Lissu is too shallow compared to Prof Kabudi

Lissu is too shallow compared to Prof Kabudi

Lissu ni mropokaji na mpiga kelele tu hajui lolote kinacho mbeba ni kwamba wananchi wanahamu kubwa ya mabadiliko ya kiuchumi na kiutawala.
Rekodi zipo Kisutu...kaulize pale.

By the way, WANAUME watatoa Noah zetu au ndio watabadili matumizi kama zilivyobadilishwa 50m za kila kijiji?
 
Hakuna wa kukudharau kwa kusema ukweli. Tena ukweli wenye ushahidi. Kwa Lissu, makinikia ilikuwa mali ya wawekezaji. Kwa Kabudi ilikuwa mali yetu. Hitimisho la mchakato na wawekezaji walinyosha mikono kwa Kabudi. Anayedharau atoe hoja.

Sent from my SM-G532F using JamiiForums mobile app
 
Aliyetoa hii mada ametumwa but anachoongea kabudi ni kuitetea serekali kisaikolojia na ukizingatia yeye ndio mwanasheria mkuu wa serekali kama angekuwa mwanasheria kweli anaefata taaluma yake angekuwa mtu mzuri ila pale kwa lissu atasubiri sana pia kibatala ni mwanasheria nguli sana yani tuseme vyama vyote vya upinzani haswa Chadema ina wanasheria wanaojielewa sana
 
naona dalili ya mtu kushiba, ama kulewa, ila acha niwaambie washibaji na walevi; mtasubiri sana jamaa hana elimu ya kiwango kikubwa ila elimu yake tu hiyo wakalale wenye maudokta na mauporofesa yao, jamaa kafanya makubwa, jamaa kawasiadia wengi, ukitaka ujue itisha sensa ya waliosaidiwa, ukiona mtu mwenye elimu ndogo analinganishwa uelewa wa mambo na mtu mwenye PhD+ tunuku ujue jibu ni MWENYE ELIMU NDOGO NI MWELEWA ZAIDI NA ANAFANYA YA MAANA kuliko linganisho lake, pole
 
100% Lisu hawezi mfikia Prof. Prof ni next level kwa sababu prof can cheat Lisu cant! Prof anaweza akatumika Lisu can't, prof anayakataa maneno aliyoyatamka kwa kichwa chake Lisu can't, prof anapinga hata kile anachokiamini Lisu can't !
 
Hivi kama tungelipwa makinikia huyo prof siungesema next level kwa Mungu? Kipimo chake ni ushirriki wake kwenye vikao vya siri na matokeo ya kuondoshwa makinikia kwa siri na kusubiri kulipwa kwa siri.
 
Mara nyingi Kabudi ni mtu anyefanya presentation kwa mihemko na kujiona kuwa hakuna mtu wa level yake na mwisho ndo anajikuta anachanganya files.
Naamini kabudi anafaa zaidi kukaa darasani na kufundisha na sio kuiapply sheria ktk maisha hilisi kwani unaweza kujua kitu na ukashindwa kukiapply.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama kikwete alimkubali lissu wewe ni nani umpinge acheni ujinga fungueni akili

Lissu sio saizi ya hao maprofesorial rubbish
 
Hajui hata katiba ya CHADEMA chama chake sembuse sheria ya nchi? Unapigwa risasi kwa mizengwe unashindwa kuyasoma mazingira?? Risasi inapigwa kulia unaumia kushoto? Then unajiita mwanasheria nguli hujui hata kuchambua mambo??
mmhh ndio umejibu nini hapo mkuu! Au bado unaagiza machozi ya simba na umeshazidiwa?
 
Naanza kwa kukubali title yangu ndiyo, kabudi ni level nyingine kwa kina Lissu na mdee,

Najua nitapigiwa kelele baada ya uzi huu wengine watasema umetumwa, wengine watasema heshima yako inashuka no sina heshima hapa, nipo kuwasilisha mawazo yangu,

Kwa uwezo wa kabudi wa uwasilishaji wa mazungumzo na mijadala huwezi kumlinganisha Lissu hata siku moja,
Lissu uonekana anajua sheria kwa wasioelewa,

Kwa kifupi lissu hupiga kelele kwa kutaja vifungu n.a. watu wanashangilia bila kujua,

Kwa ufupi nimefuatilia hata baadhi ya hoja za kibatala nikaona Lissu uanasheria wake anacheza na jukwaa tu,
Hajafika hata level za kina Marando, au Advocate Mukono, ila kwakuwa hawana platform ya kuonekana watu hawagundui

Angalia presentation style ya kabudi na relevance ya anachokisema kutokana na sheria, mwangalie LIssu presentation na relevance ya anachoongea, kwa kifupi Lissu sheria yake haijafika level hizo mnapomuweka,

Akiacha kuongea kwa kupiga kelele akiwa ametulia atakuwa mwanasheria mzuri , bado Ana nafasi afanye mazoezi

Porojo tupu, nilijuwa unakuja na hoja za kisheria kumbe ni mdandia Treni
 
Back
Top Bottom