Lissu usimjibu Albert Msando, mimi Namjibu

Lua

JF-Expert Member
May 19, 2011
704
305
leo katika vyombo vya habari, wakili wa kujitegemea na Diwani wa Kata ya Mabogini (cdm) ametoa kasoro za kisheria kwa Mwanasheria Mkuu wa cdm juu ya hukumu ya kitila mkumbo na zitto kabwe. Msando alisema katiba ya cdm inaeleza kuwa kiongozi yeyote hatachukuliwa hatua za kinidhamu kabla ya kupewa mashtaka kwa maandishi na mamlaka husika na kupewanafasi ya kujibu mashtaka hayo kwa maandishi, mwisho wa kunukuu.

napenda kumwambia Msando akasome katiba ya cdm vizuri hicho kifungu anachosema ni kwa viongozi yeyote wale wa kuchaguliwa, wa mabaraza, wenyeviti wastaafu, wawakilishi wa madiwani na wabunge ndio inawapaswa kufanya ivyo na sio wajumbe wa kuteuliwa kama wakina Kitila MKUMBO. kifungu ambacho kinawapa mamlaka ya kuwavua nyazifa ni hiki hapa.

7.7.16 Kazi za Kamati Kuu zitakuwa:-
(a) Kufanya utafiti wa wagombea na wa Uraisi na Mgombea Mwenza na kuwasilisharipoti zake kwa Baraza kuu kwa ajili ya mapendekezo yake kwa Mkutano Mkuu.

(b) Kuteua Wakurugenzi wa Idara Kuu za Chama Makao Makuu

(c) Kuteua Makatibu wa Wilaya na Mikoa

(d) Kuthibitisha uteuzi wa Sekretarieti za Wilaya.

(e) Kutoa mapendekezo kwa Baraza Kuu juu ya rufaa za uchaguzi na kinidhamu.

(f) Kuandaa na kutoa Mapendekezo kwa Baraza Kuu, Mikakati ya kuendesha shughuliza Chama kwa kila mwaka na kwa kipindi cha miaka mitano.

(g) Kuandaa na kutoa mapendekezo kwa baraza Kuu , Mikakati ya kupata mahitaji yaraslimali za kuendesha kampeni za wagombea wa Chama katika chaguzi za kiserikali.

(h) Kuandaa na kutoa mapendekezo kwa Baraza kuu ratiba na maelekezo ya uchaguzi wakichama.

(i) Kupitia na kutoa kwa Baraza Kuu mapendekezo ya haja ya kuzifanyia marekebishoau maboresho Kanuni za Chama ama Katiba ya Chama.

(j) Kujadili taarifa za Sekretarieti ya Kamati Kuu na kutoa maamuzi na maelekezo kwautekelezaji.

(k) Kusimamia utendaji kazi wa Sekretarieti ya Kamati Kuu

(l) Kufanya mapitio ya Sera za Chama na kutoa mapendekezo kwa Baraza Kuu kwakuzingatia matokeo ya Utafiti uliofanywa na Sekretarieti ya Kamati Kuu.

(m) Kusimamia utekelezaji wa maamuzi na maelekezo ya Baraza Kuu na MkutanoMkuu.

(n) Kuwa kiungo na kudumisha mahusiano mema kati ya Chama na vyama vingine vyasiasa nchini, Afrika Mashariki na nchi nyingine.

(o) Kuthibitisha ajira za watumishi wakuu wa Chama ngazi ya Taifa.

(p) Kuteua kamati au tume za kushughulikia masuala maalum ya kichama kwa mudamaalumu.

(q) Kuteua wakaguzi wa mahesabu ya Chama kwa kila mwaka

(r) Kuthibitisha uteuzi wa wagombea Uspika, Ubunge na Baraza la wawakilishi
Zanzibar

(s) Kuandaa agenda za Baraza Kuu na Mapendekezo ya agenda za Mkutano Mkuu.

(t) Kufanya uamuzi juu ya mpendekezo ya kufukuza Mwanachama.

(u) Kuandaa hoja za kupelekwa Bungeni na Wabunge wa Chama

(v) Kumwachisha ujumbe wa Kamati Kuu mjumbe mteule ambaye ataenda kinyume nakatiba, kanuni na maadili au kushindwa kukidhi matakwa ya kuteuliwa kwake.

(w) Kuratibu utendaji wa ofisi ndogo ya Makao Makuu Zanzibar.

(x) Kusimamia utendaji kazi wa Mabaraza ya Vijana, Wanawake na Wazee.

(y) Kuteua wajumbe maalum wawili kuingia Kamati ya Utendaji ya Jimbo/Wilaya.

kwa kuwa mkumbo ni mjumbe wa kuteuliwa anaangukia kwy kifungu hicho hapo juu (v).

nawasilisha:

Huyo wakili aache kuwaonea huruma wasaliti. Kuhurumia wasaliti ni sawa na kuishi na nyoka, black mamba, ndani ya nyumba yako. Au sawa na kumuacha mtu anayetoboa jahazi ambalo wote mnasafiria.

Sasa tuachane na mambo ya Zitto, turudi kwenye serious issue. MGAO WA UMEME umeanza kutufanya wengine maskini. Biashara zetu zimesimama na kipato kushuka. Jamani hii CCM haikubaliki, tushirikiane kuitokomeza. Miaka 50 ya uhuru bila umeme wa uhakika...
 
samahani wana jf ni ALBERT MSANDO na si ALBERT KISANDO kwy Heading hapo juu.
 
Huyo wakili aache kuwaonea huruma wasaliti. Kuhurumia wasaliti ni sawa na kuishi na nyoka, black mamba, ndani ya nyumba yako. Au sawa na kumuacha mtu anayetoboa jahazi ambalo wote mnasafiria.

Sasa tuachane na mambo ya Zitto, turudi kwenye serious issue. MGAO WA UMEME umeanza kutufanya wengine maskini. Biashara zetu zimesimama na kipato kushuka. Jamani hii CCM haikubaliki, tushirikiane kuitokomeza. Miaka 50 ya uhuru bila umeme wa uhakika...
Tatizo ni kudhani ujanjaujanja wao wa DARUSO unaweza kuwa na nafasi kwenye siasa za CDM.
 
nahisi alikuwa anataka authibitishie umma kuwa yeye ni mmoja ya mawakili kanjanja sawa na wale wachumi daraja la 1 kichwani zero knowledge.

naona dogo anampango wa kujipaka shombo ya taaluma yake feki "degree za chupi" za akina nchemba.

haoni hata aibu kutetea mashetani.

naona ana mapenzi ya kidaruso daruso.
cdm ni chama kubwa imetapakaa nchi nzima asithubutu kufananisha na jinsi alivyokuwa akiongoza daruso ya watu elfu nne na huyo chizi mwenzake.

naona utoto unamsumbua akikua attaacha.
79?!!! ni utoto tu kichwani hoja hakuna bali analeta mapenzi tu kwa mtarakiwa akiamini kuwa ni kifaa kumbe wenzake walishang'ong'a na kutupa jalalani.

kama nchi ina mawakili wa hivi kazi ipo bandugu!!!!!!!

mapenzi ya daruso peleka daruso hii ni cdm bwana......

zitto hasafishiki hata kwa jiki.......
 
(v) Kumwachisha ujumbe wa Kamati Kuu mjumbe mteule ambaye ataenda kinyume nakatiba, kanuni na maadili au kushindwa kukidhi matakwa ya kuteuliwa kwake.

kwa kuwa mkumbo ni mjumbe wa kuteuliwa anaangukia kwy kifungu hicho hapo juu (v).

Kitila naye hakukilia chabo kifungu hiki kabla ya kwenda kwenye press conference!!
 
Naona pumba tupu humu, sijui hata mtoa mada alikuwa anamaanisha nini?? Msendo ni wakili wa zitto, mtoa mada anamzungumiza kitila mkumbo
 
Huyo wakili aache kuwaonea huruma wasaliti. Kuhurumia wasaliti ni sawa na kuishi na nyoka, black mamba, ndani ya nyumba yako. Au sawa na kumuacha mtu anayetoboa jahazi ambalo wote mnasafiria.

Sasa tuachane na mambo ya Zitto, turudi kwenye serious issue. MGAO WA UMEME umeanza kutufanya wengine maskini. Biashara zetu zimesimama na kipato kushuka. Jamani hii CCM haikubaliki, tushirikiane kuitokomeza. Miaka 50 ya uhuru bila umeme wa uhakika...

Siasa bwana, mhhhhhhh!
 
Hawa maCDM hata jina la diwani wake halijuwi anakurupuka na kujibu hoja ati Albert Kisando? Huyu ni Msando ex speaker pale UDSM!

Nyie vijana wa CDM mbona mbembwe nyingi sana lakini umakini mnakosa? Kukosea jina la mtu ni mbaya sana kisheria! We umesoma wapi? Kile chuo cha mapadri cha mwanza? Maana nao wanafunzi wao wanatupa shida sana hapa maofisini!

Next time proof read kazi yako before you post ndio uungwana! No hurry in academia!
 
Naona pumba tupu humu, sijui hata mtoa mada alikuwa anamaanisha nini?? Msendo ni wakili wa zitto, mtoa mada anamzungumiza kitila mkumbo
Revo hapa hujaelewa nini? mtoa mada anamaanisha kwamba kutenguliwa kuwa wajumbe wa kamati kuu kumefuata taratibu za chama!!

Wote wawili wanaangukia kwenye kifungu cha Tano, Ujumbe wao wa Kamati Kuu ni wa Kuteuliwa, ni nini hakieleweki.
 
CDM mumelogwa na nani? Mbona mnapigana vijembe wenyewe? Kuna mtu waCCM hapo? Kuna masalia katika Hilo?

Mnajimaliza wenyewe yangu macho
 
Kitila naye hakukilia chabo kifungu hiki kabla ya kwenda kwenye press conference!!

Albert Msando na Zitto 'hawakukutana barabarani'. Ni wa siku nyingi hawa, na ingeshangaza kama asingemuunga 'swaiba' wake huu upuuzi.

Sasa hivi issue inakuwa ni mahesabu ya chama! Ama hawa wanaojiita 'wasomi' wanawaona watanzania ni mazuru au hawana kumbukumbu!
Mahesabu ya vyama ni zogo lililoibuka siku za hivi karibuni, lakini malalamiko kuhusu usaliti yapo tangu 2010 wakati wa uchaguzi mkuu.

Hivi kila mwanachema alimuunga mkono Dr Slaa wakati wa kampeni?
 
mkuu hujui kitu ndiyo maana unakimbilia kusema unayosema kama ungepata mda wa kujua hata chembe leo usingesema haya uliyosema.
 
Back
Top Bottom