Waziri Makamba ujue siyo kila kitu ni cha kubinafisisha

Kinuju

JF-Expert Member
Mar 20, 2021
2,390
5,310
Waziri wa Nishati January Makamba ajulishwe kuwa kwenye taifa siyo kila kitu ni cha kubinafisishwa kwa masilahi mapana ya taifa.
  • Umeme
  • Bandari
  • Reli
  • Viwanja vya ndege
  • Mbuga etc
Baba wa taifa Mwl Nyerere kwenye hotuba yake moja mwaka 1995 alikemea vikali akili ya kuchukua mali ya uma na kuwakabidhi watu wachache, mfano umeme ndiyo injini ya uchumi wa nchi kwa kuvutia kujengwa kwa viwanda vingi na kuzalisha bidhaa za bei ndogo zitakazoshindana kwenye soko, kamwe hatuwezi kuwapa watu wachache watufanyie biashara kwa kutuuzia umeme alafu tukategemea bidhaa zetu zishindane kwenye soko la Dunia.

Enzi za Kikwete Tanesco nusura ibinafisishwe baada ya kuwa na madeni makubwa ya kulipia capacity charges kutoka kwenye generator za kampuni la symbion.

Alipoingia Magufuli akafuta baadhi ya mikataba ya hovyo na kuliwezesha shirika kukusanya zaidi ya trillion 2 kwa mwaka hivyo likaacha kujiendesha kwa kutegemea ruzuku ya serikali na kufuta mpango wa kulibinafisisha shirika hili la uma.

Ameingia rais Samia na alipomteua waziri January Makamba tayari ameingia na mentality ileile ya enzi za Kikwete.

1. Pamoja na kwamba Tanesco ya leo hawaagizi nguzo nje ya nchi kama walivyokuwaga wanafanya huko nyuma lakini bado Makamba anataka shirika libinafisishwe.

2. Pamoja na kwamba Tanesco ya leo wanakusanya zaidi ya trillion mbili kwa mwaka lakini bado waziri Makamba anataka shirika libinafisishwe!

3. Pamoja na kwamba kupitia REA Tanesco imetapakaa nchi nzima lakini bado waziri anataka shirika libinafisishwe.

4. Pamoja na kwamba sasa hivi Tanzania inajenga bwawa kubwa kabisa la kufua umeme lakini bado waziri anataka Tanesco ibinafisishwe.

Hii speed ya 4G ya Makamba kutaka Tanesco ibinafisishwe inasukumwa na nini? Hivi kwa akili hii vipi huyu Makamba angeshinda urais mwaka 2015?
 
Kwani kunanini? Mbona nyuzi ximekuwa nyingi kwa Tanesco?
20211013_124528.jpg
 
Unabinafisaji uendeshaji maana mswahili hawezi akaendesha kitu kwa ufanisi na ishu ya security inabakia kwenye serikali kwa national security.
Check tu mfano Tazara wameshindwa japo market ni kubwa na ya uhakika.
 
Huyu bwana nashauri ATENGULIWE kwa maslahi makubwa ya taifa! Kwenye uongoz wa magu scandal zote za masuala ya umeme zilikata, lkn mama alivoingia mambo hayakuwa haba ila tatz linaanza kuonekana mapema baada ya huyu January kuingia. Pamoja na mentally yake ya ubinafsishaji lkn bado umeme umekuwa tatizo, umeme unakatika ovyo ovyo.

Haukai ukadumu ata lisaa haujakatika. SHENZI KABISA, huu umeme tunauhangaikia cc mbwa wewe. Bado tunaulipia plus makato kibao. Sasa mwambieni kama vipi aanze kumbinafsisha mke wake aone madhara yake. Mijitu mingine haina akili bc tu ina majina makubwa. Kudadeq😬😬😬
 
Waziri wa Nishati January Makamba ajulishwe kuwa kwenye taifa siyo kila kitu ni cha kubinafisishwa kwa masilahi mapana ya taifa.
Umeme
Bandari
Reli
Viwanja vya ndege
Mbuga etc
Ukiona hivyo ujue yuko nyuma ya pazia.kishatengeneza kikampuni ya kuwanyonya watz.kijana bado mdogo lkn fikra zake ni za hovyo kabisa utadhani si mtanzania.kwa kuwa yy hana uchungu na nchi hii na kwa kuwa ktk maisha hajala joto la jiwe ndo maana hata akili yake inawaza mambo ya ajabu ajabu na sijui hiyo nafasi alipewa kwa kigezo gani.
 
Nashangaa watu kupiga kelele juu ya Tanesko wakati tunasahau migodi mikubwa ya dhahabu na almasi karibu yote inamilikiwa na wageni.

Hapa tukianza kwenye matokeo ni kupoteza muda tunatakiwa tupaze sauti kwenye chanzo (Katiba) na sio huku kwenye vitu vidogo.

Binafsi natamani ata shule zote za Kata zibinafsishwe, ili kila mtu ajue kuwa ni kwanini katiba mpya inahitajika.

Kila jambo nchi hii no kwahisani ya viongozi na sio matakwa ya wananchi sababu tumeamua kuwa mashabiki wa vyama vya siasa au mtu flani.

Sasa hivi mwananchi hana pahali pa kupazia sauti yake. Tunasubiri wachache watuamulie kila kitu
 
Back
Top Bottom