Lissu: Makinikia yameshaondoka, Hatujalipwa kitu, Acacia bado wanasafirisha dhahabu, Bombardier siyo mpya, Dreamliner haina kibali cha kuruka nje

Further thoughts apropos makinikia na Bombardier za Magufuli:

Je, makinikia yaliyokuwa yamezuiliwa bandarini bado yapo??? Mimi nimeambiwa na a highly placed source kwamba yameachiliwa kimya kimya na kusafirishwa nje.

Kwa hiyo hatujalipwa shilingi trilioni 495 alizozisema Jiwe na professorial rubbish yake.

Hatujalipwa dola milioni 300 walizodai Wazungu wa makinikia wamekubali kulipa ex gratia.

Acacia Mining, tulioambiwa hawana hata leseni za uchimbaji, wanaendelea na uchimbaji Nyamongo wilayani Tarime, na wanasafirisha dhahabu yote nje ya Tanzania kama ilivyokuwa zamani.

Na Acacia Mining wameshafunga Mgodi wa Buzwagi baada ya kumaliza dhahabu yote, na wamesimamisha uzalishaji Bulyanhulu kusubiri uamuzi wa kesi ya arbitration, waliyoitolea notisi mara baada ya Magufuli kukamata makinikia.

Wahenga walisema 'wajinga ndio waliwao.' Tumeliwa!!!!

Kuhusu Bombardier za Magufuli:

Nimeambiwa kuwa mojawapo kati ya zile Bombardier mbili za mwanzo imeharibikia Mwanza kitambo sasa. Apparently, zote mbili hazikuwa mpya.

Na kati ya mbili zilizobaki, ile iliyokuwa imekamatwa Canada kwa sababu ya Magufuli kuvunja mkataba nayo ni mbovu. Ilikwenda Mwanza ikashindwa kurudi kwa sababu engine haikuwa na nguvu na kulikuwa na crack kwenye mojawapo ya rotor blades zake.

Naambiwa aliyekuwa Waziri wa Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa aliunda Tume ya wataalamu wa Wizara yake kuchunguza masuala haya.

Tume ilikabidhi Taarifa yake na, naambiwa, imethibitisha kuwa tuliuziwa ndege kuukuu. Taarifa hiyo imekaliwa mahali.

Kuhusu Dreamliner:

Bila shaka mnafahamu kwamba safari pekee iliyofanya nje ya Tanzania ni ile ya kutoka Seattle, Marekani, kuja Tanzania. Tangu ifike inafanya safari za Dar, KIA na Mwanza tu.

Sababu ni hii: Air Tanzania haina certificate ya Ukaguzi wa Usalama wa Uendeshaji wa shirika la ndege (IOSA - IATA Operational Safety Audit) inayotolewa na Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga (IATA) kwa kila shirika la ndege mwanachama.

Kwa taarifa nilizopewa, mainjinia wote waliopelekwa Marekani kwa ajili ya mafunzo ya kuendesha Dreamliner ile wamefeli mitihani yao mara mbili. Hawawezi kuruhusiwa kuirusha.

Kwa hiyo, hadi sasa, Dreamliner inaendeshwa bado na mainjinia wa Boeing Corporation walioileta Tanzania. Na hadi hapo ATCL itakapopata IOSA certification, haitaruka popote nje ya Tanzania.

Sio tu ATCL haikuwa na, na bado haina, business plan, inaelekea hakukuwa hata na maandalizi ya kuwa na shirika la ndege lenye kutimiza masharti ya kusafirisha abiria nje ya Tanzania.

Narudia tena: wajinga ndio waliwao!!!!!
Naomba kuuliza.. Wanaoendesha ndege ni mainjinia au marubani.. Natumaini nitapata jibu mapema
 
Unaweza kunikatalia lakini as a Learned member of the bar, Lissu angeweza kuprovide wise oppisition kuliko hiyo approach yake. Ukorofi, ubabe na matusi. Castro the learned Lawyer ali argue kortini akidai aliyetakiwa kizimbani ni Batista na si yeye, katika hotuba yake " La Historia Mel Absolvera". Hakunyongwa (Majaji walikuwa convinced na hoja zake). Hata hapo mahakamani alifika kwa kuwa tu kamanda wa kikosi kilichomkamata alizuia asipigwe risasi, akisema; "Mawazo mazuri hayauwawi". Mtusikue tunachosema wengine hatuna upande hapa.
Si unajua Castro aliingiaje madarakani, kwa hiyo unashauri Lissu naye atumie njia hiyohiyo?
 
Kuna mambo huwa nakubaliana na TL BT kuna mambo pia huwa sikubalian nae,
1.Anajifanya ana akili saaaana kuliko MTU yeyote probably hapa duniani(anaiita report ya makinikia kuwa 'professorial rubbish'). Kama mwana taaluma hii si saws.
2. Anakosoa tu bila kuonesha solution,kwa nn asiseme kama mwanasheria mahili ni nini altimate solution ya anachokosoa??
3. Awe mzalendo kama Zitto,unaweza kuwa unaichukia sana serikali iliyopo madarakani BT huwezi kuichukia NCHI yako. Kushangilia nchi yetu kuendelea kuibiwa au kupata hasara eti kisa tu huipendi serikali nadhani so saws.
4. Ajaribu ku-calm down kidogo,urais mtu hapewi na wapiga kura bali hupewa na 'SYSTEM'. Anaweza kupendwa saaaana na wapiga kura BT kama hajaishawishi system kwa uwezo wa kuwa a leader hawezi kupewa urais.
4. Issue ya kupigwa risasi asiifanye iaminike 100% kuwa ilifanywa na Magu as a person,kisiasa itamsaidia BT kwa system itamharibia zaidi. Hii issue ni complex sana na kuifanyia conclusion kirahisi nadhani si sawa,it might be an inside job too,only God and the assassin know this.
5. Chadema mmeshakuwa,watu wanawaamini na taasisi nyeti zimeanza kuwaamini....jiepusheni na gossips kama mlivyofanya kwa Eddo halafu baadae mkamsafisha. Siasa ni sayansi
Wewe hata akili yako haifiki chembe moja ya lissu. Na inawezekna lissu umemjua tu hiv karbuni.

Jibu hoja zako sio personal attach.

1. Kwan si kweli bokbadia inaozea uwanja wa ndege wa mza?

2..je tumelipwa pesa za makinikia?

3. Makinikia bado yapo bandarin?

4. Onyesha certificate inayoruhusu dreamliner kufanya safari za nje.
 
Mkuu umechangia kwa busara sana hadi nimefurahi. Pia umeanisha mambo fulani fulani. Kwamba urais haupewi na wananchi bali na system! Sasa huwa tunapiga kura za nini? Umesema suala la yeye kupigwa risasi asimtaje Magu as a person na kwamba atajiharibia kwa system. kwa hiyo unapaswa kunyenyekea system hata kama unafanyiwa unyama. Kwa maelezo yako system inabariki unyama. Sasa nimefahamu nini kinaendelea.
Nadhani kuna kitu hujaelewa vzr mkuu,'system' is almost everything! Ststem ndiyo inayo-harmonise masuala ya nchi na ni mhimu ujue pia kuwa nchi ina makundi mengi ya kijamii kama wakulima,wafanyakazi,wafanyabiashara,wasomi,majeshi etc etc so wanasiasa ni portion ya jamii. Mojawapo ya kazi za system ni kuhakikisha hakuna kundi moja linalokuwa over superior kuliko jengine kiasi cha kuhatarisha utengamano wa jamii. Hawa ndo huamua mwelekeo wa nchi! Na hata huyo jiwe usidhani aliokota embe dodo chini ya mwarobaini,alipewa urais kulingana na mahitaji ya wakati. Kufanya vzr au vibaya kwa kiongozi is just another case hasa baada ya kupewa nchi,ndo maana hata waliompa urais Trump wanafurahia anachokifanya(restoring America's superiority) bt WALIOMPIGIA KURA Trump wanaisoma namba!

Karibu tujadili......
 
Kuna mambo huwa nakubaliana na TL BT kuna mambo pia huwa sikubalian nae,
1.Anajifanya ana akili saaaana kuliko MTU yeyote probably hapa duniani(anaiita report ya makinikia kuwa 'professorial rubbish'). Kama mwana taaluma hii si saws.
2. Anakosoa tu bila kuonesha solution,kwa nn asiseme kama mwanasheria mahili ni nini altimate solution ya anachokosoa??
3. Awe mzalendo kama Zitto,unaweza kuwa unaichukia sana serikali iliyopo madarakani BT huwezi kuichukia NCHI yako. Kushangilia nchi yetu kuendelea kuibiwa au kupata hasara eti kisa tu huipendi serikali nadhani so saws.
4. Ajaribu ku-calm down kidogo,urais mtu hapewi na wapiga kura bali hupewa na 'SYSTEM'. Anaweza kupendwa saaaana na wapiga kura BT kama hajaishawishi system kwa uwezo wa kuwa a leader hawezi kupewa urais.
4. Issue ya kupigwa risasi asiifanye iaminike 100% kuwa ilifanywa na Magu as a person,kisiasa itamsaidia BT kwa system itamharibia zaidi. Hii issue ni complex sana na kuifanyia conclusion kirahisi nadhani si sawa,it might be an inside job too,only God and the assassin know this.
5. Chadema mmeshakuwa,watu wanawaamini na taasisi nyeti zimeanza kuwaamini....jiepusheni na gossips kama mlivyofanya kwa Eddo halafu baadae mkamsafisha. Siasa ni sayansi
Mkuu unaposema system unamanisha nini?
Je kama kama urais unapewa na system sisi wananchi tunapiga kura za nini?
 
Kwenye mambo ya kitaalamu muwe munaweka pembeni siasa zenu ili muzipeleke kwenye majukwaa.

Pengine Lissu kaambiwa kweli lakini kwa nini aweke kwenye jukwaa na GT bila kupata uhakika? Bora angeweka insta....
Kama aliye mtonya ni anti Magu so ndo siasa hizohizo?

Eti nimetonywa. Duh.


Nasubiri watalaamu watoe elimu sio siasa hizi.
Kwani makanikia yapo? Je tumelipwa?
 
Sasa jiwe ilikuaje anunue ndege kumbe hamna hata marubani kama sio kukurupuka huko??

ATCL kumbe hairuhusiwi kuruka anga za kimataifa sa dreamliner ya nn, si Jiwe alisema itakua inaruka kwenda marekani...sa mbona kaifanya daladala ya mwanza??

Hii nchi inaliwa sana. Pamoja kwamba ndege haimnufaishi mwananchi wa hali ya chini, kodi za wananchi zinatafunwa hovyo kabisa
Brother k
 
Kila kitu “nimeambiwa nimeambiwa..........”
unaaminije kuambiwa mtu professional kama wewe???
Akili za kuambiwa changanya na za kwako.
 
Lissu acha uongo.. Mainjinia ndio wanarusha ndege? Ndege inarushwa na Pilots na Pilots wengi wameshaenda Simulator course ya Dreamliner na wanaruka wazawa.. Kwnn unakuwa muongo hivi?

Kuhusu mainjinia (AME) wameenda type rating course na wamefaulu na wana rating endorsed in their AME licences..!! Kwnini Lissu muongo hivi? Na ni wazawa..!! Alafu sheria ya IATA kuhusu kuruka International flight ni kuwa na ndege zaidi ya moja ya kufanya safari za International flights.. Na sio eti tumekosa IOSA-IATA certificate.. So once tukipata ndege ya pili ya masafa marefu next year, IATA itatoa certificate ya kufanya International flights, so huo ni utaratibu wa kawaida kabisa.. Ila sio hizo sbb Lissu alizosema.. Lissu muongo sana sana.. Hivi vitu ni very scientific & technical sio kama political barking Lissu anayofanya..!!:mad::mad::oops: And no one ana ubavu wa kupinga mambo ya kisayansi haya sio siasa hii..!!:mad::oops:
Hebu tupe na jibu LA.kisayansi kuhusu Ku pack kwa bomberdier?.. Na ubovu wake?
 
Mmeamini kutegemea polisi ni ulemavu? Hapa kusipo na nguvu ya polisi kuwabeba mmeshindwa kujibu chochote zaidi ya kuwa vituko. Jengeni utaratibu wa kukabiliana na hoja kwani hata siku mkipoteza madaraka mtabaki.
Unajibu hoja ambayo inatolewa na mtu ambaye ni mentally sound!

Unaanzaje kumjibu mtu hana documents za ushahidi asemacho, kila kitu anasema NIMEAMBIWA.
 
Unadhan kwa nn yule dada wa USA alisema anarudi 1/8. Alishajua kaka ake atatoka mwezi 8 pili kuna kitu alitegemea kupata support sema mambo yamekuwa delayed.

Nchi ya Gining'iiii
 
Waalimu wanapanda daladala bure ?
Wale kahaba pale Kona bar wameisha ?
Wale bongo movies wamezuia movie za nje?
Wale waliotelekeza watoto wameishia wapi ?
Gesi ya Ntwara ipo bado ? Inazalisha umeme ?
Mil 50 Kila Kijiji
Tukimaliza kuondoa wafanyakazi hewa tunapandisha mishahara.
Oh sorry nadhani ntakuwa nimelewa.
Mimi nikikumbuka ile express boat ya bagamoyo nina imani ndege zetu ziko vizuri ni majungu tu ya chadema
 
Nafikiri kuna vitu mnamiss.Kuna umuhim gan kwa mtu ambaye mnamuona ni makini kumix ukweli na uongo tena hii sio et ni mattz ya kibinadam,Hizi ni siasa uchwara kwa kutafuta kiki za mambo ambayo hayapo.Siasa zenye nguvu ni siasa za kuongea ambayo vina evidence. Ukifuatilia huyu ndiye aliyetoa habari za kushtakiwa,habari za MIGA nk.So utaona amekua mropokaji.Na kitu mnachomis hakuna bavicha anaweza hoji jambo llt toka kwa mbowe,lisu,zito,lema nk.Kuna baadhi ya vitu sio lzm ccm waje kutoa majibu,hata mwenyewe unaweza fikiria ukaona hizi ni siasa tu
Boss natumai umeenda shule. Siegemei upande wowote, nimevutiwa tu na msimamo wako wa kuachana na habari ambayo umekuta ina taarifa hata moja ya uongo. Wakati upo shule ikitokea umepewa ripoti yako ya matokeo halafu somo moja ukawekewa 20% wakati unajua umepata 21% utatupa ripoti nzima au utaenda ofisi ya mwalimu kurekebisha Ile 20% iwe 21%.? Na je kuwekewa 20% badala ya 21% kunafuta ukweli wa maksi zako za Masomo mengine?
 
Kila kitu “nimeambiwa nimeambiwa..........”
unaaminije kuambiwa mtu professional kama wewe???
Akili za kuambiwa changanya na za kwako.

Hayo lieleze Jiwe maana lilitwambia limeambiwa acashia wapo nchini kinyume cha sheria, lilitwambia baricki wamekubali kulipa trilion zetu 424. Halafu kumbe vyote hola!!
Kwa hiyo kwako wewe jiwe likiambiwa hata kama ni fake news hiyo haina shida,Ila Lissu akiambiwa hata kama ni facts tupu hiyo kwako ni nongwa?
 
Lisu amelishwa kasa! Ukweli hujitenga na uongo.
ameozoea uongo wa vya kunyonga lakini vya kuchinja vimemdunga sindano ya nikotama...atakuwa amelaaniwa na wengi sana huyu jamaa..na laana hizi hazitamuacha bure..yeye aendelee tu kuwaingiza chaka wananachi kwa faida binafsi.
 
Kila kitu “nimeambiwa nimeambiwa..........”
unaaminije kuambiwa mtu professional kama wewe???
Akili za kuambiwa changanya na za kwako.
Si yupo nje ya nchi, wewe upo hapahapa hujui chochote
 
Back
Top Bottom