Lipumba usiwe na ubinafsi kama Lowassa

Lipumba usiwe na ubinafsi kama Lowassa

Stabilaiza

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2012
Posts
1,843
Reaction score
1,143
Ni wakati wa kumuonya Lipumba asiwe kama Lowassa ambaye kwa ubinafsi wake alifikiri Tanzania ni yeye na yeye ndiye Tanzania kana kwamba nchi hii ni mali yake. Lipumba ni wakati wa kusoma alama za nyakati.

Acha kung'ang'ania kugombea urais wakati ukijua hauna ushawishi Tanzania bara.Kura ulizopata ni ushahidi tosha, na wewe kama msomi usifiche kichwa chako kwenye machanga huku mwili wako mzima unaonekana.

Lipumba asilazimishe kupendwa kama Lowassa. Lipumba ukiwa ndani ya UKAWA, waachie CHADEMA wapeperushe bendera ya urais kwa kuwa ni ukweli uliowazi kuwa wanakubalika zaidi Tanzania bara kuliko wewe na chama chako.

Pili CUF tayari imepewa nafasi ndani ya UKAWA kupeperusha bendera ya rais upande wa Zanzibar.

Sasa ubinafsi gani tena huu wa kung'ang'ania kugombea urais kama Lowassa?

Acha hizo Lipumba, toa nafasi kwa UKAWA kumpata rais wa Tanzania kwa kumuunga mkono Dr. Slaa ambaye anauzika kirahisi kuliko wewe.
 
Stabilaiza

Umeniwahi mkuu, na unatakiwa uitwe tranquilizer.

Lipumba anatakiwa akubali ukweli kwamba hata kama akiwekwa na UKAWA, hatachaguliwa kwa kuwa tu ni ukawa kwa vile pia hana influence kubwa kwa bara.

Ninajua huyu ndugu ni msomi atarejea maafikiano ya awali kwamba katika kuteua wagombea ndani ya ukawa, watazingatia pia mafanikio ya chama katika awamu iliyopita ambapo lipumba hakuwa na kura za kujisifia kiasi hicho.

Kama anang'ang'ania kugombea uraisi akidhani atapita kwa kuwa watu wanasema hata jiwe la ukawa watalilpigia kura, siyo kwa namna anavyodhani yeye. Lipumba asimamie chama kishinde Zanzibar ambako kaachiwa nchi nzima, na huku bara aachie wengine. Tamaa si nzuri na mwisho wake ni tabu.

Ninaimani amesikia na washauri wake watamshauri vizuri sasa.
 
Last edited by a moderator:

Unajua ukimchekea nyani utavuna mabua.
 
Kwani vipi? Kwani ndiyo kikwazo cha kumpata mgombea wa urais? Lipumba asahau urais wa Tanzania, iwe ndani au nje ya UKAWA, angekuwa na uwezo mara zote alizojaribisha angeongeza ongeza kura zikatosha.
Mgombea wa ukawa kwa sasa ni Dr. Slaa tu, anayeweza kupeta kwa urahisi. Kinyume chake hata wabunge hawataongezeka kwenye vyama vya upinzani ndani ya UKAWA.
 
Alikiri kumsaidiq JK kushinda. Huyu nae ana matatizo kichwani mwake
 
Stabilaiza

Lipumba is another hopeless spent force. Mlio karibu nae mwambie afanye talling ya kura tangu agombee urais then afanye analysis! Ndio maprofesa wa bongo
 
Last edited by a moderator:
CUF nao wanataka kuchekesha, yaani wagombee uraisi zanzibar, na huku Bara pia! Kwanza washukuru mbeleko ya Chadema wataongeza viti vya ubunge na madiwani
 
Lipumba is another hopeless spent force. Mlio karibu nae mwambie afanye talling ya kura tangu agombee urais then afanye analysis! Ndio maprofesa wa bongo
Huyu naye ni kama boga sijui. Hapishani sana na yule Dr. boga wa REDET.
 
Lipumba its true tunataka mchango wako katika kulifikisha taifa a step ahead but the way I see it ...if u become a member of parliament we can benefit more than fighting for a position you will never get..
 
Mohla ya sebha
 
Hivi UKAWA hawakuwa na vigezo vya kumpata mtu atakaye peperusha bendera ya UKAWA kwenye nafasi ya rais JMT?

Kama hawakuwa na vigezo, they are hopeless na hawako tayari kuongoza nchi.

Kama walikuwa na vingezo vya kumpata mpeperusha bendera ya UKAWA na sasa kuna chama hakitaki kufuata hivyo vingezo, then they are hopeless na hawako tayari kuiondoa CCM madarakani.

What is the solution? Stick kwenye vigezo mlivyokubaliana tangu mwanzo.

Kama kuna chama hakitaki, vunjeni huo muungano kila chama kiende kivyake. Lakini one thing vyama vyote mnavyounda UKAWA msahau kabisa kuishinda CCM. Huo ndio UKWELI mchungu.
 
Hivi UKAWA hawakuwa na vigezo vya kumpata mtu atakaye peperusha bendera ya UKAWA kwenye nafasi ya rais JMT?

Kama hawakuwa na vigezo, they are hopeless na hawako tayari kuongoza nchi.

Kama walikuwa na vingezo vya kumpata mpeperusha bendera ya UKAWA na sasa kuna chama hakitaki kufuata hivyo vingezo, then they hopeless na hawako tayari kuiondoa CCM madarakani.

What is the solution? Stick kwenye vigezo mlivyokubaliana tangu mwanzo.

Kama kuna chama hakitaki, vunjeni huo muungano kila chama kiende kivyake. Lakini one thing vyama vyote mnavyounda UKAWA msahau kabisa kuishinda CCM. Huo ndio UKWELI mchungu.
Hatutaki kusema mengi kuhusu huyu Lipumba, ni mbinafsi hakuna. Unakumbuka kampeni zake za mwaka 2010. Kuna CD ilimrekodi anavunja miiko ya umoja wa nchi yetu. Leo hii inajipa umaarufa wa kupandikiza kama Lowassa. Hovyo kabisa Lipumba.
 
Lipumba na Seif ni wapenda madaraka, Tangu chama kianzishwe mpaka leo wao ndio viongozi utafikiri chama ni chao wao wawili
 
Back
Top Bottom