Ni wakati wa kumuonya Lipumba asiwe kama Lowassa ambaye kwa ubinafsi wake alifikiri Tanzania ni yeye na yeye ndiye Tanzania kana kwamba nchi hii ni mali yake. Lipumba ni wakati wa kusoma alama za nyakati.
Acha kung'ang'ania kugombea urais wakati ukijua hauna ushawishi Tanzania bara.Kura ulizopata ni ushahidi tosha, na wewe kama msomi usifiche kichwa chako kwenye machanga huku mwili wako mzima unaonekana.
Lipumba asilazimishe kupendwa kama Lowassa. Lipumba ukiwa ndani ya UKAWA, waachie CHADEMA wapeperushe bendera ya urais kwa kuwa ni ukweli uliowazi kuwa wanakubalika zaidi Tanzania bara kuliko wewe na chama chako.
Pili CUF tayari imepewa nafasi ndani ya UKAWA kupeperusha bendera ya rais upande wa Zanzibar.
Sasa ubinafsi gani tena huu wa kung'ang'ania kugombea urais kama Lowassa?
Acha hizo Lipumba, toa nafasi kwa UKAWA kumpata rais wa Tanzania kwa kumuunga mkono Dr. Slaa ambaye anauzika kirahisi kuliko wewe.