Lipumba: Sina mpango wa kuhama, bila mimi CUF haipo

Lipumba: Sina mpango wa kuhama, bila mimi CUF haipo

Ninaomba anayemwelewa Lipumba anisaidie. Tatizo lake ni nini? Anachotaka ni nini hasa? Kama CUF ni yeye, na cuf hawamtaki, na bila yeye cuf haipo, kwa nini asianzishe chama kingine hao ambao wanamtegemea yeye wamfuate ili iwe mbadala wa cuf inayokufa bila yeye?
PRO.. LIPUMBA......... unaitwa ACT WAZALENDO NENDA watu wameisha kujua wewe si mwenzao.
 
Alafu mtu kama huyu anajisumbua kugombea urais..

Mkimpa nchi si atawaambia bila mimi Tanzania haipo??
 
Lipumba kurudi uenyekiti cuf ameona mbali sana ,

Na lipumba kurudi uenyekiti cuf ni pigo kubwa kwa chadema katika harakati zao kisiasa kuelekea 2020.

Profesa alishagundua mchezo waliochezewa nccr ndani ya ukawa 2015 hadi leo wana mbunge mmoja huenda ikatokea kwa cuf 2020 wakapotezwa kisiasa kama walivyopotezwa nccr kisiasa na kama si mbatia kupata jimbo moja nccr ingekuwa ishakufa kisiasa. .....

Hebu fikiria majimbo 30 yote ya NCCR yote chadema walisimamisha kasoro kwa kafurira na mbatia tuu , .....

Hivo CUF kuishi CHADEMA wanatakiwa wawe makini sana maana chadema michezo ya kisiasa
 
Kwa sasa cuf hii taji kuongozwa na lipumba kwa sababu kapoteza sifa yakua kiongozi
 
huyu ni profesa wa aina gani..? eti bila yeye cuf hakuna..mbona alikimbia..lakini cuf ipo tena imepamba moto mpaka analialia arudi..
 
Kwa muda sasa ndani ya chama cha wananchi CUF kuna fukuto linaloendelea ambalo linasababisha mgogoro mzito miongoni mwa wanachama wa chama hicho. Sababu kubwa ni kuibuka pande mbili miongoni mwa wanachama, ambao lipo kundi linaloongozwa na katibu mkuu wa chama hicho (inasemekana) likipinga kurudi kwa aliyekuwa mwenyekiti ambaye amejiudhuru mapema kabla ya uchaguzi mkuu uliopita na kundi jingine hasimu likiongozwa na baadhi ya wabunge akiwemo naibu katibu mkuu bara (pia inasemekana).
Sasa huenda wote hawa wana nia ya dhati ya kuiona CUF ikipiga hatua. Lakini siyo kwa style hii wanayokwenda nayo, wanazidi kukipasua chama na kuwagawanya wananchi.
My take:
Iwapo prof. Lipumba utakubali kukaa kando mgogoro utakwisha, kwani ulishajiudhuru mzee wangu, watu tulikuelewa sana.
Pia nataka nikueleze tu, ukiona wewe mpinzani unafanya jambo na Lumumba wanashabikia, jua suala hilo siyo afya kwako.
Asante.
 
Hivi huyu ndie miaka ile alikua anataka achaguliwe kuwa rais? Hivi angekubal kubanduka ikulu kwel? Aiseeee.. tusithubutu kuwapa hawa jamaa nchi
 
Kazi ya ushauri wa uchumi...imemshinda....atushauli nini kifanyike hali ya uchumi mbaya.....
 
Hivi huyu ndie miaka ile alikua anataka achaguliwe kuwa rais? Hivi angekubal kubanduka ikulu kwel? Aiseeee.. tusithubutu kuwapa hawa jamaa nchi
ndio huyuhuyu ila amevalishwa ngozi ya kondoo
sema usithubutu kumpa utawala pandikizi lolote la ccm madaraka...
 
Huwa najiuliza siku anavamia mkutano kwenye zile kurupushani angepigwa angemlaumu nani?

Lipumba utakuja kupata aibu kubwa sana ukiendelea na mission yako hii sababu mchezo unaocheza unafahamika vizuri tuu.
 
Back
Top Bottom