaa waraka ule bado ni ya kisaliti na ki uwoga ... kama kweli wana hoja wameshindwa nini kuwasilisha chamani? hata kama wana hoja lakini wameonesha udhaifu wa hali ya juu wa kutofuata taratibu rasmi za chama ... i am utterly disappointed by them ... sharti la kusamehewa ni waombe msamaha hadharani kwa viongozi na wana chadema wote waliodhurika na kashi kashi hizi
 
Hawa maCDM hata jina la diwani wake halijuwi anakurupuka na kujibu hoja ati Albert Kisando? Huyu ni Msando ex speaker pale UDSM!

Nyie vijana wa CDM mbona mbembwe nyingi sana lakini umakini mnakosa? Kukosea jina la mtu ni mbaya sana kisheria! We umesoma wapi? Kile chuo cha mapadri cha mwanza? Maana nao wanafunzi wao wanatupa shida sana hapa maofisini!

Next time proof read kazi yako before you post ndio uungwana! No hurry in academia!

sasa mmeajiri watu wasio na sifa halafu unalalamika.........wafukuzeni ...kuna haja gani ya kulalamika hapa mpaka hapo wewe mwenyewe umekosa umakini.....
 
Hawa maCDM hata jina la diwani wake halijuwi anakurupuka na kujibu hoja ati Albert Kisando? Huyu ni Msando ex speaker pale UDSM!

Nyie vijana wa CDM mbona mbembwe nyingi sana lakini umakini mnakosa? Kukosea jina la mtu ni mbaya sana kisheria! We umesoma wapi? Kile chuo cha mapadri cha mwanza? Maana nao wanafunzi wao wanatupa shida sana hapa maofisini!

Next time proof read kazi yako before you post ndio uungwana! No hurry in academia!


Hapo kwenye red. Sheria inasemaje kuhusu kuanza kuandika jina la jiji na herufi ndogo,nakukosea neno.
Next time you also have to proof read before you post.
 
Pambaneni wenyewe ndio kukujenga chama Kama Slaa alivyowahi kunena! Tukaneni sasa naona kambi ya ZZk na Lissu!

Msije mkasema mumelogwa na CCM! Siye hatupo hapo tunachapa kazi sie!

Mtoto wa kiswahili utamjua tu, kazi ipi mnachapa?? Kuuwa Tembo??
 
tatizo la vijana wanye nia ya kugombea ubunge 2015 waliingia makubaliano na Zitto kuwa atawapa vifaa vya matangazo wako vijana 16 mmoja wao ni ALBERT MSONDO
 
Mwambie nayeye asikurupuke........ atakula kadi sasahivi.
 
(v) kumwachisha ujumbe wa kamati kuu mjumbe mteule ambaye ataenda kinyume nakatiba, kanuni na maadili au kushindwa kukidhi matakwa ya kuteuliwa kwake.

kifungu hicho kinasema kuwa kamati kuu ina uwezo wa kumvua mtu ujumbe wa kamati kuu na si kumvua uongozi mwingine.
 
Huyu Albert Msando anajipendekeza sana,alishamzungukazunguka LEMA mpaka nahisi hakuambulia UKIBARAKA,ameona kambi inayomfaa ni MASALIA

Namshauri aachane na maamuzi ya kamati kuu. Ndessa hebu muite huyo kijana haraka sana pale majengo oficin umwajibishe arudi arusha akamalizie starehe kwa magari aliyoachiwa na mawalla.
 
Ndio shida ya wanaotetea kila kitu katika mfumo: Kupindisha ukweli. Haya ngoja tukusaidie. Dk Kitila Mkumbo hakuwa mjumbe wa Kamati Kuu kwa kuteuliwa. Yeye alichaguliwa na Baraza Kuu katika kundi la wanaume bara, pamoja na Marehemu Shelembi na Profesa Baregu. Aliongoza kwa kura Profesa Baregu akafuatia Dk Mkumbo.

Wajumbe wa kuteuliwa na Mwenyekiti mpaka sasa hivi ni wanne tu: Chiku Abwao, Marando, Safari na Mbogolo. Mwenyekiti amebakisha wawili. Hao ndio pekee wanaoweza kuvuliwa ujumbe wao na KK.

Ni uungwana kukiri kosa kwamba Mwanasheria wetu Mkuu alichemsha kuwashauri wajumbe wa KK wawafukuze hawa wandugu. Ingekuwa busara kuwaruhusu wajiuzulu kama walivyoomba. Lakini kwa sababu chuki ilitawala wakafanya maamuzi kwa ubabe na jazba. Matokeo yake wamevunja Katiba. La pili alilosema Msando ni kwamba kwa mujibu wa katibu ya CHADEMA huwezi kumhukumu mtu bila (i) kumpa tuhuma zake kwa maandishi (ii) mtuhumiwa ajibu tuhuma kwa maandishi. Yote haya hayakufanyika kwa sababu maamuzi yalifanywa nje ya vikao na KK ilitumika tu kuhalalisha.

Hili wala sio Msando tu. Hata Marando alijaribu kushauri ndani ya KK lakini wapi bwana kwa sababu ndani ya CDM mwanasheria pekee anayeheshimika ni TL.

Hapa makao makuu hali si shwari. Baada ya mkutano wa akina ZZK jana mambo ni magumu. Wakurugenzi wapo baridi sana, hasa Mrema na Kigaila. Wengine wanacheka, wakisema kwamba tuliwaambia huyu TL msimwamini ataua chama. Haya mambo ndiyo hayo sijui huko mbele kuna nini...
 
Back
Top Bottom