Lipumba: Usaliti unaitafuna CHADEMA, nikirudi watakwisha

Mwenyekiti halali wa chama cha siasa cha upinzani cha CUF leo amempasha Katibu Mkuu wa chama hicho kwamba hayupo tayari kuona chama hicho kinauzwa kwa CHADEMA ama kwa Lowassa.


Chanzoo: ITV habari.
 
Sasa huyu Pro Pesa naona kaishiwa kabisa , anajitafutia umaarufu kupitia CHADEMA anafikiri ataweza , alishindwa enzi hizo akiwa na nguvu ni sasa anapepesuka ndio ataweza ? Mzee Mnafiki sana Maalim kamuumbua jana kumbe alimwambia Lowassa aende NCCR-Mageuzi ...kwa sababu ya wivu wake dhidi ya CHADEMA .....
Haya yote ni ushabiki ambao hata kwenye khanga zimo. La msingi zama kwenda ajenda za Lipumba alizoongea na ujibu hoja. Au discuss basi. Unaruka hoja unakimbilia ushabiki. Ulofa kweli huuu
 
Hapo Akili zinaanza kurejea sasa,kumbe anatambua kabisa kwamba si m/kiti wa CUF??Mtungi naye asikie hilo sasa..Kuhusu akirejea CHADEMA watamtambua,nathubutu kusema ANAJITEKENYA hapo
 
Kajitekenya....sasa anacheka....
Kujifungia kote kule buguruni, kumbe bado anajua hajarudi.
Usaliti wake kwa chama chake cha zamani hauoni!!!
Mbona yeye ndie alikuwa mpiga debe wa mwanzo sana kwa Lowasa.
Usiombe kushikiwa akili kabisa.
 
Hawakubali yeye na nani? Kwani siku ile wakati wanamkaribisha Lowasa yeye si alikuepo???? Muambie aende akalee wajukuu
 
Lipumba alimpokea Lowassa na akasema mwenye uthibitisho kama Lowasa ni fisadi aende mahamakani, akadai tatizo ni mfumo na sio mtu.

Lipumba akatangaza kujiuzulu wadhifa maana ameona dhamira yake inamsuta kumleta Lowasa awe mgombea urais akaiacha CUF katikati ya mapambano.

Baada ya kuona uchaguzi umekwisha na akaona chama chake kimepiga hatua kuliko hata alivyokua yeye sasa anataka kurudi kwenye nafasi yake!

Lipumba uliondoka mwenyewe na aliekufanya uondoke ni Lowasa ambae bdo yupo ndani ya UKAWA hvyo kama akirudi maana yake ataiondoa CUF ndani ya UKAWA, umoja huo uliowasaidia leo anaukana!!!!

Huyu ni Prof wa uchumi hesabu za siasa haziwezi angalia anavyojidhalilisha! Ni heri angebaki na uchumi wake ili kulinda heshima yake.
 
Profesa Ibrahim Lipumba Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) aliyefutwa uanachama na Baraza Kuu la Uongozi Taifa la Chama hicho, amesema usaliti uliofanywa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwa aliyekuwa Katibu Mkuu wake Dkt. Wilbroad Slaa na kukiuka makubaliano ya Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) katika kipindi cha kampenzi za uchaguzi mkuu wa 2015 utakigharimu chama hicho.

Lipumba ameyasema hayo Novemba 26, 2016 katika mkutano wake na baadhi ya viongozi wa kata za Jimbo la Temeke kwenye Ukumbi wa Sunrise ulioko Tandika jijini Dar es Salaam.

“Usaliti wa Chadema kwa Dkt. Slaa utaendelea kuigharimu na ndio maana hawataki nirudi katika wadhifa wangu na nikirudi watakwisha,” amesema.

Amedai kuwa, usaliti wa Chadema umesababisha upinzani kupokonywa ajenda yake ya ufisadi na kuruhusu Rais John Magufuli kuitumia ajenda hiyo kumaliza nguvu ya upinzani.

“Rais Magufuli ametunyang’anya ajenda ya kusimamia ufisadi, leo hii Chadema hawana ajenda ya kupinga ufisadi kwa sababu ya kumuasi Slaa,” amesema.

Kuhusu Ukawa Lipumba amedai kuwa, baadhi ya viongozi wa Chadema wanautumia umoja huo kuiua CUF Bara huku akituhumu baadhi ya viongozi wa CUF kuwa wananjama za kukiuza chama hicho.

Aidha, amesema alifikia hatua ya kujizulu mwezi Agosti mwaka jana uenyekiti wa CUF kwa madai ya kutokubaliana na hali ya kuwa mpiga debe wa Edward Lowassa aliyekuwa mgombea wa kiti cha urais kwa tiketi ya Chadema na mwamvuli wa Ukawa.

“Nilikataa kuwa mpigadebe wa Lowassa, niligombea urais mara nne leo hii nisimame kumpigia debe Lowassa? Ambaye kwenye orodha ya majina ya mafisadi jina lake lilikuwa namba nmoja. Nisingeweza fanya hivyo nikaona bora kujiudhuru,” amesema.
akalale mbele hivi haoni aibu?
 
Back
Top Bottom