Our politicians need to be true patriots.
Ntafurahi sana kama Dr. Salim atajitoa CCM na kwenda kugombea urais kupitia CCJ au chama kingine chochote.
Kwenye kongamano la Nyerere waliongea mambo mengine sana kwa manufaa ya taifa ambayo wanajua JK hawezi kuyatolea maamuzi. Kwann wasiachane na CCM na kujiunga na upinzani ili waiweke nchi katika mstari sahihi?!
The right thing that he can now do it to quit CCM and join opposition. Asipofanya hvyo hatakuwa mzalendo wa kweli. Haiwezekani aone nchi inapelekwa kuangamia halafu anyamaze ashindwe ku-play his part.
Inflation inakaribia double digits, mishahara ya wafanyakazi kima cha chini haiwezi kufikia 315,00/= even after 8yrs, donors wamepunguza misaada by 25% (I think), Nchi haina Vision inayoeleweka kwa kila mwananchi kwamba over the next 50 to 100 years tunataka nchi yetu ifikie level gani, bei ya petrol na vyakula inapanda kila kukicha, barabara zinaharibika kila kukicha and no action, bidhaa feki zimejaa mpaka tunaziona ni genuine, Tshs inazidi kushuka dhamani kila siku, hata kuzuia matumizi ya dollar nchini ameshindwa ndo kwanza ana insist TRA wawe wanadai kodi kwa dollar(Si aifute shillingi kabisa tujue hatuna hela), umeme nao unapanda, nauli za daladala nazo zinapanda, mabasi yandayo kasi yamekuwa nightmare, traffic jam kashindwa kuiondoa, yaani hata kuplan kuhamisha uwanja wa ndege uende nje ya mji hawezi, anafaikiria kuendelea kuwabomolea watu (Sijui tutabomoa mpaka wapi?). It is a mess, I can't even mention EPA, Richmond and the like.
Tunapelekwa na sera mpya kila kukicha zisizo na mchanganuo wa kweli wa kiutekelezaji. Mara kasi mpya, mara misha bora, mara kilimo kwanza na nna uhakika wakati wa uchaguzi atakuja na mpya.
Pamoja na hayo yote; I still strongly believe: one day change will happen, and I'll be part of that change!
Sure I'll!
God have mercy with this Country!
Ingekuwa vizuri sana CCM ingeng'olewa kutoka madarakani mwaka huu. Lakini sitegemei mabadiliko hayo katika uchaguzi ujao. Ni Kikwete tena.
Salim Ahmed Salim anajua hawezi kuingia Ikulu bila CCM. Ni chama ambacho hakina upinzani mkubwa, au wa kutosha, hasa Tanzania bara. Akichaguliwa mwaka huu na vigogo wa CCM kuwa makamu wa raisi, badala ya Ali Mohammed Shein, kuna tumaini kubwa sana kwamba atakuwa raisi wa Muungano baada ya Kikwete kuondoka Ikulu mwaka wa 2015.
Wanaosema ni zamu ya Zanzibar kulipa taifa letu raisi wa Muungano wataridhika Dr. Salim akichaguliwa 2015, ingawa katiba ya Muungano haisemi tupeane zamu kati ya visiwa na bara tunapomchagua raisi wa nchi yetu.
Pia hao Wazanzibari wanao lialia na kusema ni zamu yao kulipa taifa letu raisi wa Muungano, wakumbuke kwamba ndiyo wao wenyewe waliompinga Dr. Salim tangu 1985 kuhakikisha kwamba haingii Ikulu. Walimpinga Dr. Salim Mwalimu Nyerere alipokuwa hai, na walimpinga hata baada ya Mwalimu kutuondoka. Na hata leo kuna wengi visiwani ambao wanampinga na hawataki awe raisi wa Jamhuri ya Muungano au Zanzibar.
Akichaguliwa kuwa makamu wa raisi wa Muungano mwaka huu ili apate njia na nafasi ya kuingia Ikulu baada ya Kikwete kuondoka Ikulu 2015, itakuwa ni kwa sababu vigogo wa CCM kutoka Tanzania bara wameamua kufanya hivyo. Hakuna kiongozi anayeweza kuchaguliwa kuwa kiongozi wa Muungano bila uamuzi wa vigogo katika CCM upande huu wa Muungano, yaani Tanzania bara.
Ndugu zetu visiwani wakumbuke kwamba ikiwa vongozi wa CCM wanataka tupeane zamu, kati ya bara na visiwa kulipa taifa letu raisi au makamu wa raisi wa Muungano, ni kwa sababu wanataka kufanya hivyo, na siyo kwa sababu ya katiba. Ni sawa na kule Nigeria ambako viongozi wa chama cha utawala, People's Democratic Party, kutoka kaskazini na kusini ya nchi, wamekubaliana kwamba ikiwa raisi wa Shirikisho la Nigeria anatoka kusini, makamu wake ni lazima atoke kaskazini. Na baada ya hapo, raisi ni lazima atoke kaskazini ikiwa kabla ya hapo raisi wa Shirikisho alitoka kusini. Tofauti kati ya CCM na People's Democratic Party kule Nigeria ni kwamba chama cha Winigeria kina katiba inayosema hivyo.
Hata tukiendelea kupeana zamu kati ya bara na visiwa kumchagua raisi wa Muungano, na ikiwa Dr. Salim ataingia Ikulu baada ya uchaguzi wa 2015, jambo la kusikitisha, na ambalo ni la kusikitisha sana, ni kwamba bado tutakuwa chini ya uongozi wa chama kibovu: CCM.
Salim angechaguliwa kuwa raisi wa Muungano 2005, au kabla ya hapo, wapinzani wake wasingemchafulia mambo miaka hiyo. Lakini bado kuna uwezekano atachaguliwa kuwa raisi wa Tanzania, vigogo wa CCM bara wakiamua kufanya hivyo, ingawa kuna Watanzania wanaosema muda wake umepita.