Mashauri,
sijawahi kuwa mwanachama wa CCM maisha yangu yote na ninamwomba mungu kila siku nisijiunge na chama hicho. Nimekuwa mwanachama wa CHADEMA toka nikiwa na umri wa miaka 16 na sijawahi kuwa mwanachama wa chama kingine chochote! Muhimu zaidi la kuzingatia ni kuwa kwetu Kigoma, CHADEMA ni zaidi ya chama cha siasa. mtu yeyote wa Kigoma mwenye akili timamu hawezi kuhama CHADEMA au hata kuwa pandikizi la CCM ndani ya CHADEMA. Kwa Kigoma, CHADEMA ni 'movement' na msaliti wa movement hutengwa - tazama Dkt. Kabourou.
Suala la Dowans ni suala la msimamo wa mtu binafsi. Nihukumiwe kwa hilo hilo!
Ni msimamo thabiti kwamba unakubali kuwa kwa suala la Dowans uhukumiwe kwa utashi wako wewe binafsi!! As long as your conscience is very clear on the Dowans issue you can soldier on; bahati mbaya wengi walipata hisia kuwa kijana wetu tulikwisha kupoteza kwa VIJISENTI vya Rostam!!