Lipumba usiwe na ubinafsi kama Lowassa

Lipumba usiwe na ubinafsi kama Lowassa

umoja wa mashaka huu.... ukiyaomba majina yako ndo utazimia kabisa ,, na ndio utajua pingamizi lina chanzo chake
 
Sasa naona ukumazan ushaanza ukawa... badala ya kuwaza UKOMBOZI... mnawaza umimi, ubinafsi, nani bora kuliko nani... mtatembelea hadi tigo zenu, bila KUSHINDA mkiacha kuungana na Lowassa mfanye very strong combination ya ushindi...

Watu wa Ukawa, waache kufikiria madaraka, wawaze KULIKOMBOA TAIFA... sio muda wa kuwaza kugawana vyeo au nani awe nani, fikirieni mbinu za ushindi...!!" Makumazan nyie
 
Soory charlie !!! mimi sijakuuliza mambo ya biashara

suali lilikuwa

kwani chadema wangaligombea Zanzibar wangalishinda ??
Chadema wamezingatia kwamba CUF inakubalika zaidi Zanzibar wakawaachia CUF watoe mgombea huko. Ni busara na kwa Lipumba kutambua kuwa hana ushawishi bara na awaachie Chadema wanaokubalika zaidi bara. Halafu, Lipumba azingatie kuwa si busara wao CUF pekee wasimamishe mgombea sehemu zote, bara na visiwani. Hapa napata mashaka makubwa na u-professa wa Lipumba na pia sijui ana agenda gani binafsi iliyojificha.
 
Kauli Ya lipumba kasema ni mambo tu yanamzidi yy hapingi maamuzi Ya UKAWA.
Hii habari ya kuwa CUF watatoa uamuzi tarehe 25 July siyo game ya mapatano bali Lipumba amedhamiria kukwamisha malengo ya UKAWA kwa sababu ya ubinafsi wake.
 
Ni wakati wa kumuonya Lipumba asiwe kama Lowassa ambaye kwa ubinafsi wake alifikiri Tanzania ni yeye na yeye ndiye Tanzania kana kwamba nchi hii ni mali yake. Lipumba ni wakati wa kusoma alama za nyakati.

Acha kung'ang'ania kugombea urais wakati ukijua hauna ushawishi Tanzania bara.Kura ulizopata ni ushahidi tosha, na wewe kama msomi usifiche kichwa chako kwenye machanga huku mwili wako mzima unaonekana.

Lipumba asilazimishe kupendwa kama Lowassa. Lipumba ukiwa ndani ya UKAWA, waachie CHADEMA wapeperushe bendera ya urais kwa kuwa ni ukweli uliowazi kuwa wanakubalika zaidi Tanzania bara kuliko wewe na chama chako.

Pili CUF tayari imepewa nafasi ndani ya UKAWA kupeperusha bendera ya rais upande wa Zanzibar.

Sasa ubinafsi gani tena huu wa kung'ang'ania kugombea urais kama Lowassa?

Acha hizo Lipumba, toa nafasi kwa UKAWA kumpata rais wa Tanzania kwa kumuunga mkono Dr. Slaa ambaye anauzika kirahisi kuliko wewe.

Mimi nawashangaa mnaomtaka lipumba akatae kugombea urais,kuna kitu watu wanakikwepa hapa,
1.cuf kwa mlengo wao wa kisiasa jinsi ilivyo hawawezi kumuunga mkono mkatoliki tena padre,
2.cuf ndio chama ambacho kichinichini kinajinasibu kuwa ndio mtetezi wa waislamu,sasa kitamuungaje mkono mgombea ambae ni mkristo?
NOTE:Muulize ni mtatiro kwanini hayupo kwenye ile nafasi ambayo iko chini ya sakaya kwa sasa!
 
Mimi nawashangaa mnaomtaka lipumba akatae kugombea urais,kuna kitu watu wanakikwepa hapa,
1.cuf kwa mlengo wao wa kisiasa jinsi ilivyo hawawezi kumuunga mkono mkatoliki tena padre,
2.cuf ndio chama ambacho kichinichini kinajinasibu kuwa ndio mtetezi wa waislamu,sasa kitamuungaje mkono mgombea ambae ni mkristo?
NOTE:Muulize ni mtatiro kwanini hayupo kwenye ile nafasi ambayo iko chini ya sakaya kwa sasa!

Na vilevile CHADEMA ndio chama ambacho kichini-chini kinaonekana kama chama cha wakristo. Hivyo basi ikiwa UKAWA watamuweka Slaa agombee urais wasitegemee kwamba waislamu watampigia kura na ikiwa UKAWA watamuweka Lipumba wasitegemee kwamba wakristo watampigia kura huo ndio ukweli na ndio tatizo na kitu cha kusikitisha wao kama viongozi inamaana hawakuijua situation hii mpaka inafika dakika za lala salama ndio wanaanza kuwachanganya watu?!
 
Sio lipumba tu hta dr slaa nae inabidi akae pembeni cz hauziki kwa wananchi wote walishagombea na wakakosa tunahitaji sura mpya ukawa
 
Sio lipumba tu hta dr slaa nae inabidi akae pembeni cz hauziki kwa wananchi wote walishagombea na wakakosa tunahitaji sura mpya ukawa
Ona ukweli mkuu. Slaa alipata kura nyingi kiasi kwamba alikaribia kuwa rais. Hata takwimu za urais wa Kikwete haijawahi kuwa wazi na ya kuaminika. Wengi wanaamini Slaa alipata kura za kutosha kuwa rais. Lipumba hana ushawishi bara na kura zake zinaonyesha hivyo kwa mara nne alizogombea urais. Lipumba anatambua kuwa hakubaliki bara ndiyo maana aliamua kumfanyia kampeni Kikwete ilihali na yeye alikuwa anagombea urais. Kikwete alikuwa na hali mbaya kwa Dr. Slaa na hili Lipumba analijua. Lipumba kungangania kugombea urais bara ni mwendeleze uleule wa kutotaka kumuunga mkono Dr. Slaa kwa sababu ya ubinafsi wake kama alivyofanya mwaka 2010.
 
Hawa maprofesa wetu balaa. Jana anasema Lowassa ni msafi kwa sababu ufisadi umeendelea kuwepo hata baada ya Lowassa kujiuzulu uwaziri mkuu halafu leo anasema dhamira inamsuta kwa maamuzi aliyofanya kumuunga mkono Lowassa. Hivi Professor anashindwa kuwa consistent ndani ya siku chache anawezaje kuaminika kwa kauli yoyote nyingine anayotoa? Sasa u-professor wa nini na ameupataje kama anakuwa inconsistent kwa kiwango hiki?
 
Mkuu Stabilaiza. utasumbuka bure, kansa imeshakula watu, hawasikii wala kuona.
WAO WAKIONESHWA BLUU WANASEMA NI NYEUPE
 
Usidanganyike mkuu dini na siasa Ni vitu tofauti na ukisema uchambue huwezi jivua gamba toka huko
 
Back
Top Bottom