Lissu: Makinikia yameshaondoka, Hatujalipwa kitu, Acacia bado wanasafirisha dhahabu, Bombardier siyo mpya, Dreamliner haina kibali cha kuruka nje

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
21,271
47,271
Further thoughts apropos makinikia na Bombardier za Magufuli:

Je, makinikia yaliyokuwa yamezuiliwa bandarini bado yapo??? Mimi nimeambiwa na a highly placed source kwamba yameachiliwa kimya kimya na kusafirishwa nje.

Kwa hiyo hatujalipwa shilingi trilioni 495 alizozisema Jiwe na professorial rubbish yake.

Hatujalipwa dola milioni 300 walizodai Wazungu wa makinikia wamekubali kulipa ex gratia.

Acacia Mining, tulioambiwa hawana hata leseni za uchimbaji, wanaendelea na uchimbaji Nyamongo wilayani Tarime, na wanasafirisha dhahabu yote nje ya Tanzania kama ilivyokuwa zamani.

Na Acacia Mining wameshafunga Mgodi wa Buzwagi baada ya kumaliza dhahabu yote, na wamesimamisha uzalishaji Bulyanhulu kusubiri uamuzi wa kesi ya arbitration, waliyoitolea notisi mara baada ya Magufuli kukamata makinikia.

Wahenga walisema 'wajinga ndio waliwao.' Tumeliwa!!!!

Kuhusu Bombardier za Magufuli:

Nimeambiwa kuwa mojawapo kati ya zile Bombardier mbili za mwanzo imeharibikia Mwanza kitambo sasa. Apparently, zote mbili hazikuwa mpya.

Na kati ya mbili zilizobaki, ile iliyokuwa imekamatwa Canada kwa sababu ya Magufuli kuvunja mkataba nayo ni mbovu. Ilikwenda Mwanza ikashindwa kurudi kwa sababu engine haikuwa na nguvu na kulikuwa na crack kwenye mojawapo ya rotor blades zake.

Naambiwa aliyekuwa Waziri wa Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa aliunda Tume ya wataalamu wa Wizara yake kuchunguza masuala haya.

Tume ilikabidhi Taarifa yake na, naambiwa, imethibitisha kuwa tuliuziwa ndege kuukuu. Taarifa hiyo imekaliwa mahali.

Kuhusu Dreamliner:

Bila shaka mnafahamu kwamba safari pekee iliyofanya nje ya Tanzania ni ile ya kutoka Seattle, Marekani, kuja Tanzania. Tangu ifike inafanya safari za Dar, KIA na Mwanza tu.

Sababu ni hii: Air Tanzania haina certificate ya Ukaguzi wa Usalama wa Uendeshaji wa shirika la ndege (IOSA - IATA Operational Safety Audit) inayotolewa na Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga (IATA) kwa kila shirika la ndege mwanachama.

Kwa taarifa nilizopewa, mainjinia wote waliopelekwa Marekani kwa ajili ya mafunzo ya kuendesha Dreamliner ile wamefeli mitihani yao mara mbili. Hawawezi kuruhusiwa kuirusha.

Kwa hiyo, hadi sasa, Dreamliner inaendeshwa bado na mainjinia wa Boeing Corporation walioileta Tanzania. Na hadi hapo ATCL itakapopata IOSA certification, haitaruka popote nje ya Tanzania.

Sio tu ATCL haikuwa na, na bado haina, business plan, inaelekea hakukuwa hata na maandalizi ya kuwa na shirika la ndege lenye kutimiza masharti ya kusafirisha abiria nje ya Tanzania.

Narudia tena: wajinga ndio waliwao!!!!!
 
Lissu acha uongo.. Mainjinia ndio wanarusha ndege? Ndege inarushwa na Pilots na Pilots wengi wameshaenda Simulator course ya Dreamliner na wanaruka wazawa.. Kwnn unakuwa muongo hivi?

Kuhusu mainjinia (AME) wameenda type rating course na wamefaulu na wana rating endorsed in their AME licences..!! Kwnini Lissu muongo hivi? Na ni wazawa..!! Alafu sheria ya IATA kuhusu kuruka International flight ni kuwa na ndege zaidi ya moja ya kufanya safari za International flights.. Na sio eti tumekosa IOSA-IATA certificate.. So once tukipata ndege ya pili ya masafa marefu next year, IATA itatoa certificate ya kufanya International flights, so huo ni utaratibu wa kawaida kabisa.. Ila sio hizo sbb Lissu alizosema.. Lissu muongo sana sana.. Hivi vitu ni very scientific & technical sio kama political barking Lissu anayofanya..!!:mad::mad::oops: And no one ana ubavu wa kupinga mambo ya kisayansi haya sio siasa hii..!!:mad::oops:
Hapa Kazi Tu..!!:mad:
 
Lissu acha uongo.. Mainjinia ndio wanarusha ndege? Ndege inarushwa na Pilots na wemgi wameshaenda Simulator course ya Dreamliner na wanaruka wazawa.. Kwnn unakuwa muongo hivi?

Kuhusu mainjia (AME) wameenda type rating course na wamefaulu na wana rating endorsed in their AME licences..!! Kwnini Lissu muongo hivi? Na ni wazawa..!! Alafu sheria ya IATA kuhusu kuruka International flight ni kuwa na ndege zaidi ya moja ya kufanya safari za International flights.. Na sio eti tumekosa IOSA-IATA certificate.. So once tukipata ndege ya pili ya masafa marefu next year, IATA itatoa certificate ya kufanya International flights, so huo ni utaratibu wa kawaida kabisa.. Ila sio hizo sbb Lissu alizosema.. Lissu muongo sana sana.. Hivi vitu ni very technical sio kama political barking Lissu anayofanya..!!:mad::oops:
Umejibu vizuri tatizo Lisu ni parrot yaani domokaya chochote akisikia kiwe hearsay yeye lazima abweke kujionyesha yuko well informed nk Ni domokaya hasa huyo aliyempa taarifa hiyo ni Yule mwongo mwingine Zitto Kabwe .Lisu kazivalia kidedea Bila Ku confirm.Highest placed source kwake ni Zitto Kabwe
 
Back
Top Bottom