Lissu amlima barua Shibuda

Lissu amlima barua Shibuda

Hii ishu ya Shibuda inahitaji umakini wa hali ya juu..
 
Wapendwa jana niliweka thread hii kuhusu mustakabali wa Shibuda ndani ya Chadema kuhusu utovu wake wa nidhani kwenda kinyume na maazimio ya chama chake.
Kama mmesikia leo Marin Hassan wakati akiohojiana na aliyekuwa katibu wa Bunge, George Mlawa, ameweka wazi kuwa Shibuda anaweza kabisa kulindwa na Katiba ibara ya 100 inayomkinga Mbunge na KUCHUKULIWA HATUA YA KISHERIA/UWAJIBIKAJI KWA lolote atakalolitamka Bungeni. Amekwenda mbali na kutoa mfano wa Jidawi aliyekuwa CUF alivyokipeleka chama High court na kushinda kufukuzwa kwake.
Narudia tena Busara kubwa itumike ku-handle issue hii.
FIKIRI CHUKUA HATUA

Mimi Si na wala sijawahi kuwa mwanasheria lakini nakumbuka Cheyo 'mapesa' alinyang'anywa wadhifa wa waziri kivuli kwa matamushi yake Bungeni. Akafurukuta lakini spika akasema Opposition wako sahihi kumpiga teke. Ikawa hivyo!

Ni maamuzi gani ambayo yanapita na yapi hayapiti?
 
Hapa hapa kuna waandishi watatu wamemhoji Mh Shibuda, huyu moja wa kike namfahamu bila shaka hawezi kupeleka hii taarifa kwa maana maboss wake watamshangaa sana, mimi nilimuuliza swali tofauti kidogo...."je mh Shibuda unaonaje mustakabali wako wa siasa kutoka CCM na sasa CHADEMA.?.."

Akajibu hivi..."ni sawa ila angalizo langu kwa CHADEMA wajifunze kuheshimu mtu mwenye mawazo tofauti na wao.."

Sasa katika kujibu maswali ya wenzangu ndiyo akasema hayo maneno ya kwenye thread hapo juu, ila msihofu wadau kesho nitajitahidi kwa nia yoyote niichomeke hii habari kwenye gazeti toleo la kesho.
 
Kama unataka kujua kwamba hiyo sheria ni ya Kisese, jaribu siku moja kumtukana Mkwekwe pale bungeni ndio utajua kama kweli kuna kinga hiyo au la. Ni hao hao vibaraka kama Kashilila ndio watakaotuambia kwamba kinga kama hiyo hakuna
 
Hii sheria inamlinda mbunge awapo bungeni, i mean kama mbunge, lakin mbunge huyu afukuzwapo na chama chake basi hana chake tena, Anapoteza sifa ya ubunge na hata hiyo sheria haitoi ulinzi tena!
mkuu sheria ipo wazi mbunge anakinga kwa lolote asemalo au atendalo akiwa bungeni, hawezi kushitakiwa kwa kitu alichosema au kutenda akiwa bungeni, Chama CDM haina mamlaka ya kumuwajibisha kwa matamshi yake bungeni. Kama amekiuka shreia ndani ya bunge basi kanuni za bunge na bunge ndo linatumika kumwajibisha sio mahakama wala chama unless such miscounduct is criminally in nuture to the extent that immunity is rebbuted.... legal issue are dealt with laws not politics, maamizi mengi yana igharimu hii inchi na taasisi tofauti kwa kukuika vipengele vidgo sana, maamuzi ya kukulupuka bila kujua sheri inasemaje itatucost.... ngoja nikupe mfano.... wewe ni bosi, mfanya kazi wako kaiibia kampuni na umemkata, kwa kukurupuka unamfukuza bila kumpa haki ya kumsikilza, akienda mahakmani utamlipa fidia kubwa ya mshahra wa miezi isyopungua 12.... unaona tonavyopteza haki kwa uzembe mdogo
 
Hii ni thread ya Kutunga iliyoletwa na Kibaraka wa Nape. Akaipeleke CCM ndipo watamwamini maana kule ndipo kulikojaa Makapi hayana akili ya kuchambua uongo na ukweli
 
Nakushauri upitie katiba ya Tanzania usome ibara ya 100 inasemaje
Powers and Privileges of Parliament"100.-(1) There shall be freedom of opinion, debate and procedure of business in the National Assembly, and that freedom shall not be breached or questioned by any organ in the United Republic or in any court or elsewhere outside the National Assembly. (2) Subject to this Constitution or to the provisions of any other relevant law, a Member of Parliament shall not be prosecuted and no civil proceedings may be instituted against him in a court in relation to any thing which he said or done in the National Assembly or has submitted to the National Assembly by way of a petition, bill, motion or otherwise."Je, Shibuda analindwa na Ibara hiyo?
 
Sidhani kama akifukuzwa chadema na yeye atatoka na kundi la watu wake! atatoka peke yake tu. acha tuone
 
Powers and Privileges of Parliament"100.-(1) There shall be freedom of opinion, debate and procedure of business in the National Assembly, and that freedom shall not be breached or questioned by any organ in the United Republic or in any court or elsewhere outside the National Assembly. (2) Subject to this Constitution or to the provisions of any other relevant law, a Member of Parliament shall not be prosecuted and no civil proceedings may be instituted against him in a court in relation to any thing which he said or done in the National Assembly or has submitted to the National Assembly by way of a petition, bill, motion or otherwise."Je, Shibuda analindwa na Ibara hiyo?
Na KATIBA ya CHADEMA inasemaje kuhusu kumfukuza mtu uanachama?
 
Kama unataka kujua kwamba hiyo sheria ni ya Kisese, jaribu siku moja kumtukana Mkwekwe pale bungeni ndio utajua kama kweli kuna kinga hiyo au la. Ni hao hao vibaraka kama Kashilila ndio watakaotuambia kwamba kinga kama hiyo hakuna
mkuu kinga ina mipaka, hata uhuru wa kutoa maoni pia unamipaka, kinga ni kwa shughuli rasmi za kibunge, hata akitoa matusi bunge kwa kanuni za bunge litamtaka afute kauili kwanza, akigoma hatua nyingine zitafuata, unapoongea fikilia sipendi kushusha udhamini was uwezo ako wa kufikilia ila pia sidhani unaweza kumpigia kula mtu wa kwenda kutukna bungeni
 
Na KATIBA ya CHADEMA inasemaje kuhusu kumfukuza mtu uanachama?
hata kaitiba ya chadema isemeje, sheria yoyote inayopingana au inayoenda kinyume na KATIBA YA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA ni batili, null and void
 
Suala hapa sio kwamba chadema inamfukuza Ubunge bali inamvua uanachama. Kwa hiyo hilo bunge litaamua kama wanaweza kumwachia aendelee kuwa mbunge hali si mwanachama wa chama chochote hiyo nikazi kwao, na hapo watakuwa wamehalalisha mgombea binafsi.
 
Powers and Privileges of Parliament"100.-(1) There shall be freedom of opinion, debate and procedure of business in the National Assembly, and that freedom shall not be breached or questioned by any organ in the United Republic or in any court or elsewhere outside the National Assembly. (2) Subject to this Constitution or to the provisions of any other relevant law, a Member of Parliament shall not be prosecuted and no civil proceedings may be instituted against him in a court in relation to any thing which he said or done in the National Assembly or has submitted to the National Assembly by way of a petition, bill, motion or otherwise."Je, Shibuda analindwa na Ibara hiyo?

Mimi nadhani yapo mambo mengi tena mabaya zaidi aliyosema Shibuda nje ya bunge, alipofanya mahojiano na gazeti la Mtanzania na ambayo nadhani wanaweza kuyatumia.
 
mkuu sheria ipo wazi mbunge anakinga kwa lolote asemalo au atendalo akiwa bungeni, hawezi kushitakiwa kwa kitu alichosema au kutenda akiwa bungeni, Chama CDM haina mamlaka ya kumuwajibisha kwa matamshi yake bungeni. Kama amekiuka shreia ndani ya bunge basi kanuni za bunge na bunge ndo linatumika kumwajibisha sio mahakama wala chama unless such miscounduct is criminally in nuture to the extent that immunity is rebbuted.... legal issue are dealt with laws not politics, maamizi mengi yana igharimu hii inchi na taasisi tofauti kwa kukuika vipengele vidgo sana, maamuzi ya kukulupuka bila kujua sheri inasemaje itatucost.... ngoja nikupe mfano.... wewe ni bosi, mfanya kazi wako kaiibia kampuni na umemkata, kwa kukurupuka unamfukuza bila kumpa haki ya kumsikilza, akienda mahakmani utamlipa fidia kubwa ya mshahra wa miezi isyopungua 12.... unaona tonavyopteza haki kwa uzembe mdogo

Afadhali umeonyesha njia. Chadema wasikurupuke kumfukuza Shibuda, atawadhalilisha mahakamani. The law relating to parliamentary immunity is so express such that it does not need interpretation or extrapolation. hapa hakuna intention of the legislature or court discretion etc
 
Nani amtimue? utawala wa cdm wamesha ona lakini wakimgusa tu jimbo hilo bye bye. mtakuwa mnalisikilizia kwenye mitandao. kwani mpaka kuhama chama na ghafla kushinda inaonekana jimboni kwake anakubalika yeye kama yeye na siyo chama.

Nimeguswa na mtizamo wako mdau kuhusu Mh. Shibuda. Sishawishiki kuamini kwamba eti Mh.huyu alitumwa na CCM kwenda CDM kwenda kuvuruga.Na hii ni kutokana na ukweli unaojengwa katika historia ya harakati za kisiasa za comrade huyu. Kwa wenye kufuatilia kwa karibu siasa za hapa nchini hasa ndani ya CCM watakubaliana nami kwamba Mh.Shibuda alikuwa ni mwanasiasa asiyeaminika mbele ya viongozi wenzake ndani ya CCM kwa muda mrefu kuanzia kipindi ambacho alikuwa akigombea nafasi ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM enzi za Mzee Iddi Simba.Mara kadhaa jina lake lilikuwa likikatwa na vikao husika.Na mara zote alikuwa akilalama sana juu ya hali hiyo ya viongozi wenzake ndani ya CCM kutokuwa na imani naye pindi alipokuwa anaonesha nia ya kutaka kushika nyadhifa kubwa kubwa ndani ya CCM ingawa alishawahi kuwa mjumbe wa NEC-Wazazi kwa miaka kadhaa huko nyuma akiwa anaishi visiwani Zanzibar.
Hata lilipokuja suala la kumteua kugombea ubunge mwaka 2005 kwenye jimbo lake kwa tiketi ya CCM haikuwa kazi rahisi kutokana na ukweli kwamba viongozi wa CCM Mkoa wa Shinyanga hawakuwa wakiunga mkono kuteuliwa kwake pamoja na ukweli kwamba ndiye aliyekuwa chaguo la wanaccm wa Maswa. Vikao vya juu vya CCM vya uteuzi kwa kutambua ukweli kwamba Bwana huyu anakubalika jimboni,vikawa havina mbadala zaidi ya kuamua kurudisha jina lake na Mh.Shibuda akashinda kwa kura nyingi tu.
Sasa ilipotokea kwamba mwaka jana 2010 kuna mwanaCCM kaibuka na kumzidi kete kwenye kura za maoni , CCM wakafanya kosa kwa kujikita zaidi kwenye matokeo ya kura za maoni bila kupima hali halisi ya kukubalika kwake jimboni.Bwana huyu alilalamika sana kwamba wananchi bado wanamkubali na kwamba kilichotokea ni ghiliba za kura maoni.Hatahivyo,kilio chake hakikusilikizwa na haswa kwakuwa alikuwa ni mtu anayewindwa na makada wenzake. Kilichotokea ndicho hicho tulichoshuhudia kuamua kutafuta njia nyingine ya kurudi bungeni huku mataji wake mkubwa ukiwa ni wapiga kura wa Maswa na wala sio Chama au viongozi wake.Kwa lugha nyingine ni kwamba, kama nchi yetu ingeruhusu mgombea binafsi naamini kwa asilia zote kwamba bwana huyu angesimama kama mgombea binafsi na kuweza kushinda bila tatizo. Kwahiyo, ni changamoto kwa wanacdm mtakapotaka kuchukua uamuzi wa aina yoyote basi ni dhahiri pia mjiandae kukubaliana na lolote litakalotokea. Mh.Shibuda ni aina ya wanasiasa ambao sio rahisi kuwaelewa kiundani dhamira zao. Kwahiyo ni suala la busara na uvumilivu linalotakiwa kuzingatiwa unapokuwa na wanasaisa wa aina yake.
 
Inasikitisha km katibu wa bunge hajui kuwa ukifukuzwa uanachama wa chama cha siasa basi na ubunge wako unakoma,mkumbuke hatuna sheria ya mgombea binafsi bado.chadema wanaweza kumfukuza shibuda kwa kosa la uwajibikaji wa pamoja.
 
Kama nilivyoandika mwaka jana,Shibuda ni mlevi. Kwamba alipokuwa anaishi Upanga,alikuwa ana tabia ya kutoka kwenye pombe usiku na kupaki gari kwenye parking lot ya CCM Upanga,na kulala ndani ya gari mpaka asubuhi. Kwa hiyo siyo ajabu kwamba they cannot see eye to eye kuhusu posho yeye na wana CHADEMA wenzake.
I would say what wanakitamani kiti chake cha ubunge na wanataka kumtimua,au wameshamtimua. I would imagine kwamba this is a little bit unfair. Kwa sababu defection ya Shibuda wakati ule iliongeza prestige ya Chadema katika Uchaguzi.
This is not fair. Sasa utakuwa na mtu hawezi kukaa CHADEMA na hawezi kurudi CCM.
Watu walevi,watu wanaotaka kuishi maisha ya tamaa,oftentimes wanakuwa wezi. Kuna ubaya gani mtu kuing'ang'ania posho ili baadaye asishawishike kuwa mwizi?
 
Back
Top Bottom