Lissu amlima barua Shibuda

Lissu amlima barua Shibuda

Suala hapa sio kwamba chadema inamfukuza Ubunge bali inamvua uanachama. Kwa hiyo hilo bunge litaamua kama wanaweza kumwachia aendelee kuwa mbunge hali si mwanachama wa chama chochote hiyo nikazi kwao, na hapo watakuwa wamehalalisha mgombea binafsi.
Jamani haya mambo ni ya kisheria. Mahakama zina busara sana kama hakuna rushwa. Unamfukuza uanachama in order to defeat parliamentary immunity!!!!!!!!!!!!! wakati kosa limeoriginate kutokana na kauli yake bungeni ambayo ina immunity. Think twice,
 
Ninamashaka na mleta mada na mada yenyewe!

Nitakuwa wa mwisho kuiamini na kuitolea maoni habari hii!
 
Ninyi mpo nchi gani? hata kama mko ulaya hamsomi mitandaoni habari za bongo? eeh! mnatia aibu kwanza yaelekea hamfahamu mahali anapofanyia shopping huyu Shibuda, sasa njoo hapa posta mpya barabara inayokwenda IFM oppsite na Embassy Hotel kuna duka la Imalaseco, njoo uongee naye Shibuda mwenyewe sasa hivi au toka hapo nyumbani kwenu nenda kibanda cha magazeti kaitafute hii habari uisome kwa undani we vipi bhana? unataka utafuniwe kila kitu halafu umeze tu, duuh! hapa tunapeana suna tu mkuu, mi nimekuchomolea tu hii kutoka chumba cha uhariri wa hili gazeti la harakati za mageuzi bongo, nipo hapa nachapa kazi, au nikupatie namba ya Shibuda mwenyewe, ila wabongo noma utaanza kumdisturb, just assure me utakuwa mvumilivu hata msimamo wake ukiwa tofauti na wako nikuunganishe naye sasa hivi mkuu!

Mkuu wangu una matatizo ya kufikiri
Hivi wewe shibuda yuko mfukoni mwako au vipi?
Sasa sie tutaingiaje mfukoni.
 
Ninyi mpo nchi gani? hata kama mko ulaya hamsomi mitandaoni habari za bongo? eeh! mnatia aibu kwanza yaelekea hamfahamu mahali anapofanyia shopping huyu Shibuda, sasa njoo hapa posta mpya barabara inayokwenda IFM oppsite na Embassy Hotel kuna duka la Imalaseco, njoo uongee naye Shibuda mwenyewe sasa hivi au toka hapo nyumbani kwenu nenda kibanda cha magazeti kaitafute hii habari uisome kwa undani we vipi bhana? unataka utafuniwe kila kitu halafu umeze tu, duuh! hapa tunapeana suna tu mkuu, mi nimekuchomolea tu hii kutoka chumba cha uhariri wa hili gazeti la harakati za mageuzi bongo, nipo hapa nachapa kazi, au nikupatie namba ya Shibuda mwenyewe, ila wabongo noma utaanza kumdisturb, just assure me utakuwa mvumilivu hata msimamo wake ukiwa tofauti na wako nikuunganishe naye sasa hivi mkuu!

ingekuwa rahisi sana kutaja source kuliko kuandika upupu wote huu.
 
Mimi nadhani yapo mambo mengi tena mabaya zaidi aliyosema Shibuda nje ya bunge, alipofanya mahojiano na gazeti la Mtanzania na ambayo nadhani wanaweza kuyatumia.
Kuna watu wanataka kuwapotosha CHADEMA katika shauri hilo, nina imani Shibuda anastahili adhabu na wanachopaswa CDM ni kumkusanyia ushahidi usiotia mashaka. Ibara ya 100 ya katiba haiwezi kumkinga na makosa yake iwapo mashtaka yataandaliwa vizuri.
 
km ni hbr ya kutunga, basi aliyeitunga kampatia shibuda, hayo maneno yanafanana kabisa na shibuda, sishangai hata kidogo.
 
Na KATIBA ya CHADEMA inasemaje kuhusu kumfukuza mtu uanachama?
Mkuu niko mbali na maktaba yangu, tusaidiane kuitafuta. Hata hivyo hiyo Ibara ya 100 ya Katiba haiwezi kutumiwa kama kichaka cha kujificha Shibuda provided ushahidi unakusanywa vizuri.
 
11.jpg
Tulipojitolea kuionya CHADEMA tukaambiwa tukome lakini ukijaribu kupima nasaha zetu za wakati ule ni kama vile tulikuwa tunatoa unabii juu ya madhara ya CHADEMA kusomba makapi kutoka CCM, sasa nani asiyejua kuwa Shibuda anatumiwa na CCM? Sasa yametimia kwani kwa kinywa chake mwenyewe Shibuda amerudia kauli zake mbili zenye utata, kwanza kasema kuhama msikiti sio kuacha uislamu na pili kawaambia wana CCM wenzake kuwa kule CHADEMA yuko uhamishoni hivyo wasihofu atarudi nyumbani tu!
Naomba source mkuu,..maana niseje tolewa nishai ktk vijiwe vyangu vya draft
 
km ni hbr ya kutunga, basi aliyeitunga kampatia shibuda, hayo maneno yanafanana kabisa na shibuda, sishangai hata kidogo.
Miaka kadhaa iliyopita pale Nairobi, Embakassy Airport, waandishi wa habari walimzonga Mwalimu kwa habari za uongo.
Mwalimu aliwauliza" hivi ninyi mkiambiwa mama zenu ni wake zangu mtaamini"
Waandishi wakaanza kutoweka mmoja mmoja.
Zumbemkuu mix with yours.
 
duh! hii nayo kali ha ha ha ha ha ha!
 
Wapendwa jana niliweka thread hii kuhusu mustakabali wa Shibuda ndani ya Chadema kuhusu utovu wake wa nidhani kwenda kinyume na maazimio ya chama chake.
Kama mmesikia leo Marin Hassan wakati akiohojiana na aliyekuwa katibu wa Bunge, George Mlawa, ameweka wazi kuwa Shibuda anaweza kabisa kulindwa na Katiba ibara ya 100 inayomkinga Mbunge na KUCHUKULIWA HATUA YA KISHERIA/UWAJIBIKAJI KWA lolote atakalolitamka Bungeni. Amekwenda mbali na kutoa mfano wa Jidawi aliyekuwa CUF alivyokipeleka chama High court na kushinda kufukuzwa kwake.
Narudia tena Busara kubwa itumike ku-handle issue hii.
FIKIRI CHUKUA HATUA

mkuu iyo kanuni inamlinda mbunge kutochukuliwa hatua kisheria. Ccm haiwezi kumtumia katibu wa bunge kulinda wavunja kanuni za vyama. Ivi kuna mtu anaweza kukichagulia chama wabunge?? Cdm ikitaka kadi ya chibuda inarudi tu! We can decide to call back and forteit the membership without prior referral permit from the government provided the resolution by member representatives is considered. Ccm msijidanganye na kinga yenu. Je cdm ikiitaka kadi mtafanya chibuda private member of parliament au?? Ccm acheni ujuha!
 
Jamani toeni source ili tuamini, halafu ndiyo tuijadili hii thread!!

Wala usiumize kichwa Siku CHADEMA wanazindua Kampeni Dar nilimsikia Mimi kwa Masikio yangu akisema.ukitaka kwenda mjini umepanda gai likapata pacha unashuka na kusimamisha lingine bora tu mjini ufike wakati wa kurudi utajua njia ya kurudia "BASI LA CCM LIMEPATA PANCHA NIMEDANDIA BASI LA CHADEMA NAENDELEA NA SAFARI"
 
kwa masikio yangu nilimsikia kabisa pale jangwani.
 
Mleta mada anaweza kuwa na hoja lakini ameshindwa kabisa kujenga hoja
 
kw tunavyomjua shibuda haya siyo kitu cha ajabu ndo anavyoongea. Nadhani anajiamini kuwa anaweza kurudi bungeni kwa njia nyingine.

NAFIKIRI KITU CHA MSINGI HAPA SIYO KWA CHADEMA KUPOTEZA AU KUTOPOTEZA JIMBO.

cha msingi hapa ni kipi chadema wanansimamia kama wapinzani na je shibuda anasimamia yaleyale? Kama hasimamii mambo ya msingi ya kipinzani basi haijalishi kama chadema itabaki na wabunge watano wanao beba mahitaji ya kipinzani wanayoyataka watanzania walio wengi hivi sasa.

sidhani kama chadema wanapaswa kuhangaika na kupotea au kurejesha jimbo la shibuda.

Wote tunajua kama wananchi wa jimbo la shibuda wameamka, hawataweza kumrudisha shibuda bungeni kwa kauli zake alizozitamka mwenyewe kwa mdomo wake.

Chadema wakae waamua kulingana na wengi wanataka nini. Nadhani shibuda hatafukuzqa na chadema ila atafukuzwa na wanaharakati wa mageuzi tanzania. Maana kama uongozi wa chadema watamkingia kifua basi wanaharakati wa mageuzi watawahukumu na wao pia.

Nilishawahi kuchangia kuwa shibuda wamkabidhi kwa mkutano mkuu wa chadema waamue wenyewe. Lakini pia ni gharama kubwa zisizo na msingi wakati maoni ya wadau wengi wa upinzani tayari yanamkataa shibuda.
 
Je munafikiri ni sababu hizi hapa juu tu zitatosha kumfukuza uanachama na hatimaye Ubunge wake?
Kumbukeni kwa mujibu wa kinga za Bunge akiwafikisha mahakamani atawabwage na kuendelea na Ubunge kwa jimbo la Mahakama.

Punguzeni jazba muangalie nchi Yenu inakwendaje.

Je mnajua kuwa Mkoa wa Shinyanga na Mwanza kuna Njaa? jana nilikuwa ngudu hali ni mbaya sana. magonjwa yameingia mashambani hivyo vyakula vyote vimakauka. Njaa kali kweli kweli.

Je

kwani wabunge wa huko huwajui? Kwani serikali inayoitawala tanzania huijui? Sasa vijineno vyako wamletea nani jamvini. Narudia cdm inaweza kumfuta mwanachama yeyote bila kujenga mashtaka,hata kwa kutokuwa na imani naye. Ccm mwajisumbua tu. Hamna wa kwenda mahakaman kumstaki shibuda,hapa na kumfuta uanachama basi. Kama anautaka ubunge abaki nao ila si kupitia mtu goi goi.
 
Unaongea too much tena pumba, hata mchango ulioutoa hakuna value yoyote ya kugain. Ndio maana umewaudhi wachangiaji hadi unatukanwa. Kama ni kweli usemayo kuwa kuna gazeti unaliandikia basi wamekula hasara. Kama mhariri wako hajakujua upeo wako hadi sasa na yeye hafai vilevile.

Funga mdomo wewe! acha wenye upeo mkubwa wajadili haya mambo kwa mantiki wewe kanywe mbege kule! we vipi aisee? kama umezoea umbeya hapa si mahala pake, kwanza ulijiungaje hapa? na shaka na uwezo wako wa kujenga hoja kidogo naweza kushawishika wewe ni mtaalamu wa kutukana tu,pumbafuuuu!
 
Wala usiumize kichwa Siku CHADEMA wanazindua Kampeni Dar nilimsikia Mimi kwa Masikio yangu akisema.ukitaka kwenda mjini umepanda gai likapata pacha unashuka na kusimamisha lingine bora tu mjini ufike wakati wa kurudi utajua njia ya kurudia "BASI LA CCM LIMEPATA PANCHA NIMEDANDIA BASI LA CHADEMA NAENDELEA NA SAFARI"

ndugu mbona mnachanganya habari? Umeombwa source ya mada hii wala si source ya maneno asemayo shibuda popote. Kweli kabisa gari ikiwa mbovu mtu anashuka,na kama akipanda gari ya cdm ataenda ila si kupanda gari alaf unamwambia dreva wa gari ya cdm eti apige u turn afuate mizigo yako kule gari mbovu ya ccm,hata ikiwezekana itabidi ikugharimu kama inavomgharimu magale shibuda. Hatupingi kuwa gari bovu ccm lakini kama ukishashuka unashuka kabisa. Hatutailaumu cdm kuwapokea wanaCCM waliouona ukombozi ila wakienda cdm wawe wameiva. Yupo Dr. Willbroad Slaa,alikuwa ccm damu damu ila sisiemu ilipokengeuka akashuka,ivi leo anaendesha gari mpya akiwa co pillot na mbowe! Tunaowengi waliotokea huko. Ila yeyote asiye upande wa cdm basi awe upande mwingne. Shibuda hatufai milele.
 
Hapa hapa kuna waandishi watatu wamemhoji Mh Shibuda, huyu moja wa kike namfahamu bila shaka hawezi kupeleka hii taarifa kwa maana maboss wake watamshangaa sana, mimi nilimuuliza swali tofauti kidogo...."je mh Shibuda unaonaje mustakabali wako wa siasa kutoka CCM na sasa CHADEMA.?.."

Akajibu hivi..."ni sawa ila angalizo langu kwa CHADEMA wajifunze kuheshimu mtu mwenye mawazo tofauti na wao.."

Sasa katika kujibu maswali ya wenzangu ndiyo akasema hayo maneno ya kwenye thread hapo juu, ila msihofu wadau kesho nitajitahidi kwa nia yoyote niichomeke hii habari kwenye gazeti toleo la kesho.

aisee kama we ni muandishi basi mwandishi wa ngazi ya familia. Hauna professiönal ethics hata robo. Yani unasema umetoa dokezo/suna alaf habari uiweke kwenye gazeti? Itanichukua miaka mingi kujua kama we umesomea uandishi wa habari au ni deiwaka ktk habari. Hauaminiki tena.
 
Back
Top Bottom