Lissu amlima barua Shibuda

Lissu amlima barua Shibuda

SIKU chache baada ya Mbunge wa Maswa Magharibi, John Shibuda (CHADEMA) kupingana na msimamo wa chama hicho kwa kuunga mkono posho, Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Tundu Lissu, amesema chama hicho kiko tayari kwa lolote kuhusu mbunge huyo.Lissu aliyasema hayo ofisini kwake jana alipotakiwa kuzungumzia kuhusu hatima ya mbunge huyo.“Namwandikia barua leo kumtaka aeleze kwa nini msimamo wake ulikuwa kinyume cha wa kambi ya upinzani na kama yupo tutamkabidhi leo, baadaye tutalipeleka kwenye Kamati Kuu ya CHADEMA yenye nguvu ya maamuzi, ikiwamo kumfukuza uanachama.“Tuko tayari kwa lolote kuhusu Shibuda hata kwenda kwenye uchaguzi mdogo, kama anaona CHADEMA ni mbaya arudi alikotoka au kama ataona atageuka jiwe, atafute sehemu nyingine ya kwenda,” alisema Lissu.Alisema wao binafsi hawawezi kuchukua uamuzi wa kumfukuza Shibuda zaidi ya kutangaza kumtenga, bali wenye uamuzi huo ni kamati kuu ya chama.Alisema baada ya kuwasilisha utetezi wake kabla ya kumpeleka kwenye kamati kuu watakaa kwanza na kumjadili na kuchukua hatua dhidi yake, kwani suala hilo liko wazi.Kuhusu mabaya ambayo Shibuda anayaendeleza kuhusu CHADEMA, Lissu alimtaka ayaendeleze na kumponda kuwa hana kipya zaidi ya kuzungumza ‘matapishi.’ “Shibuda hana chochote kipya zaidi ya matapishi ya wale wa jana na juzi waliokuwa wakisema kuwa CHADEMA ni cha familia ya Mtei (Edwin) na mkewe Mbowe, ni cha Wachaga. Nje ya hayo sijui kama ana kipya,” alisema Lissu.Kwa mujibu wa Lissu, mbunge huyo aliingia kwenye chama hicho mwaka jana alipopata ubunge na kwamba hakuna anachokijua kuhusu chama hicho.Wakati akichangia hotuba ya makadirio ya matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu, wiki iliyopita, Shibuda alikigeuka chama chake (CHADEMA) kuhusu posho akitaka ziongezwe hadi kufika sh 500,000.Shibuda alikwenda mbali zaidi na kumtaka waziri mkuu kufanyia kazi haraka ongezeko hilo la posho, ambalo alilibatiza jina la ujira wa mwia.
No utani CDM moto.
 
JINAMIZI la kutaka Mbunge wa Jimbo la Maswa Magharibi mkoani Shinyanga, John Magale Shibuda (CHADEMA), afukuzwe uanachama ndani ya chama hicho limezidi kumwandama, safari hii wananchi wa Musoma mkoani Mara wakiutaka uongozi wa chama hicho kumtimua haraka. Wananchi hao wameonekana kukerwa na msimamo wa Shibuda kuunga mkono kuchukua posho, hivyo kusisitiza kuwa hawataki kumuona Musoma akiwa amekuja kwa kazi za CHADEMA. Katika hilo wananchi hao wa Musoma wamemtuma Mbunge wa Jimbo la Musoma Mjini mkoani Mara, Vincent Nyerere (CHADEMA), kupeleka suala hilo kwa uongozi wa chama hicho taifa. Shinikizo hilo la kutaka Shibuda afukuzwe na kunyang'anywa kadi ya uanachama ndani ya CHADEMA, lilitolewa juzi na wananchi wa Musoma, wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Mara Sekondari mjini Musoma, ambao uliitishwa na Mbunge Nyerere kwa ajili ya kuzungumzia utekelezaji wa maendeleo jimboni humo. Kauli za kumkataa Mbunge Shibuda zilianza kusikika mkutanoni hapo wakati Nyerere alipokuwa akizungumzia suala la ofisi yake ya mbunge kupewa sh milioni 34 mwaka huu kama mfuko wa jimbo, ambapo umati wa watu ulisikika ukisema: “Safi sana, ila tunakerwa na Shibuda, afukuzwe CHADEMA.” Baada ya kauli hiyo, Nyerere aliwauliza wananchi mkutanoni hapo kwamba: "Nani anataka Shibuda afukuzwe ndani ya CHADEMA? Anyoshe mkono.” Kisha karibu umati mzima uliofurika mkutanoni hapo kunyoosha mikono juu huku wakipaza sauti juu kutaka aondoke Shibuda, wakidai “afukuzwe, huyo anatamaa, hatumtaki.” Mbali na hayo, wananchi hao pia walimuomba mbunge wao huyo kupeleka wito kwa wabunge wa CCM wanaotetea posho bungeni, ambapo Nyerere naye aliahidi kuufikisha ujumbe huo kama ulivyo. “Ndugu zanguni, wengi wape. Hili suala nitalifikisha kama mlivyonituma kwa uongozi wa CHADEMA taifa...na Jumatatu naenda bungeni Dododma nitafikisha sauti yenu ya umma,” alisema mbunge huyo wa Musoma Mjini. Akizungumzia mgogoro wa madawati katika Manispaa ya Musoma na aliyekuwa mbunge wa zamani wa jimbo hilo, Vedastus Mathayo (CCM), Nyerere alimtaka Mathayo kukimbia haraka mahakamani kwenda kuwashitaki madiwani anaowatuhumu kuchukua madawati hayo, vinginevyo watamburuza yeye (Mathayo), mahakamani. Hata hivyo, alisisitiza ujenzi wa maabara moja kubwa na ya kisasa katika shule za sekondari tano zilizopo ukanda mmoja wa Bweri mjini Musoma, na kwamba tayari utekelezaji wa miradi mbali mbali ukiwemo ujenzi wa barabara jimboni humo umeshaanza ndani ya kipindi kifupi cha uongozi wake, tofauti na ilivyokuwa uongozi wa CCM. Wakati huo huo, Mchungaji Jacob Mwita Chacha aliyegombea ubunge wa Jimbo la Tarime mkoani Mara katika uchaguzi mkuu mwaka jana kupitia Chama cha UDP, ameamua kujiunga na CHADEMA baada ya chama chake kukosa nguvu ya kutosha wilayani Tarime. Mwanachama huyo mpya alikabidhiwa kadi yenye namba 0191229 mbele ya viongozi wa chama hicho ofisini hapo jana asubuhi alipoamua kwa hiari yake kujiunga na chama hicho, kwa madai kuwa alivutiwa na utendaji wa dhati wa chama hicho kutetea wananchi. Katika vikao vyake vya Bunge wabunge na madiwani wake katika halmashauri mbali mbali nchini kwa ajili ya maslahi ya wananchi na taifa kwa kwa ujumla.
Mtanzania daima.
 
dah hii kitu wasiifanye ki papara namna hiyo wakae kwanza kwenye vikao vyao wasuluhishe au wamuonye kwanza wasianze kufukuzana itaharibu credibility ya chama.
 
Nyie pigeni kelele tu, lakini Shibuda analindwa na ibara ya 100 ya katiba ya Tanzania, hongera Shibuda
 
dah hii kitu wasiifanye ki papara namna hiyo wakae kwanza kwenye vikao vyao wasuluhishe au wamuonye kwanza wasianze kufukuzana itaharibu credibility ya chama.

Vipi mkuu, unaogopa kuchukua maamuzi magumu? Wacha Shibuda ahukumiwe na umma ...
 
Shibuda bado ni mchanga sana kwenye chama. Matatizo ya kutoelewana na wenzake lazima yatajitokeza tu! Cdm wnatakiwa wawe wavumilivu na kuzidi kuelimishana ili wafike wanapoenda. Wakianza kufukuzana na kutimuana, wataanza kugawanyika vipande vipande na mwisho chama kitasambaratika!
 
Nyie pigeni kelele tu, lakini Shibuda analindwa na ibara ya 100 ya katiba ya Tanzania, hongera Shibuda
Mkuu una uhakika gani kuwa hicho kipengere kitamlinda? Je unafahamu katiba ya CDM inasemaje kuhusu mtu kukiuka katiba ya chama?
 
Waangalie sana!kunaweza kukibomoa chama kwa upande mwingine.Shibuda ana wafuasi ndani ya chama.
 
Shibuda ukifukuzwa CHADEMA,hamia NCCR ukachukue jimbo maswa.
 
watu wa musoma ndio walimchagua? wakisema wananchi wa maswa atleast inaweza kuwa na mashiko.
 
Waangalie sana!kunaweza kukibomoa chama kwa upande mwingine.Shibuda ana wafuasi ndani ya chama.
Kama shibuda anawafuasi wanaounga mkono hoja zake basi waondoke wote maana hawajengi chama cha upinzani bali wanajenga chama ambacho ktakuwa ni mke mdogo wa magamba ambacho si msimamo wa chadema.
 
Wapendwa jana niliweka thread hii kuhusu mustakabali wa Shibuda ndani ya Chadema kuhusu utovu wake wa nidhani kwenda kinyume na maazimio ya chama chake.
Kama mmesikia leo Marin Hassan wakati akiohojiana na aliyekuwa katibu wa Bunge, George Mlawa, ameweka wazi kuwa Shibuda anaweza kabisa kulindwa na Katiba ibara ya 100 inayomkinga Mbunge na KUCHUKULIWA HATUA YA KISHERIA/UWAJIBIKAJI KWA lolote atakalolitamka Bungeni. Amekwenda mbali na kutoa mfano wa Jidawi aliyekuwa CUF alivyokipeleka chama High court na kushinda kufukuzwa kwake.
Narudia tena Busara kubwa itumike ku-handle issue hii.
FIKIRI CHUKUA HATUA
 
Hii sheria inamlinda mbunge awapo bungeni, i mean kama mbunge, lakin mbunge huyu afukuzwapo na chama chake basi hana chake tena, Anapoteza sifa ya ubunge na hata hiyo sheria haitoi ulinzi tena!
 
Back
Top Bottom