Lipumba: Usaliti unaitafuna CHADEMA, nikirudi watakwisha

1480424054690.jpg
 
Utakua umelipwa wwwe ili utoe uharo huu. Hivi unajua suala la uchunguzi kuwa linakua na mapana yapi. Hivi unajua kazi ya uchunguzi inayofanywa na vyombo vya dola huwa inafanyikaje. Hivi ni nani kati yao ambaye ameshapitia mafunzo ya utaalam wa uchunguzi. Unataka kutuletea habari za kitoto kamanda. Hii ni sawa umemwona mwanao anaiba mboga ukamwita. Ukamuuliza umekula mboga? Akisema hajala huna ushahidi kuwa atakua amekula sababu amesha imeza. Sasa ndio story yako ya kitoto. Hivi unadhan chadema kumweka huyo mzee kwwnye list of shame walikurupuka tu bila walau kutafuta ukweli. Na ndio maana kila kiongozi ana statement yake.
Mbowe.-Lowasa hasafishiki
Mbowe-ni janga kuwa na rais bubu kama huyu
Lema-lowasa ni fisadi
Kubenea-ndio kabisa na magazeti yake
Msigwa- atakayem support lowasa akapimwe akili.
Na matamshi meeeengi kwazaidi ya miaka nane. Hivi unachambua habari hii. Unalalamika eti maelezo yamekua yakitolewa watu hawaelewi. Hayo maelezo nenda kamweleze mwanao nyumbani kamanda. hatudanganyiki. Hapa suala lilivyofanywa ni kuwa aliambiwa ajiuzuru ili makubwa yasijemkuta. Na akajiuzuru. Wamesitiri mzee wa watu tu lakini msilete habari fyongo kama hizi
haahaaaa kiongozi usipanic hoja yangu ni kuwa hao wote iwe chadema au ccm walimbana kutumia ushahidi uliokuwepo kipindi kile sasa kama lowasa alijitetea mbele ya chadema kwa ushahidi mpya ulitaka wamkatae?? lowasa lazima aliogopa kumwangusha kikwete akaona bora atolewe kafara kuiepusha ikulu na lawama za watanzania maana wote tunajua kabisa thr is no way scandal kama escrow au richmond pesa zipigwe rais asijue no way so pale collective responsibility ikawa ya lowassa na yye ameshalieleza hilo mara nyingi. Sasa kama mtu kajitetea kwa ushahidi ambao alionyesha kamati kuu jinsi gani rais ndo alishirki kushinikiza mkataba wa richmond ukubaliwe unataka tuendelee kumuita fisadi???? kamanda twemde pole pole tuko hapa kueleimishana sio kushindana natumaini umenielewa
 
Hawakubali yeye na nani? Kwani siku ile wakati wanamkaribisha Lowasa yeye si alikuepo???? Muambie aende akalee wajukuu
Keshafafanua awali walichompokea hakikuwa kugombea urais bali kuja kuupa nguvu upinzani na wenyeviti wa CCM 19 ambao angekuja nao kumuunga mkono Mgombea atakayepitishwa na UKAWA ambaye alitegemewa ni Slaa ...swali alilokomaliwa ni wako wapi hao viongozi wa CCM na Mbowe na Seif wakaipiga kimyakimya katika ule mtindo maarufu KUBADILI GIA ANGANI ...tuwe na KUMBUKUMBU
 
Profesa Ibrahim Lipumba Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) aliyefutwa uanachama na Baraza Kuu la Uongozi Taifa la Chama hicho, amesema usaliti uliofanywa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwa aliyekuwa Katibu Mkuu wake Dkt. Wilbroad Slaa na kukiuka makubaliano ya Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) katika kipindi cha kampenzi za uchaguzi mkuu wa 2015 utakigharimu chama hicho.

Lipumba ameyasema hayo Novemba 26, 2016 katika mkutano wake na baadhi ya viongozi wa kata za Jimbo la Temeke kwenye Ukumbi wa Sunrise ulioko Tandika jijini Dar es Salaam.

“Usaliti wa Chadema kwa Dkt. Slaa utaendelea kuigharimu na ndio maana hawataki nirudi katika wadhifa wangu na nikirudi watakwisha,” amesema.

Amedai kuwa, usaliti wa Chadema umesababisha upinzani kupokonywa ajenda yake ya ufisadi na kuruhusu Rais John Magufuli kuitumia ajenda hiyo kumaliza nguvu ya upinzani.

“Rais Magufuli ametunyang’anya ajenda ya kusimamia ufisadi, leo hii Chadema hawana ajenda ya kupinga ufisadi kwa sababu ya kumuasi Slaa,” amesema.

Kuhusu Ukawa Lipumba amedai kuwa, baadhi ya viongozi wa Chadema wanautumia umoja huo kuiua CUF Bara huku akituhumu baadhi ya viongozi wa CUF kuwa wananjama za kukiuza chama hicho.

Aidha, amesema alifikia hatua ya kujizulu mwezi Agosti mwaka jana uenyekiti wa CUF kwa madai ya kutokubaliana na hali ya kuwa mpiga debe wa Edward Lowassa aliyekuwa mgombea wa kiti cha urais kwa tiketi ya Chadema na mwamvuli wa Ukawa.

“Nilikataa kuwa mpigadebe wa Lowassa, niligombea urais mara nne leo hii nisimame kumpigia debe Lowassa? Ambaye kwenye orodha ya majina ya mafisadi jina lake lilikuwa namba nmoja. Nisingeweza fanya hivyo nikaona bora kujiudhuru,” amesema.
"...ndiyo maana hawataki nirudi kwenye wadhifa wangu...."
alichosema Lipumba kwenye mkutano na Wana-CUF ambao upo you tube ni:-
"....Seif anadanganywa na Waganga ..aje hapa Ofisini nimpangie kazi za kufanya tuijenge CUF Bara kwani Zanzibar tumeshamaliza..sitakubali CUF iuzwe kwa CHADEMA au LOWASA ...katika kipindi hiki kama Mwenyekiti na Mungu akipenda mpk 2019...sitakubali''
 
Sababu za Lipunba Inabadilika kadri muda unavyosogea .
Tatizo ni Urais wala sio ufisadi

Walikuwa wabagombania nafasi ywye na silaa wakakosa .

Kwanini ukubali nguvu ya mtuhumiwa wa fisadi ikusaidie kuingia ikulu kama wewe unachukia ufisadi ?

Hongera kumshughulikaiaje ?
 
naanza kupoteza imani na mtandao wa jf ni mipasho kama taarabu mawazo yanayo fanana siasa yetu itakua kweli mkubwa mboe maji ya shingo, zito at least anajitoa muhanga tunadai ccm lipumba na tegemea vichwa vinne pamoja na mbatia huenda wskalishambulia chama kongwe,sie ni ukanda tu xaxa hao watu wakanda ote wataisha lupango,mi naona kwa hawamu hii umoja unahitajika nakama kuna ajenda nyuma ya pazia basi ccm wataongoza mpaka tutaomba po
 
Huyu professor kamwe hatakuja kufanikiwa kuwa hata waziri mkuu, sembuse ya kuwa Rais.
 
da hatari kumbe hakuna haja ya kusoma kana hawa type ya huyu bwana ndio vichwa vya hii nchi bora niendelee kulima huku kijijini kwangu sengerema.
 
Mwanakijiji Alishawahi Kuonya Chadema Kujiunga Na Vyama Vingne Wasimame Km Wao Sbb Walishajijenga Hawakumsikia Akaja Akawashauri Wasijewakamchukua Luwasa,leo Ndyo Hayo Chadema Kwshney,hawajui Wanasimamia Wapi
 
Back
Top Bottom