Lissu: Dr. Slaa ni Rais ajaye

Lissu: Dr. Slaa ni Rais ajaye

Hatufai ataifilisi hazina kwa kujikopesha kila siku, then ameshindwa kuidhibiti vhadema katika ubadhirifu ataiweza jamhuri ya muungano wa tanzanai.
Nasika rais wa awamu ya tatu aliiacha vizuri hazina, hebu tupe status ya sasa kukoje!?

 
kwa taarifa yako huyo ndio firstlady wako..... Unamuona alivyoshupavu na jasiri anakabiliana na hali halisi bila kujali umevaa gamba au gunia.. HEBU MPELEKE HAPO MAMA NANILIUU TUONE KAMA ATAWEZA HIYO KASHKASH YA POLICCM... si atajinye.....a

Kuiba bwana wa mtu na kumuachanisha na utumishi wa Mungu, Na kumzalia mtoto padri, kwa kweli huu ni ushujaa kabisa!
 
Uchaguzi mwaka huu lazima pachimbike wa tz tumefunguka coz ccm mmetudanganya kwa miaka mingi xana !!! Kwanza kwa kua na ukawa nidhahiri kwamba mabadiliko ni makubwa!!
 
Eti mnakuwa na mtu anaitwa slaa mbona nchi kila mtu atakuwa na slaa na kitakachofuata ni vita tu.
 
Hata kama palijengwa wakati wa chama kimoja lakini ungozi imara wa chama ndio waliohamasisha, sasa nyie mnashindwaje kuhamasisha wanachama wenu!? By the way TANU kabla ya kuzuiliwa vyama vingi ilikuwa na majengo yake zamani ambayo yalikujaboreshwa baada ya kuingia mfumo wa chama kimoja na baadaye tena kurudi vyama vingi. Mbona mmeshindwa kuwatumia watu wenu vizuri mnabaki kutokwa povu na tamaa ya kudhani mtamiliki mali za ccm! Haiwezekani.

Kaka muogope Mungu, hebu niambie kutokana na ukubwa wa ccm toka mfumo wa vyama vingi uingie nchini ni jengo gani kubwa la maana walilojenga? Halafu ukae chini ujiulize kwa dhamira yako ni vingapi vikubwa mlivyojimilikisha lakini vilijengwa kwa nguvu ya wananchi wote wakati chama kikiwa kimevaa koti la serekali? Suala hili halihitaji kujidanganya kwani wewe sasa umeshakuwa mtu mzima unajua wapi ni kweli na wapi ni uongo, sikatai ukweli unauma lakini ndio ukweli.

Kwa bahati mbaya sana ama nzuri cdm kipao mbele chao sio majengo bali ni kupanda elimu ya uraia kwa wananchi na kwa kiasi kikubwa hili wamelifanikisha na matokeo yake leo hii wewe unaweza kuja hapa jukwaani kukutana na watu wa pande tofauti tofauti mkichangia kutoa hoja. Ili nikupe tofauti kubwa ya nyinyi wenye majengo tena mliyojimilikisha kibabe na wale wasio na ofisi lakini wakato elimu ya uraia ni katika kujenga hoja. Ni nadra sana kuwakuta wanaccm wakijenga hoja zenye ushawishi hapa jukwaani kulinganisha na hao wasio na majengo/ofisi kwani hao cdm walichofanya ni kuwafundisha watu kuvua samaki wakati ccm nyinyi mmeamua kuchukua samaki lakini hamna uwezo wa kuvua.

Halafu kitu kingine ninachoweza kukuambia na hili ni dhahiri, ukitaka kujua hayo majengo mliyamiliki kibabe ni hali halisi ya hayo majengo mlipoyachukua na jinsi yalivyo sasa. Kwa kweli ni chakavu na hayana matengenezo yoyote ya maana bali yamegeuka ni sehemu ya watu kupigia majungu, wivu, kuendekeza ushirikina na upuuzi mwingine kama huo. Na kwa kiasi kikubwa yamegeuka kama sehemu ya kuua fikra za viongozi wengi wa chama chenu, kwani wamebaki kubweteka na kugeuze kama miradi yao ya kujikimu na familia zao. Na sehemu kubwa yanatumika kama sehemu ya kupanga siasa chafu kwani mnajua mkitoka madarakani tu yatarudishwa serekalini na ndio utakuwa mwisho wa ulaji. Rejea nimesema nyinyi hamjafundishwa kuvua samaki bali mlipewa samaki sasa mtaenda wapi?
 
Uchaguzi mwaka huu lazima pachimbike wa tz tumefunguka coz ccm mmetudanganya kwa miaka mingi xana !!! Kwanza kwa kua na ukawa nidhahiri kwamba mabadiliko ni makubwa!!

umeonaeee lazima pachimbike
 
Slaa ni kilema wa mkono na mguu hataweza kukabiliana na changamoto za nchi yetu

kwani wewe una uhakika wa kesho kuwa na viungo vyote salama? by the way tunachohitaji kwake ni ubongo wake ili utumike kwa maslahi ya watanzania..
 
kura yangu kwa dr.slaa ama lisu wakipitishwa kugombea urais. nje ya hapo ni kuharibu kura badala ya kuwapa mafisadi waendelee kubebana.
 
Kuna kila dalili kwamba Chadema na vyama washirika vina mpango wa kumsimamisha Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa kugombea urais Oktoba mwaka huu.

Dalili hizo zilijitokeza hadharani juzi kutokana na kauli ya Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu aliyoitoa katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Viwanja vya Majengo, Moshi akimtaja Dk Slaa kama ndiye rais ajaye huku akieleza uwezekano wa Ukawa kuchukua nchi.

Lissu alimtaja Dk Slaa na Mbunge wa Moshi Mjini, Philemon Ndesamburo kuwa ndiyo wabunge wa Chadema ambao hawajawahi kushindwa na CCM tangu mwaka 1995.

“Historia hiyo itasema mbunge mmoja kati yao (ambao hawajawahi kushindwa na CCM) ni Mzee Ndesamburo na historia hiyo itasema mbunge wa pili ambaye hajawahi kushindwa na CCM ni Dk Willibrod Slaa, rais wetu ajaye,” alisema Lissu.

Mjumbe huyo wa Kamati Kuu (CC) ya Chadema, alisema katika historia ya Taifa hili kuna uwezekano mkubwa wa Chadema na vyama washirika kuingia Ikulu baada ya Oktoba.

Vyama washirika ambavyo vinaunda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) vya Chadema, CUF, NCCR-Mageuzi na NLD, vimepanga kusimamisha mgombea mmoja katika ngazi zote za uchaguzi kuanzia urais hadi udiwani katika Uchaguzi Mkuu ujao.

Dk Slaa aligombea urais 2010 na kushika nafasi ya pili kwa kupata kura milioni 2.3 sawa na asilimia 26.34 nyuma ya Rais Jakaya Kikwete aliyeshinda kwa kura milioni 5.3 sawa na asilimia 61.17.

Hadi sasa Ukawa haijateua wagombea wake katika ngazi hizo ambazo ni urais, ubunge na udiwani ambao watachuana na wagombea wa vyama vingine.


Chanzo: Mwananchi
Nilisema huyu Jamaa mropokaji na kweli anazidi kuonyesha rangi zake. Inakuwaje UKAWA hawajafikia maamuzi tayari mtu anakuja na hoja kama hii sii kutaka kuleta ugonvi ndani ya UKAWA.. Ndio maana nikasema UKAWA are not for real ni wasanii tu kama wasanii wengine wa siasa.....
 
Hata kama palijengwa wakati wa chama kimoja lakini ungozi imara wa chama ndio waliohamasisha, sasa nyie mnashindwaje kuhamasisha wanachama wenu!? By the way TANU kabla ya kuzuiliwa vyama vingi ilikuwa na majengo yake zamani ambayo yalikujaboreshwa baada ya kuingia mfumo wa chama kimoja na baadaye tena kurudi vyama vingi. Mbona mmeshindwa kuwatumia watu wenu vizuri mnabaki kutokwa povu na tamaa ya kudhani mtamiliki mali za ccm! Haiwezekani.
Nafikiri hujui chama na serikali vilivyokuwa vinafanyakazi kabla ya vyama vingi,

CCM haijawahi kusimama peke yake bila msaada wa serikali tofauti na Chadema, CCM ilikuwa inajenga kwa mgongo wa serikali viwanja vya michezo inavyodai kumiliki siyo vyake ni sisi wananchi tuliokuwa tunalazimishwa kuvichangia,

Kama unasema majengo au viwanja vilijengwa kwa uongozi imara wa chama nipe mfano wa kiwanja kimoja tu kilichojengwa na CCM baada ya 1992, kama hakuna kwa hiyo unataka kutuambia uongozi imara wa CCM uliisha baada ya mfumo wa vyama vingi kuanza? mbona leo hawajengi.
 
Nilisema huyu Jamaa mropokaji na kweli anazidi kuonyesha rangi zake. Inakuwaje UKAWA hawajafikia maamuzi tayari mtu anakuja na hoja kama hii sii kutaka kuleta ugonvi ndani ya UKAWA.. Ndio maana nikasema UKAWA are not for real ni wasanii tu kama wasanii wengine wa siasa.....

mkuu kwni kutoa maoni ni kosa? nakuhakikishia Dr slaa atagombea urais wa muungano na maalim seif atagombea urais wa zanzibar.
 
Back
Top Bottom