Bondia Larry Holmes: Ken Norton alinipiga ingawa majaji walinipa Ushindi

The Evil Genius

JF-Expert Member
Mar 21, 2014
5,464
17,301
Wale wapenzi wa ndondi, tunawakumbuka mabondia wa miaka ya 70 na 80 kina Mohamed Ali, Smoking Joe Frazier, Ken Norton, Jimmy Young, Leon Spinks, Big George Foreman, Ernie Shavers, Ron Lyle nk.

Mwaka 1978, Leo Spinks akiwa ameshinda taji ya WBC kutoka kwa Mohamed Ali, aligoma kupigana kama ratiba inavyotaka na Ken Norton badala yake akaamua kurudiana na Mohamed Ali.

Hiyo ikapelekea WBC kumnyang'anya taji ama mkanda wa WBC Leon Spinks na kumpatia Ken Norton. Ken Norton alikua mshindi namba 2 kwa rankings kwa wakati huo.

Kumbuka Ken Norton amewahi kupigana na Mohamed Ali akashinda pambano lao la kwanza na Mohamed Ali kushinda mashindano 2 kati ya 3 ingawa wachambuzi wa ngumi wanakiri kwamba hakuna pambano Mohamed Ali alimpiga Ken Norton ingawa alipewa ushindi. Ali amewahi kukiri baada ya pambano lao la 3 kwamba mshindi alikua Ken Norton kwenye pambalo lao ingawa yeye ndie alipewa ushindi na majaji, kwa maana kwamba alibebwa na majaji.

Baada ya miezi 3 Ken Norton alipaswa kulinda mkanda wake wa WBC dhidi ya Larry Holmes ambae hapo awali alikua mpambe(Sparring partner). Hawa ni wale wanakua na bondia wakati wa mazoezi wanakua wanapigana na bondia. Kila bondia ana Sparring partner wake wa kupigana nae wakati wa mazoezi na wanakua wameajiriwa na mabondia.

Mabondi wengi walianza kama Sparring partner wa mabondia wakubwa. Ken Norton alikua Sparring partner wa Joe Frazier.

Pambano lao la uzito wa juu kati ya Ken Norton na Larry Holmes lilipigwa Caesars Palace, Las Vegas, NV Ijumaa June 9 mwaka 1978.

Pambano lilikua la raundi 15,
holmes-norton-GettyImages-81398828.jpg
majaji wanasema walimpatia ushindi Larry Holmes kwa sababu alitumia roundi 2 za mwisho vizuri.

Baada ya Pambano Larry Holmes alitangazwa kama The New World Heavyweight champion. Larry Holmes alitumia miaka 7 mbele kutawala heavy weight division hadi mwaka 1985 ambapo alipoteza ubingwa kwa kupigwa na Michael Spinks.

Hivi karibuni Larry Holmes amkiri kwamba Ken Norton alimpiga mwaka 1978 ila ndio hivyo majaji walimpatia yeye taji ila Ken Norton alimdunda. Katika mapambo yake yote zaisi ya 60, Larry Holmes anakiri Pambano la Ken Norton ndio pambano lake gumu kuliko yote na hua akisikia jina la Ken Norton anakumbika kipigo cha mwaka 1978.


View: https://youtube.com/shorts/VCcZrHio1fc?si=AxFW5hPF5I4ttaXy
norton-holmes-poster.jpg
holmes-norton-GettyImages-181166470-770.jpg
holmes-norton-GettyImages-81340741.jpg
Holmes-Ken-Norton.jpg
 
Back
Top Bottom