Keynez
JF-Expert Member
- Feb 12, 2007
- 2,397
- 3,884
Mara kadhaa nimelinganisha mtanange wa uchaguzi wa mwaka huu na pambano la ngumi kati ya Muhammad Ali na George Foreman.
Leo hii nitagusia jambo ambalo nadhani wengi mtakuwa mmeligundua. Nalo ni hii tabia ya mgombea wa Urais wa CCM, John Magufuli kukataa kata kata kutaja jina la mpinzani wake mkuu, Bw. Tundu Lissu. Sikumbuki kama nimewahi kumsikia Magufuli akitaja jina la Lissu hata siku moja.
Najua kwenye medani za saikolojia, kutotaja jina la adui yako inaweza kuwa ni ishara ya kumdharau na kujaribu kuonyesha kuwa haumuwazii lakini inaweza kuwa ishara ya woga uliozidi kipimo.
Muhammad Ali, bondia maarufu kuwahi kutokea duniani aliwahi kubadilisha dini yake iliyopelekea kubadili na jina lake kutoka kuitwa Cassius Clay. Media na baadhi ya watu walisuasua kuanza kutumia jina lake jipya jambo ambalo kumbe lilikuwa linamkera sana Ali.
Siku moja akawa anapambana na bondia Ernie Terrell. Bondia huyu alikuwa anakataa kumuita Ali kwa jina lake jipya hata walipokutana katika TV Show kabla ya pambano. Ali akamwambia:
"My name is Muhammad Ali, and you will announce it right there in the centre of that ring after the fight, if you don't do it now,". Terrell bado akakataa!
Kilichofuata ni Ali kumchakaza Terrell kwa kipigo cha mbwa koko katika moja ya mapambano ya kihistoria yanayokumbukwa katika mchezo wa ngumi. Ali alikuwa anamchakaza mpinzani wake huku akimrushia maneno ya hasira na kejeli, “Jina langu Nani? What’s my Name?”.
Lissu amekuja katika uchaguzi huu kutoa changamoto ya karne katika medani za siasa. Anajua hilo, wapinzani wake wanajua hilo, na sisi tunajua hilo.
Kuna siku aje amuamuru hasimu wake mkuu, alitaje jina lake sasa au atakuja kulitaja akiwa katika mazingira yasiyo rafiki sana kwake. Itapendeza akimuuliza hilo swali September 07, 2020.